Golikipa Aishi Manula kujiunga na Simba SC kambini Afrika Kusini kesho

Golikipa Aishi Manula kujiunga na Simba SC kambini Afrika Kusini kesho

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Golikipa wa Kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja Agosti, anatatajiwa kujiunga rasmi na kambi ya Klabu yetu ya Simba iliyopo Eden Vale Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Manula ambaye ndio Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na Klabu yetu, na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu, sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu.

Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

Orlando ambayo ndiyo klabu maarufu zaidi nchini humo, imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando lililopo jijini Johannesburg.

Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamisi ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest.

Mwisho

Klabu ya Simba kesho inawaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wake utakaofanyika kwenye ukumbi wa Kilenga uliopo jengo la New Millennium, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama hapa Dar es salaam
Mkutano huo kwa waandishi tu, unatarajiwa kuanza saa nne na nusu asubuhi.

Imetolewa Na ...

HAJI MANARA

Mkuu wa Habari wa Simba

Simba Nguvu Moja
 
SSC ni walemavu kwa YANGA.

Manula naye....uiache Azam SC uende kwa wachovu simba?

Daah,
 
SSC ni walemavu kwa YANGA.

Manula naye....uiache Azam SC uende kwa wachovu simba?

Daah,
Ulitaka aje kwenu? Mngepata wapi fedha ilhali sasa usajili wenu ni mkopo au mali kauli

Daima mbele Uturuki imebaki story

Shubamit!!!
 
Ulitaka aje kwenu? Mngepata wapi fedha ilhali sasa usajili wenu ni mkopo au mali kauli

Daima mbele Uturuki imebaki story

Shubamit!!!
Usajili wa Yanga unatosha...sawa?

Ligi inaanza keshokutwa, usije kukimbia hapa jamvini.

Mimi nawashangaa sana mashabiki wa simba kujivunia usajili ambao hautishi...na mwaka jana mlibweka hivi hivi.
 
Ila mjitahidi watani hzo mech zenu za kirafiki msije mkapigwa WIKI tena aiseeH
 
Ila mjitahidi watani hzo mech zenu za kirafiki msije mkapigwa WIKI tena aiseeH
Thubutuu.. Haijatokea wala haitatokea, hizo wiki labda umekumbuka sukuma wiki zinazoendelea kuliwa pale Bondeni kwa vile ukata umeingia

Subiri mauaji ya Shalubela kutoka kwa mnyama.. Shubamit..!!
 
Thubutuu.. Haijatokea wala haitatokea, hizo wiki labda umekumbuka sukuma wiki zinazoendelea kuliwa pale Bondeni kwa vile ukata umeingia

Subiri mauaji ya Shalubela kutoka kwa mnyama.. Shubamit..!!
🙂🙂🙂🙂 haya bhana mtani, tuwait 23 August ngao ya jamii
 
Back
Top Bottom