Goli la Gaucho wa Gang!

Goli la Gaucho wa Gang!

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
Yule mchezaji kipenzi wa Gang Chomba, Ronaldinho (i.e. Ronaldo Mdogo) amegoma kustaafu kusakata gozi. Pamoja na kiwango chako kuisha, mkongwe huyo bado anang'ang'ania kulisakata kabumbu japo magoli anayoyafunga sasa siyo yale ya kiwanjani bali ni ya 'kule'. Amesahau kwamba wachezaji huja na wachezaji huondoka.

Mshauri Mtaalamu wa 'Mchezo Mzuri', Comredinho Companero, anamshauri gwiji huyo 'zilipendwa' atandike daluga. Kuna vitu vingi ambavyo wachezaji wastaafu wanaweza kufanya. Mathalan, wanaweza kuwa wachambuzi mahiri wa soka ila tu wasijiabishe kama nguli wa zamani, Thiery Henry, alivyojidhalilisha kwa kukandia ushangiliaji wa bao murua la Chicarito.

Ronaldo Moreira Asis (a.k.a. Gaucho) shurti sasa aache vitu viwili vinavyomsisimua na visivyoendana alivyovifuata huko Mexico, yaani kukata viuno na kusakata kandanda. Awaachie uwanja vijana waliobukia na wanaolekea kumzidi pia - akina Edin Harzard na Lionel Messi ambao hata mchawi wa soka mstaafu, Zinadine Zidane (Zizzou), amekiri wanamvutia zaidi.

Rejea:

Ronaldinho: I'm not retiring - Goal.com

Tom Marshall: Time running out for Ronaldinho in Mexico - Goal.com

Ronaldinho Reveals Why He Moved to Mexico: To Win Trophies...and Girls | Bleacher Report

Ronaldinho proves he is the ladies' man of Mexico - Mirror Online
 
Last edited by a moderator:
udadisi bana dah...
unaambiwa hivi Dinho Magic awapo uwanjani basi Malaika huacha shughuli zao huko Mbinguni na kuanza kumuangalia na kumshangilia..
 
udadisi bana dah...
unaambiwa hivi Dinho Magic awapo uwanjani basi Malaika huacha shughuli zao huko Mbinguni na kuanza kumuangalia na kumshangilia..

uchawi hauvuki bahari, vivyo hivyo 'magic' hai-cross 'age' maana wakati ukuta; muda ukifika shurti uachie ngazi, urithishe mikoba wengine - dinho aache kuwa king'ang'anizi kama mugabe!

na wewe tafuta mchezaji mwingine wa kumshabikia, edin harzard atakufaa maana una chuki binafsi na soccer whiz, the one only football magician messi!

kama vipi tuachie soka siye, wewe nenda kwenye jukwaa la lasagna na pizzeria!
 
Udadisi;

Watoto mliojua soka juzi mna shida sana.... Kwa hiyo lengo la hii thread yako ni kuleta ubishi wenu wa kitoto wa siku zote? Narudia tena..... Hajawai tokea Kama Ronaldinho Gaucho, pengine kuna siku mungu atatushushia nabii mwingine wa soka.. tuendelee kuomba
 
Hujui Kila zama na kitabu chake na nabii wake?

Zama za Gaucho zimepita - sasa ni zilipendwa!

Leo ni zama za kina Harzard, Neymar na Messi!
 
Udadisi;

Hao wote wa kawaida sana... hawajafikia hata kiwango cha kina Malota Soma 'Ball Jagler", Hamis Gaga "Gagarino" au Hussein Amani Masha enzi hizo!! Ndio maana hatuwaongelei kina De Lima, Pavel Nedved, Rivaldo, Batistuta, Asprila, George Weah, Cantona etc... kwa sababu wote hao walikua wakali kwa enzi zao.

Gaucho is out of this world... kuna watu huwa najaribu kuwaweka kwenye mzania wa Gaucho nao ni Zinadine Zidane Zizzou" na Diego Armando!! hawa kina Messi na CR7 ni just above average
 
Last edited by a moderator:
Soccer pia ni hobbie kwa hiyo dihno pia anacheza just for fun! Bora aendelee kucheza asije ishia kubwia unga kama maradona
 
Udadisi;

Hao wote wa kawaida sana... hawajafikia hata kiwango cha kina Malota Soma 'Ball Jagler", Hamis Gaga "Gagarino" au Hussein Amani Masha enzi hizo!! Ndio maana hatuwaongelei kina De Lima, Pavel Nedved, Rivaldo, Batistuta, Asprila, George Weah, Cantona etc... kwa sababu wote hao walikua wakali kwa enzi zao.

Gaucho is out of this world... kuna watu huwa najaribu kuwaweka kwenye mzania wa Gaucho nao ni Zinadine Zidane Zizzou" na Diego Armando!! hawa kina Messi na CR7 ni just above average

Mosi, mtake radhi Ronaldo wa Ukweli. Ilibidi Gaucho aitwe Ronaldinho, yaani Ronaldo Mdogo, maana kulikuwa na Ronaldo Mkubwa ambaye Wabrazili walimuitwa Tukio la Ajabu Sana (The Phenomenon). Hakuwa na mfanowe na Dinho alikuwa akitamani sana kufanana naye! Batistuta alishakiri kwamba Football is Ronaldo, akimaanisha bila Ronaldo hakuna mpira.

Pili, Dinho mwenyewe amekiri zaidi ya mara moja kwamba Messi ni zaidi. Ya nini kuongelea mate ilhali wino huu hapa upo: "He [Messi] has been playing at a level we've never seen anyone else playing before" (Yeye Messi amekuwa anacheza katika kiwango [cha juu sana] ambacho hatujawahi kukiona mchezaji mwingine yeyote [yaani Pele, Maradona, Zinadine, Ronaldo, Ronaldinho na wengine wote] akikicheza kabla" (http://www.ronaldo7.net/news/2012/604-ronaldinho-cristiano-ronaldo-is-making-history-but-messi-is-the-best-in-the-world.html)

Tatu, lazima Dinho alaumiwe sana kwa kutotumia ujana wake vizuri - alikuwa na fursa ya kucheza kwa kiwango cha juu mno kwa muda mrefu ili kukata kabisa kiu yenu mashabiki wake kama asingeendekeza michezo mingine; hili wachambuzi wote mahiri wa soka tunalitambua kasoro nazi wake, Gang Chomba; hebu msome huyu pundit:

"No one doubts that Ronaldinho is now far from his prime and it has to be said that it was a true shame that such a talented player couldn't manage to perform at the high level for more years than he did" [Hakuna ubishi kwamba Ronaldinho sasa amekwisha na ni jambo la aibu kubwa kwamba mchezaji mwenye talanta kubwa kiasi hicho hakuweza kucheza katika kiwango cha juu kwa muda mrefu kuliko alivyocheza" (Ibid).

Mkuu haya maandiko yenu wapenzi wa Messi tulishayazoea.. kwa sisi tunaopenda soka na vimbwembwe vyake wala hatupepesi macho wala kupindisha maneno. Gaucho alinifanya nikaipenda soka zaidi na zaidi na zaidi
 
uchawi hauvuki bahari, vivyo hivyo 'magic' hai-cross 'age' maana wakati ukuta; muda ukifika shurti uachie ngazi, urithishe mikoba wengine - dinho aache kuwa king'ang'anizi kama mugabe!

na wewe tafuta mchezaji mwingine wa kumshabikia, edin harzard atakufaa maana una chuki binafsi na soccer whiz, the one only football magician messi!

kama vipi tuachie soka siye, wewe nenda kwenye jukwaa la lasagna na pizzeria!

hakuwepo, hayupo na hatokuwepo wa kumrithi Dinho Magic...

nakili hii na uiweke akilini.
 
kuna mtu aliwahi kusema hapa kila siku tunawapata akina Nesi wapya, Cristiano wapya, Hazard wapya ila hakuna siku utakayosikia eti New Gaucho....

period
 
kuna mtu aliwahi kusema hapa kila siku tunawapata akina Nesi wapya, Cristiano wapya, Hazard wapya ila hakuna siku utakayosikia eti New Gaucho....

period

mkuu awa waloangalia mpira kuanzia mwaka 2009 wana shida kweli, iv mtu mwenye akili timamu unamlinganishaje gaucho na hazard, messi na cr7
huo ni utovu wa nidhamu.
 
Gang Chomba, unamshibikia mtu mpaka unambishia mtu huyo? Hebu msikilize Ronaldinho mwenyewe na vinara wenzie wakimwongelea mtu alipachikwa jina la TUKIO LA AJABU SANA (THE PHENOMENON):

1.Zidane: "Ronaldo is my idol, he is the best player with whom I played together and against".
2.Kaka: "Ronaldo is the second, after Pele".
3.Maldini: "Only Maradona is better than Ronaldo, but Ronaldo is the top scorer goals that I have seen."
4.Pato: "Ronaldo is the best player of all time, he is a phenomenon."
5.C.Ronaldo: "Ronaldo is my idol, I want to be like him."
6.Ibrahimovic: "Ronaldo is my childhood idol, I search comrades called" Ronaldo "when played on the road."
7.Neymar: "Ronaldo is the best of all time."
8.Ronaldinho: "Ronaldo is my idol and the best player in the history of football."
9.Fabio Capello: "Ronaldo is the best player I've trained".
10.Messi: "Ronaldo was a" Hero "for me, when I was a femije.Une I learned a lot from him and when I met him for the first time in Brazil has brought to mind many memories."
11.Maradona: "Ronaldo is" Master "Football".
12.Pele: "You can not compare Ronaldo with anything, he is absolutely the best."
13.Benzema: "Ronaldo is my model, I came to Real because he played here and I want to become like him."
 
Last edited by a moderator:
Abdulwahid , kha na wewe unabishana na Ronaldinho mwenyewe? Hebu msome kwa tuo:

Ronaldinho: "Messi is the best in the world right now. He has been playing at a level we've never seen anyone else playing before. I'm always proud of speaking about Leo, because I was right there with him, when he started his professional senior career in Barcelona. He's now the best football player in the World and that just makes me tremendously happy!", said Ronaldinho as he put a big smile on his face, with his traditional big teeth standing out, as it is usual in him.

Ronaldinho
: "I still remember the game where Leo Messi scored his first senior goal. It was a very special moment and I still recall having assisted him for that goal!", noted the Brazilian, when referring to a home game between Barcelona and Albacete, back in May 2005. Ronaldinho: "It was an honor to live and share that moment with him.Messi knows I'll always hold a place for him in my heart!", stated the 32-years old former Balon d'Or winner, as he closed his interview to ESPN Soccernet.
 
Last edited by a moderator:
Gang Chomba mwambie Blaza wako astaafu.. awaachie akina Leo wenye nguvu walisakate kabumbu..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom