Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

Katika kutapatapa kwake Msekwa anasema Kuondoka kwa Mpendazoe ni kama kutoa ndoo moja ya maji kutoka mto Rufiji.

All in all he is ahead of them if at all they had any plans to expel him fro the party
 
safi sana mpendazoe ccm sio mama yako helena

safi sana
 
Kuna habari kuwa msajili wa vyama vya siasa ana maagizo kutoka kwa mkulu kuwa asikipe CCJ usajili wa kudumu mpaka baada ya uchaguzi. Na ukizingatia kuwa hataki kuruhusu suala la mgombea binafsi bado CCM wataendelea kupeta
 
Tambwe ni mtu ambae yuko tayari kusema lolote ili atimize na kupata ugali wake wa kila siku, sasa kali zaidi ni kua Tambwe hiza ndie mshauri mkuu wa maswala ya kisiasa wa mzee Makamba.
 
PJ.. usiwe na wasiwasi.. kwa chama kidogo kama CCJ kitapewa usajili wa kudumu mapema sana kwa sababu it is not to THE INTEREST OF KIKWETE to deny them! Kwa mtu anayetukuwa wahisani na wawekezaji.. atafanya kosa ambalo hawezi kulitetea..
 
Huu ni mwanzo mzuri, sasa wale waliobaki nao wafunge magoli ya haraka haraka kabla mabeki wao hawajajipanga sawa
 
Mwingine anaweza kusema “kapigwa kanzu halafu akapigwa tobo”.
Mzee, mchezaji akimpiga kanzu golikipa anakuwa anaelekea golini, sasa akipiga tena na tobo si atakuwa anarudisha mpira uwanjani badala ya kufunga !?
 
Mpendazoe F. wa 2010 ninamfananisha na Mrema A. L. wa 1995.

Tusubiri matokeo.
 
Kuna habari kuwa msajili wa vyama vya siasa ana maagizo kutoka kwa mkulu kuwa asikipe CCJ usajili wa kudumu mpaka baada ya uchaguzi. Na ukizingatia kuwa hataki kuruhusu suala la mgombea binafsi bado CCM wataendelea kupeta
Mimi mwenyewe nina wasiwasi jamaa wasijekuharibu mchakato wa kutoa usajili wa kudumu kwa CCJ.
 
Mzee, mchezaji akimpiga kanzu golikipa anakuwa anaelekea golini, sasa akipiga tena na tobo si atakuwa anarudisha mpira uwanjani badala ya kufunga !?

hujawahi kuona kitu kinaitwa "kunyanyasa"..?
 
Shida ni moja. Mpendazoe hatadhoofishwa kwa namna moja au nyingine? Tumewaona wengi tangu enzi za Mwalimu wakidhoofishwa kwelikweli akina mzee Chris KasangaTumbo, yule mzee wa CHAUSTA (Mapalala), Kolimba, Bibi Titi, akina Kadego,.......
 
CCM jamani acheni mambo ya longolongo, kama hakuwahi kuongoza hata shina,kwanini mlimpa ubunge? Me najua wabunge wengi sana hata mawaziri hawajawahi hata kuongoza katika CCM.
 
Kwa tunaoiombea nchi neema huu kwetu ni mwanzo mwema, mshikamano wowote wa wezi ni hatari kwa jamii inayowazunguka hivyo kwa vyovyote vile kutoelewana kwao ni faraja kwetu. Tunaomba yatokee zaidi ya haya!! Amina.
 

kweli haya maneno yametamkwa kama ulivyo mquote ama??
 
na wenyewe wana vituko.. sasa kama alikuwa mzigo kwanini hawakumtua au wao ndio walikuwa mzigo yeye kawatua..

Wansema eti ni sawa na maji ya mto Rufiji kupoteza ndoo moja hakuna kilichoharibika wa kautikisika?
 

True mkuu... ni kama Man U jana na Bayarn, man u walikuwa wanaongoza ugenini mpaka dakika ya 76 jamaa wakasawazisha na dk ya 90 jamaa wakaweka la ushindi. So hata mimi sijakata tamaa nadhani hata dakika ya 90 tunaweza bado kuwashinda mafisadi. Bravo Mpendazoe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…