Naomba niwe muwazi .
Mimi ni mdau wa Simba Sports Club .
Goli la Ajibu ni goli zuri .
Ni goli alilolifunga akiwa hana upinzani wowote toka kwa walinzi wa Mbao FC , alikuwa na muda wa kutosha kufanya alichofanya . Akili na mwili wake vilikubaliana .Pia tunapomsifia Ajibu tusisahau pia hata goli la kichwa la Daud lilikuwa zuri .
Pamoja na ukweli huo , natofautiana sana maoni na wanailiita goli la msimu .
Msimu nd'o umeanza . Bado magoli mengi mazuri pengine kuliko hilo la Ajibu yatafungwa .
Yatafungwa na wachezaji tofauti au pengine hata huyo Ajibu bado anaweza kufunga magoli mengine mazuri kuliko hilo .
Mimi nafikiri tuseme ni moja kati ya magoli bora ambayo yameshafungwa mpaka sasa kuliko kuhitimisha msimu kwa goli moja tu .
Wenye akili kubwa watanielewa na wenye akili ndogo watatoa povu .
Nawasilisha .