GE2025 Golugwa: Pamoja na kumpoteza Nyalusi, CHADEMA itaendelea kupigania haki na ukombozi wa taifa

GE2025 Golugwa: Pamoja na kumpoteza Nyalusi, CHADEMA itaendelea kupigania haki na ukombozi wa taifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, amesema kuwa chama hicho kitaendelea kupigania haki na ukombozi wa taifa licha ya changamoto mbalimbali zinaoendelea nchini . Kauli hiyo ameitoa wakati akishiriki mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Iringa Mjini, marehemu Frank Nyalusi.

Akizungumza mbele ya mamia ya waombolezaji waliohudhuria mazishi hayo yaliyofanyika katika makabuli ya Makanyagio Kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa, Golugwa alisema kuwa marehemu Nyalusi alikuwa shujaa wa kweli, ambaye alijitoa kwa moyo wote katika kupigania haki za wanyonge na kuimarisha misingi ya demokrasia nchini.

Golugwa alikumbusha moja ya kauli maarufu ya marehemu Nyalusi iliyorekodiwa katika moja ya video zake ambazo zilitazamwa na watu wengi kwenye mitandao ya kijamii. Katika clip hiyo, Nyalusi aliwahi kusema:

"Waliomkamata Lissu ni wavuta bangi " kauli ambayo ilizua mjadala mkubwa kwenye mitandao kutokana na uzito na ujasiri wake.

Golugwa alitumia kauli hiyo kuonyesha namna Nyalusi alivyokuwa mkweli, jasiri na asiyeogopa kusema ukweli hata mbele ya hatari. Alisisitiza kuwa, licha ya kupoteza mwanachama muhimu, CHADEMA itaendelea na mapambano ya kidemokrasia hadi pale haki, uhuru na usawa vitakaposhinda.​
 
Back
Top Bottom