Goli la mkono 2015

Goli la mkono 2015

Joined
Apr 25, 2013
Posts
19
Reaction score
29
Hiki ni chumba chenye kompyuta kilichotumika kujumlishia matokeo mwaka 2015, chumba hiki maalumu cha IT kipo MASAKI JIJINI DSM, Kwa hakika hawa ndio walio msaidia kuhakikisha Rais Magufuli anaingia madarakani kwa namna yeyote ile.

Katibu mkuu wa CCM Kanari Kinana pamoja na uzee hakuweza kulala na wakati mwingine aliwapa kampani vijana hawa akina Makamba katika kujumlisha matokeo ya mgombea wao wa CCM Dr. Magufuli.

Chumba hiki ndicho kilichotumika kujumlishia matokeo ya mgombea Urais wa CCM mwaka 2015, matokeo yote kutoka kila pembe ya Tanzania yalijumlishiwa hapa.

Kwa lugha nyepesi masuala yote ya goli la mkono lilikuwa likitangazwa na Nape lilifungiwa hapa kwenye hiki chumba cha IT kilichopo masaki jijini DSM, mainjia wakubwa wakiwa mzee Kinana, Januari Makamba na mara chache Nape Nnyauye alikuwa akija kwenye chumba hiki kuangalia kama goli la mkono linaingia vizuri.

Pamoja na kuwa na makompyuta kibao mezani lakini muda wote walikuwa wakifuatilia runinga kujua nini kinachojiri huku chanell yao ikiwa imewekwa ITV ...Kwa hakika wazee hawa walifanikiwa kufunga goli la mkono.

Katika chumba hiki cha goli la mkono hakukuwa na Paul Makonda, Mrisho Gambo, Cyprian Musiba wala Ally Happi, chumba hiki cha goli la mkono kilikuwa na hizi njemba, Cde Kinana, J. Makamba na mara chache Nape Nnauye.

Ajabu ni kuwa watu hawa walio muingiza HAWAFU MWENYE NGUVU wanadharauliwa, wanatukanwa, na kudaiwa kuwa wanamhujumu Rais Magufuli na mhuni kama Cyprian Musiba, sio jeshi la polisi, sio chama cha Mapinduzi wala chombo chochote cha ulinzi kimethubutu kumtia nguvuni Mhuni Musiba.

Kijana mpumbavu hajaishia hapo ameendelea kuwatusi viongozi wengine wastaafu akina Bernard Membe, Mzee Kikwete akiwaita ni majizi na hawakufanya lolote enzi za utawala wao huku akisema mkombozi Magufuli ameingia kuwatetea anao waita.

Mtu huyu asiye na haya anaendelea kutoa lugha chafu kwa viongozi wa upinzani na kuwatuhumu bila kuchukuliwa hatua yeyote.

Poleni sana Mzee Kinana na January Makamba kwa kufanya kazi kubwa hata kutumia goli la mkono ili hawafu mwenye Nguvu ashinde lakini leo hii hawafu anawaacha mtukanwe, madharirishwe na mhuni kama Musiba. ©Kumbusho Dawson
 

Attachments

  • IMG_20190719_181953_331.jpg
    IMG_20190719_181953_331.jpg
    75.8 KB · Views: 41
  • IMG_20190719_181949_089.jpg
    IMG_20190719_181949_089.jpg
    65.1 KB · Views: 39
  • InShot_20190719_182132832.jpg
    InShot_20190719_182132832.jpg
    205.1 KB · Views: 44
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] Tanzania bhana.

Sasa kama ni chumba cha siri waliweka hiyo picha ya Chagua Magufuli kwa minajili ipi na wote wanajua kilichowapeleka humo ndani.

Vipi kama ingetokea wakasanukiwa wanakutwa na vipicha ukutani vya mgombea!!!!!
 
Back
Top Bottom