Goli Tatu, Alama Tatu, Soka Chafu

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Ninawapongeza watani kwa ushindi. Lakini ushindi wenu umejaa sintofahamu sana. Maana usajili wenu hauendani na aina ya mpira mnaocheza.

Yaani butua butua zimekuwa nyingi mno. Mmekosa kabisa uhatari katika lango laa mpinzani kama wenzenu Yanga.

Nadhani wengi wetu tumeona game ya Yanga pale Arusha. Licha ya changamoto ya ubora aa uwanja bado walicheza mpira safi mno.

Imagine wao ndio wangekuwa wanaanza na Geita G FC tena kwenye kapeti la Lupaso, Nina uhakika wangepiga goli zaidi ya 6 hivi leo.

Watani timu yenu bado haija settle vya kutosha, cha ajabu zaidi inaonekana hata kocha wenu bado hajapata first 11 yake. Ugonjwa ule ule mliokuwa nao last season.

Watani ninaona mkifanya vibaya sana kwenye viwanja vya nje ya Dar. Msipo badilika basi mtaiacha meza mapema tu.
 
Mkuu upo kweli? Ulipotea sana karibu,,Ila wakati mnajiuliza kuhusu Simba na kikosi chake ni bora mkajifua zaidi kule nyuma kwa kina mwamnyeto La sivyo wakati mnyama anaondoka na clean sheet nyie mnapenyezewa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hadi wamekupuuza lol.
 
Pole sana...Yaonyesha umeumia sana baada ya kushuhudia pira Udambwi udabwi jana likiambatana na ushindi wa pointi 3 goli 3 . pia ukikumbuka kilichotokea Arusha pira papatu papatu na mipenati ya mchongo mliyopewa mkakosa...inauma sana.
 
Shehe simba ni mbovu niliwaambia toka msimu mwa mwaka juzi unaanza wakabisha lakini ukweli simba ni mbovu na tutarudi hapa baada ya game 20 za ligi tena gemu za mikoani

Simba walipoishia ndipo wanapoanzia timu Haina jipya fulubeki hakuna kiungo mkabaji hakuna strikes hakuna

Huu ndio ukweli mchungu
 
Makolo bado sana kufikia level za Wananchi.. Lile Gwaride la Wananchi sio la nchi hii
 
Mkuu upo kweli? Ulipotea sana karibu,,Ila wakati mnajiuliza kuhusu Simba na kikosi chake ni bora mkajifua zaidi kule nyuma kwa kina mwamnyeto La sivyo wakati mnyama anaondoka na clean sheet nyie mnapenyezewa.
Mkuu nipo?

Nimepotea vipi mbona DerbyDay nilikiwasha humu?

Au ulikuwa katika mazingira korofi yaliyopelekea ukose kuingia mtandaoni?
 
Pole sana...Yaonyesha umeumia sana baada ya kushuhudia pira Udambwi udabwi jana likiambatana na ushindi wa pointi 3 goli 3 . pia ukikumbuka kilichotokea Arusha pira papatu papatu na mipenati ya mchongo mliyopewa mkakosa...inauma sana.
Hahaha

Kumbe ule mpira ndio mnaita udambwi dambwi?[emoji23][emoji23]
 
Mkuu nipo?

Nimepotea vipi mbona DerbyDay nilikiwasha humu?

Au ulikuwa katika mazingira korofi yaliyopelekea ukose kuingia mtandaoni?
Mbona nilingia? Sikukuonaa labda mida ya kuwepo hapa uwanja huru wa JF ilikua tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…