Mjini Goma, raia wengi wameonyesha wasiwasi kuhusu bunduki nyingi zilizopo mikononi mwa wenzao.
Jeshi la serikali la FARDC, liliposhindwa vita, wanajeshi walitupia bunduki na risasi mtaani, ambapo raia wengi waliziokota na kutokomea nazo.
Miongoni mwa waliochukuwa, ni wafungwa waliokuwa katika gereza la Munzenze huko Goma. Baada ya hali kuwa shwali kiasi chake, mpaka sasa bunduki hizo hazijakabidhiwa uongozi.
Hali hiyo inawapa wasiwasi wakazi wa Goma, huenda matukio ya siku za nyuma yakajirudia, huku walikuwa wakiona tofauti kubwa.
Wameomba uongozi mpya kuwasaidia hata kutumia kikosi maalum, kipite nyumba hadi nyumba, na raia wamesema wapo tayari kusaidia kuwatambua watu wasiojulikana, wajieleze, wanaotiliwa shaka wachukuliwe kwa mahojiano zaidi.