Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Yule mchezaji kipenzi wa Gang Chomba, Ronaldinho (i.e. Ronaldo Mdogo) amegoma kustaafu kusakata gozi. Pamoja na kiwango chako kuisha, mkongwe huyo bado anang'ang'ania kulisakata kabumbu japo magoli anayoyafunga sasa siyo yale ya kiwanjani bali ni ya 'kule'. Amesahau kwamba wachezaji huja na wachezaji huondoka.
Mshauri Mtaalamu wa 'Mchezo Mzuri', Comredinho Companero, anamshauri gwiji huyo 'zilipendwa' atandike daluga. Kuna vitu vingi ambavyo wachezaji wastaafu wanaweza kufanya. Mathalan, wanaweza kuwa wachambuzi mahiri wa soka ila tu wasijiabishe kama nguli wa zamani, Thiery Henry, alivyojidhalilisha kwa kukandia ushangiliaji wa bao murua la Chicarito.
Ronaldo Moreira Asis (a.k.a. Gaucho) shurti sasa aache vitu viwili vinavyomsisimua na visivyoendana alivyovifuata huko Mexico, yaani kukata viuno na kusakata kandanda. Awaachie uwanja vijana waliobukia na wanaolekea kumzidi pia - akina Edin Harzard na Lionel Messi ambao hata mchawi wa soka mstaafu, Zinadine Zidane (Zizzou), amekiri wanamvutia zaidi.
Rejea:
Ronaldinho: I'm not retiring - Goal.com
Tom Marshall: Time running out for Ronaldinho in Mexico - Goal.com
Ronaldinho Reveals Why He Moved to Mexico: To Win Trophies...and Girls | Bleacher Report
Ronaldinho proves he is the ladies' man of Mexico - Mirror Online

Last edited by a moderator: