Goli lile pale Tanga angefungwa Manula mitandaoni pangechafuka

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Sinema inaanza Steering akiwa Aish Manula. Tambala linaitwa SimbaVsPrison. Ghafla watazamaji wanaanza kumzomea Steering sababu ya;
Hafai[emoji441][emoji441]
Mpuuzi[emoji441][emoji441]
Kaisha [emoji445][emoji445]
Kauza[emoji441][emoji441][emoji441]
Fukuza[emoji3548][emoji375][emoji373]
Bora Lakred huyu kazeeka.
Lakini Jana Lakred kapigwa goli ambalo ni dhahiri ni yeye tu anayepaswa kulaumiwa maana mpira umepigwa toka mbali na Mtakatifu wa Kusini, hakukuwa na nafasi ya Beki kuokoa mpira ule wa juu, lakini cha kushangaza poor positioning ya kipa inawapa goli Coast.
Cha ajabu mpaka naandika thread hii sijaona yeyote akimlaumu Lakred. Au yeye hapaswi kulaumiwa kama Manula aliyebebeshwa lawama baada ya mabeki wote wa Kati kupigwa chenga na kudondoka. Nabaki na Manula Kwa maana ni kipa mzuri na akikosea ni kama kipa mwingine. Nadhani tumeanza kusahau makosa ya Lakred Mechi ya Zambia.
 
Manula alifungwa lile goli kwa uzembe wake hasa la kwanza dhidi ya Prison mashabiki wanacholalamika ni kweli kabisa. Goli alilofungwa jana Ayoub nadhani anapaswa asifiwe mpigaji kwa sababu kila mchezaji aliyekua anadefend wa Simba aliamini ile ni cross na sio shot kuelekea golini. Kwahiyo position ya Ayoub ilikua sahihi ila mpigaji ndio aliidanganya defense ya Simba.

BTW mi ni shabiki wa mpira nikiwa na mapenzi zaidi na Yanga
 
Manula ajifue kwanza, katoka kuuguza majeraha anakimbilia kupangwa kucheza badala ya kujiimarisha.
Amefungwa na Prison sababu ya kuzubaa golini.
Mshambuliaji anapiga pasi mdefu hadi inaaingia kwanye 18 yake yeye amesimama tu na kushangaa.

Amwangalie Diara anavyotokea mipira ya kutangulizwa.
Kuna wakati anatakiwa kucheza mpira kwa miguu yeye anataka kudaka tu kwa mikono.

Anavyo ambiwa udhaifu wake aupokee na kuufanyia kazi na sio kukasirika.
 
Mpira kama ule angeserve kama angekuwa modern goalkeeper, lakini Manula ni kipa Aina ya zamani. Anakusubiri uje ndo aokoe. Angetoka pale angepigwa chenga na maneno ndo yangekuwa mengi zaidi.
 
Ayoub hapokei bahasha zenu, tulieni dawa iingie, hata akifungwa poa tu
 
Goli alilofungwa Ayoub kwa ligi ya EPL wangeandika kajifunga, maana mpira ulikula nguzo ukawa unarudi uwanjani ndio ukamgonga kipa na kubadili muelekeo kuelekea nyavuni
 
Mpira kama ule angeserve kama angekuwa modern goalkeeper, lakini Manula ni kipa Aina ya zamani. Anakusubiri uje ndo aokoe. Angetoka pale angepigwa chenga na maneno ndo yangekuwa mengi zaidi.
Goli la Kwanza la Prison alikuwa na nafasi ya wazi ya kuuwahi mpira kabla ya mshambuliaji.
Tumeliangalia sana kwenye clips za uchambuzi.
Alikuwa anajitafakari kuwa aende au asiende.
 
Infact manula hafai hata kidogo..anahariibu sifa ya Simba sc..uto wamchukue tu
 
Sio manula tu, rejea match ya prison lawama nyingi alipewa Kennedy, lakini makosa yalifanywa na Inonga pamoja na kapombe ila lawama zote kazibebe Kennedy.
 
Sio manula tu, rejea match ya prison lawama nyingi alipewa Kennedy, lakini makosa yalifanywa na Inonga pamoja na kapombe ila lawama zote kazibebe Kennedy.
Unamlaumu vipi Inonga wakati aliteleza na kuumia pale?ulidhani kajifanyisha kuanguka na wakati kaikosa mechi ya Coastal kwa kuumia kule?Ungekuwa umewahi kucheza japo mpira ungeelewa
 
Manula kafungwa goli 2 hakuwa na save yoyote kwenye match Ile....

Ayubu anafungwa ila best saves unaziona ....rejea game ya Jana ya arsenal Wala sidhani kuna shabiki wa arsenal wa kumlaumu keeper wa arsenal ....(Amechoma na amesave sana kuhakikisha timu inapata ushindi)

Rejea match ya Simba vs Jkt .....Ayoub kafanya save ngapi mpaka tukashinda Ile game......
 
Unamlaumu vipi Inonga wakati aliteleza na kuumia pale?ulidhani kajifanyisha kuanguka na wakati kaikosa mechi ya Coastal kwa kuumia kule?Ungekuwa umewahi kucheza japo mpira ungeelewa
Labda haumfahau vizuri Inonga, aliumia nini pale kama sio kutaka aoenekane hakuhusika na mistake
 
Labda haumfahau vizuri Inonga, aliumia nini pale kama sio kutaka aoenekane hakuhusika na mistake
Lini Inonga alijifanyisha kuumia na kukosa mechi?Unadhani kuna mchezaji anapenda kukosa mechi kwa sababu zozote zile?labda kama ile mechi ulitazama kwenye TV ya Chogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…