Goli ni Goli; la Mpendazoe nalo Goli!

 
Nimetonywa na mzee wa siasa za bongo kuwa Kina Sitta, Lucas Seleri, Mwakyembe n.k wana card mbili mbili za CCM na chama kingine cha upinzani mambo yakienda kumbo wanahamia CCJ ama CHADEMA pia uchaguzi mwaka huu kutakuwa na vurugu kama la kule Kenya tena si la kikabila bali ni la kati ya wakristo na waisilamu..
 
Kwa hiyo wewe uko kundi la mafisadi unashangilia mafisadi kushinda sema tujue ili tusihangaike kujaza thread hapa uendelee kushangilia mwenyewe
 
Nakumbuka pale nyamagana tulimuzomea Nyerere alipoingia na Mkapa, lakini aliponyosha kafimbo kake kasi, mara kusi ,mara mangaribhi na mashariki, tukatuliza soka kumsikiliza.

cool.. I was there too.. fortunately as an independent observer..
 

Ngoja nisubiri nione wapinzani wako je? hasa CCJ. Lakini waliopo hadi sasa hakuna cha vurugu na ccm itateleza tu. Hope zangu nazisikilizia kwa CCJ kuona hayo unayosema kama ni kweli.
 
Ngoja nisubiri nione wapinzani wako je? hasa CCJ. Lakini waliopo hadi sasa hakuna cha vurugu na ccm itateleza tu. Hope zangu nazisikilizia kwa CCJ kuona hayo unayosema kama ni kweli.

Mhh .. ya kweli haya?
 
Kwa hiyo wewe uko kundi la mafisadi unashangilia mafisadi kushinda sema tujue ili tusihangaike kujaza thread hapa uendelee kushangilia mwenyewe

Kwenye jukwaa la washangiliaji wapo washangiliaji wa timu zote zilizoko kwenye mpambano, sasa hiyo ya kunipangia upande umeleta wewe. Ninachosema tu ni kwamba Mpendazoe ameukimbia mstari wa mbele wa mapambano ima kwa kujua au kutokujua, na nimekiri ni haki yake pia kufanya hivyo. Amewaangusha wapiga kura wake kwa sababu amewanyima nafasi ya kumtuma tena bungeni. Na hata chama cha CCJ kitakapopata usajili wa kudumu, vita itakuwa ama imeisha au mpiganaji huyu atakuwa amepoteza uwezo wake kutokana na damage aliyojisababishia mwenyewe.
 
Congo
Nilikuwa sijakuelewa kumbe kuchemsha kwa Mpendazoe kwa maana yako ni kukosa Mil.40, inavyoonekana mawazo yako yako ni finyu sana inawezekana hata huu muda unaotumia kuandika hapa JF unalipwa kwa sababu unasema labda huko alikoenda kaahidiwa zaidi, huwezi fikiria biashara nyingine zaidi ya kuwa mwana CCM?

watu tuko tofauti wakati wewe unawaza pesa wengine tanawaza maendeleo ya taifa pesa si kila kitu unafikiri Mpendazoe hakujua kuna Mil. 40 unafikiri hizo mil. 40 ni nyingi sana ukilinganisha na utu wake mbona zinapatikana tu hata bila kuwa mbunge wangapi wana zaidi ya hizo wala hatujawahi hata kuuona mlango wa bunge

mawazo mengi ya wana CCM yamepumbazwa na rushwa ya uongozi hayafikirii zaidi wao bila ya kuwa kiongozi au mbunge ndani ya chama umefulia hamjui kwamba nje ya chama kuna biashara zingine tena zinalipa ndiyo maana mko tayari kutumia mamilioni kupata madaraka ukiwemo ubunge lakini wengine hatuna hata mawazo ya uongozi tunapeta tu tena bila pressure za kupigiwa kura
 
Mpendazoe alijua hatapita kura ya maoni ndio maana amehamia upinzani.Sidhani kama atashinda uchaguzi .Zaidi ya kupiga makelele ametoa ushauri gani kuleta maendeleo ya taifa.Uamuzi alioufanya ataujutia maishani mwake.
 
Kuwakosesha wapiga kura wake uwakilishi katika kipindi hiki ambacho bunge la bajeti ndio kikao muhimu sana kilichobaki, tena mwaka wa fedha wa mwisho katika tenure yake, ni usaliti. Ni kujijali maslahi binafsi kuliko ya waliomchagua. Hajaikimbia CCM huyu, kawatosa wapiga kura wake. Angekuwa mwema huyu, angewawakilisha vema wananchi amalize mkataba wake waliompa, kisha aondoke.

Ni sawa na baba kusikia vishindo nje usiku, kisha anaikimbia nyumba na kuacha mlango wazi ilhali wanaomtegemea wako ndani! Usaliti wa dhahiri.

Hao mafisadi anaowakimbia ndio aliowaachia jimbo lake la Kishapu wajivinjari watakavyo! What a shame! And you call this patriotism! Amechemsha bana!
 
Mpendazoe alijua hatapita kura ya maoni ndio maana amehamia upinzani.Sidhani kama atashinda uchaguzi .Zaidi ya kupiga makelele ametoa ushauri gani kuleta maendeleo ya taifa.Uamuzi alioufanya ataujutia maishani mwake.
Nani kakuambia anataka ubunge huko CCJ afterall akiukosa wewe utamsaidia nini au utaisaidia nini familia yake hadi unasema ataujutia hivi ukisimama wewe na yeye mbele ya watu nani ataonekana mjutaji zaidi acheni hizo jamani
 
Mtoto wa Jakaya Kikwete, yaani Ridhiwan Kikwete amemponda aliyekuwa mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya CCM, Fred Mpendazoe na kusema hakuwa na lolote acha aende zake.

Ridhiwan alikuwa leo mkoani Shinyanga kama ambako alialikwa kama mgeni Rasmi na Mjumbe wa baraza kuu la Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) kusimika makamanda 17 wa wilaya za mkoa wa Shinyanga.

Alisema kuondoka kwa mbunge huyo toka CCM na kukimbilia chama cha CCJ kinaonyesha viongozi ambao wamekuwa mzigo kwa chama lakini pia aina ya viongozi ambao wamekuwa wakichanguliwa katika uchaguzi na wananchi kumbe hawafai.

Alisema "Mwacheni aende Mpendazoe.... wala msihuzunike, kuondoka kwakwe kusiwafanye kukosa raha, wala CCM isisikitike, wapo wengi waliondoka na chama bado kipo imara, muhimu kusonga mbele na kuendelea kudumisha mshikamano wenu”

Alisema alikuwa Mpendazoe alikuwa akifanya mambo mengi kinyume na kanuni za chama na kuwaomba wananchi kutulia na kuangalia viongozi wengine lakini akisisitiza kuwa walio makini na siyo wale wa kuja.

Hata hivyo Ridhiwan alisisitiza “Hapa tunapaswa kuangalia, tunapochagua viongozi tuchague lakini tukichagua viongozi kwa kuangalia sura au hela za mtu, tukaacha wenye moyo na msimamo wa kukitetea na kuimarisha chama kwa vitendo…, yatatokea kama ya mpendazoe".

Vijana nao walitoa Tamko lao kwa Ridhiwan wakisema;
kwa muda mrefu mwenendo mzima wa mbunge huyo ulikuwa na mwelekeo wa kukiangamiza chama ambao ulikuwa unakinzana na maadili ya Chama pia, na kuongeza kuwa alichokifanya ni uamuzi mzuri kwa vile umekipunguzia mzigo chama.

"Alikuwa kero, alishafanya mambo mengi kwa chama, siyo kwa chama tu hata katika jimbo lake lote kwa ujumla alikuwa mzigo mkubwa sana.

Hatukujua kama tuliteua mbunge asiyekuwa na uchungu na wapiga kura wake kiasi cha kuwatelekeza na kuwanyima haki yao ya kuwa na mwakilishi hasa katika kipindi hiki cha bajeti, tunaamini hakuna kitakachoharibika kwani tunatambua mshikamano wa watu Kishapu’’
 
Hajui atendalo...after all, who is he by the way!..ndo shida ya kutumia cheo cha baba...too low!
Wataachama midomo sana hawa, ngoja ianze April!
 
Ningeshangaa sana kama angesema tofauti na hayo..................LIKE FATHER......LIKE SON............. msitegemee nyoka azae sungura....hata siku moja..............
 
wataibuka wengi tu..Wiki nzima tutasikia habari za kuponda na kupongeza Mpendazoe..Boring.
 
Ridhwani ajibu tuhuma za kwamba hakumaliza shule pale Hull University baada ya kuendekeza starehe na ubishoo...kwanza yeye mwenyewe anajua ni mzigo na hizo nafasi alizopewa ndani ya UVCCM hakustahiri..ni kilaza wala hastahiri kunyooshea vidole watu wanaolitakia mema taifa letu
 
Huyu Ridhiwan ni nani? Alikuwa wapi siku zote mpaka aibuke sasa baada ya baba yake kuwa rais? Hebu kaa kando dogo, usije ukaumbuka bure. Tutaanza kukuchambua na kuanika uozo wako wote sasa hivi. Hii sio nchi ya kifalme, eti mtoto wa rais naye ajikweze na kujifanya kuwaponda watu. Unamjua Mpendazoe wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…