Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Golikipa wa Kimataifa wa Tanzania Aishi Salum Manula kesho tarehe moja Agosti, anatatajiwa kujiunga rasmi na kambi ya Klabu yetu ya Simba iliyopo Eden Vale Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Manula ambaye ndio Golikipa namba moja wa nchi hii ameshamalizana kila kitu kuhusu kujiunga na Klabu yetu, na ameahidi kuwapa furaha wanachama na washabiki wetu, sambamba na kuisaidia klabu kushinda mataji itakayowania msimu huu.
Wakati huo huo kesho timu ya Simba inatarajiwa kucheza mechi ya kwanza ya maandalizi ya msimu dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.
Orlando ambayo ndiyo klabu maarufu zaidi nchini humo, imeahidi kushusha silaha zake zote muhimu ili kuwapa maandalizi ya kutosha Simba, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye dimba la Orlando lililopo jijini Johannesburg.
Mechi nyingine ya mwisho itakayochezwa na Simba nchini humo itapigwa siku ya Alhamisi ya wiki hii dhidi ya mabingwa wa soka nchini humo kwa sasa Bidvest.
Mwisho
Klabu ya Simba kesho inawaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wake utakaofanyika kwenye ukumbi wa Kilenga uliopo jengo la New Millennium, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama hapa Dar es salaam
Mkutano huo kwa waandishi tu, unatarajiwa kuanza saa nne na nusu asubuhi.
Imetolewa Na ...
HAJI MANARA
Mkuu wa Habari wa Simba
Simba Nguvu Moja