Huu ni mwanzo mzuri, sasa wale waliobaki nao wafunge magoli ya haraka haraka kabla mabeki wao hawajajipanga sawa
..Kweli kabisa mkuu, lakini isiwe ile hadithi ya kina Lamwai, Kabourou na Njeru Kasaka...Maana sisiem ni mafia kinyama.Mpendazoe kaonyesha njia, tunasubiri na wengine wenye ujasiri wachomoke kutoka sisisem!
yaaani mpendazoe bonge la striker.....yaani kanikumbusha jana goli la pili la Bayern Munchen....eti alikuwa mzigo CCM bana yaani kama walevi wa ulanzi jinsi wanavojibu mambo ya msingi.....well done mpendazoe
Mpendazoe hajaifungaCCM goli bali amejifunga mwenyewe kwenye mechi isiyokuwa na referee.Huo umaarufu wa mpendazoe unaodaiwa na watu si chochote kwani wanaoona kama ni maarufu ni watu wa aina yake na wale wengine wanaojiita mashujaa wa kupambana na ufusadi.Lakini kama ni mkweli mbona hawajaeleza hao wanatuhumiwa na ufisadi wamefanya nini na kuthibitisha tuhuma hizo.kilichosikika ni kelele za mbwa mwoga tuu.tena kwa mtuu yeyote makini hakuna mchango wowote wa maendeleo walioufanya aidha katika majimbo yao na hata katika chama chao katika ngazi ya wilaya.Hasara walioifanya katika majimbo yao ni kujenga makundi tuu.Let them go na hao wengine.GOLI NI GOLI HATA LA MPENDAZOE NALO GOLI!
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwenye kandakanda kuna magoli yanaudhi sana na yanakera. Kuna magoli ambayo mtu unakubali tu kuwa goli hilo "halina utata" na mnajitahidi kurudisha majibu.
Lakini, wakati mwingine magoli mengine yanamfanya mtu usikie donge kooni, presha ipande na kushuka na hata kuna mengine yanaweza kufanya timu nzima muende kumzonga mwamuzi kwani goli lililokubaliwa linaonekana kama limependelewa.
Bahati mbaya goli ni goli liwe la kuudhi au kukera lakini alimradi limekubaliwa basi wakati wengine wanasikia machungu wajue kabisa ipo timu nyingine inashangilia hata kama na wao wanaona kwa kweli lile goli lilikuwa baya.
Mbunge wa Kishapu Mhe. Fred Mpendazoe kawafunga bao CCM tena bao la kuudhi, kukera, kupandisha hasira na kwa kila kipimo bao ambalo CCM ile ya zamani isingeweza kufungwa kijinga hivi. Bao alilowafunga naweza kulilinganisha na bao la "tobo" au linakaribiana na bao la kipa "kupigwa kanzu"! Mwingine anaweza kusema "kapigwa kanzu halafu akapigwa tobo".
Kujiondoa kwa Mpendazoe kutoka Chama cha Mapinduzi kwa sababu yeyote ile kwa namna aliyotoka kunatufanya tusubiri kwa hamu maelezo ya CCM ya kutufafanulia kwanini goli hili siyo goli.Chama cha Mapinduzi bila ya shaka ambacho kina wasomi na watu waliobobea katika propaganda ya uzugaji kwa maneno kinakaribiwa na wakati mgumu wa kuelezea kujiondoa kwa Mpendazoe na bila ya shaka wanachama wengine huko mbeleni.
Wameshasema eti hakuwahi kuongoza hata shina. Shem on them.
Eti alikuwa mzigo..... Lol
kama hakuwa maarufu kwanini wamjadili, Mpendazoe kaipiga Bao CCM, na ndio maana media yote TZ imehamia kwenye sakata hili, utatamani usiujue ukweli huo, lakini habari ndio hiyo.Mpendazoe hajaifungaCCM goli bali amejifunga mwenyewe kwenye mechi isiyokuwa na referee.Huo umaarufu wa mpendazoe unaodaiwa na watu si chochote kwani wanaoona kama ni maarufu ni watu wa aina yake na wale wengine wanaojiita mashujaa wa kupambana na ufusadi.Lakini kama ni mkweli mbona hawajaeleza hao wanatuhumiwa na ufisadi wamefanya nini na kuthibitisha tuhuma hizo.kilichosikika ni kelele za mbwa mwoga tuu.tena kwa mtuu yeyote makini hakuna mchango wowote wa maendeleo walioufanya aidha katika majimbo yao na hata katika chama chao katika ngazi ya wilaya.Hasara walioifanya katika majimbo yao ni kujenga makundi tuu.Let them go na hao wengine.
huyu ni mwanaume wa shoka, anatambua thamani ya utu na mali, anajua kua vyoote viujazavyo ulimwengu ni ubatili na kujilisha upepo.Nampongeza kwa ku-sacrifice ubunge na marupuru yaliyobakia. Ni wachache wanaweza kujilipua hivi manake njaa ndo imetawala.
Taratibu tu asije akakosa ubunge, afu akarudi tena CCM. Ngoja tuwasikilize wengine, halafu na sera zao. Pengine kura yangu tis time itakua ya manufaa. im not raising my hopes though.