MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Baada ya wiki mbili, kufuatia vita vya serikali ya DRC na kundi la waasi la M23, wanajeshi wa FARDC, waliokuwa wamekimbilia kwenye kambi ya MONUSCO, wameamua kutoka na kujipeleka kwenye kambi ya jeshi ya M23 ili iamue yenyewe hatma ya maisha yao.
Hili limetokana na maisha magumu waliokuwa wakipitia wakiwa huko kwenye kambi ya MONUSCO. Huduma za mhiumu ikiwemo maji na chakula, vimekuwa changamoto kubwa kwao, huku serikali na yenyewe ikikaa kimya, jambo waliloona kama kutelekezwa, na kuamua kujisalimisha.
Awali, waliojisalimisha, walipelekwa kambi ya jeshi ya Katindo,walihudumiwa,na wenyewe kukili hawakutegemea wangepokelewa vizuri.
Badae walipelekwa kambi ya Rumangabo, kwa ajili ya masomo maalumu, baada ya hapo watakaokuwa na nia ya kuendelea na jeshi na kukizi vigezo, watapewa mafunzo ya kijeshi yatakayowawezesha kujiunga na jeshi hilo.
Watakaojisikia kupumzika na wale waliotupwa na umri, watawezeshwa kurudi uraiani. Kwa mjibu wa uongozi wa AFC/M23, wanajeshi hao licha ya kukamatwa na kuwa chini ya ulinzi wa M23, mishahara yao watalipwa kama kawaida.