Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Polisi msituchokoze hatuji kufanya fujo mahakamani Wanachadema na Watanzania wote tusikubali kupigwa kama kuku
Mnatamani sana kupigana bila kujua tabaka la watawala litabaki lile lile hata baada ya sisi kupigana...Polisi hii mbegu ya chuki wanayoipanda kwa wanachadema ikija kukomaa ni wao polisi ndiyo watakuwa wahanga kwa sababu wanachadema ni wengi kuliko idadi ya poisi. Wanachadema wanakuja mahakamani kwa amani na hawana silaha zozote lakini huu uonevu ukizidi watu wataanza kutembea na silaha ili kujihami na ukatili wa polisi na hapo ndiyo mwanzo wa vita sasa. Polisi msitufikishe huko tafadhalini san
Wewe mpaka sasa umechukua hatua gani ndugu?Vijana wa Tanganyika wamelala fofofo - wanaona matatizo haya ni HAKI yao, hawajui mengi ya hayo yanatengenezwa na CCM.
Kutawala Taifa ambalo vijana hawajielewi ni kazi nyepesi mno.
Sijakusoma, kwa hiyo unapendekeza watu waendelee kupigwa tu na hawa majambazi wanaovaa uniform na wasijitetee? Nilifikiri ungetoa solutions kumbe unaponda tu, hivi huu ushenzi wa jeshi la polisi huoni kuwa ni tatizo? Poor you.Mnatamani sana kupigana bila kujua tabaka la watawala litabaki lile lile hata baada ya sisi kupigana...
Tutafuteni solution nyingine lakini nchi zote zilizofanya mapigano ya wao kwa wao bado tabaka la watawala lilibaki na waliendeea kula keki ya taifa. Baada ya mapigano ya kenya baada ya uchaguzi tabaka la watawala limebaki lilelile... baada ya ita ya libya tabaka la watawala limebaki lilelile tu, hakuna kipya.
Mark my words... ikishatokea utakuwa dissapointed mara 1000 zaidi ya hapa...