Goli la msimu ni la Ajibu Migomba

Goli la msimu ni la Ajibu Migomba

Umeandika kidogo sana hebu ungeza kulisifia basi khaaa
We jamaa umenichekesha sana. Ili ujue goli la Ajibu nimelifurahi sana hapo ulipo agiza kinywaji chochote utumiacho.
 
Naomba niwe muwazi .
Mimi ni mdau wa Simba Sports Club .
Goli la Ajibu ni goli zuri .
Ni goli alilolifunga akiwa hana upinzani wowote toka kwa walinzi wa Mbao FC , alikuwa na muda wa kutosha kufanya alichofanya . Akili na mwili wake vilikubaliana .Pia tunapomsifia Ajibu tusisahau pia hata goli la kichwa la Daud lilikuwa zuri .

Pamoja na ukweli huo , natofautiana sana maoni na wanailiita goli la msimu .
Msimu nd'o umeanza . Bado magoli mengi mazuri pengine kuliko hilo la Ajibu yatafungwa .
Yatafungwa na wachezaji tofauti au pengine hata huyo Ajibu bado anaweza kufunga magoli mengine mazuri kuliko hilo .
Mimi nafikiri tuseme ni moja kati ya magoli bora ambayo yameshafungwa mpaka sasa kuliko kuhitimisha msimu kwa goli moja tu .

Wenye akili kubwa watanielewa na wenye akili ndogo watatoa povu .
Nawasilisha .
 
Ajib ananifurahisha sana, mechi zote na Simba anagoma kucheza mpira wake, sijui mapenzi au anakuwa vizuri kwenye mechi average.
Ajibu anajua kuwa ni mtoto wa Simba.
Kocha Amog ndiye aliyemlazimisha kusaini Yanga fc, kwa kitendo chake cha kumuweka benchi msimu mzima yeye na Mkude.
Ajibu ni zao la Simba, kama alivyo Ngasa.
Mrisho Ngasa aliwahi kuichezea Simba, na kwenye mechi na Yanga alikuwa anajidondosha tu akifika langoni kwa Yanga na hakuwahi kuifunga Yanga hata mechi moja, na hata alipokuwa Azam fc.
Ajibu ni mwanetu hawezi kutuangusha, labda apate nafasi ya wazi kabisa.
 
Back
Top Bottom