Gombe!

Gombe!

Mwalimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
1,585
Reaction score
1,073
Gombe dume limekata - Linazaga mitaani
Lataka leta matata - Wenzangu tahadharini
Popote hupitapita - Laangaza hata ndani

Gombe dume limekata - Litatutiya hasara


Huvila vyakula vyote - Wala si hoja majani
Taka wali na mikate - Hata piya doriani
Fanyeni tulikamate - Tusingiye hasarani

Gombe dume limekata - Litatutiya hasara

Gombe sugu kweli kweli - Hii nawapa yakini
Lapiga na halijali - Litakuja mpaka ndani
Huharibu yote mali - Lateka hata vyumbani

Gombe dume limekata - Litatutiya hasara

Gombe na ujamu wake - Ni mkubwa wa kifani
Wala halina makeke - Bazazi la namba wani
Bora sasa tulisake - Litaleta kisirani

Gombe dume limekata - Litatutiya hasara

 
Utenzi nimeusoma, uloletwa na mwalimu
Gombele limeyoyoma, mitaani kama sumu,
Wakazi wanalalama, Gombe limetia timu,
Gombe hilo Gombe gani, linalofungwa na kamba?

Ng'ombe hafungwi kamba, bali yuazunguka
Kwenye konde na mashamba, kuutafuta mzuka
Na huko atambatamba, bila kuwa na mipaka
Gombe hilo gombe gani, linalofungwa na kamba?

Kama ngombe wa kisasa, bandani tunamuweka,
Anatunzwa kama kasa, mpaka anapozeeka,
Hakuna anachokosa, si haba vyaogezeka
Mwalimu wanichanganya, ng'ombe hafungwi kamba.
 
Jamani.. mkikopi mashairi ya watu wapeni wenye credit:

Shairi la Gombe ni la 1969..
Na. Dr. Said Ahmed wa Wete Pemba.
 
Jamani.. mkikopi mashairi ya watu wapeni wenye credit:

Shairi la Gombe ni la 1969..
Na. Dr. Said Ahmed wa Wete Pemba.

Asante Mwanakijiji, Ukweli kutueleza,
Nimeipata meseji, mwezetu ameteleza,
Kumbe si chake kipaji, alonayo kueleza
Gombe la mwalimu zee, wala msitie hofu.

Mnawaweza toka ndani, mitaani kubarizi,
Pamoja na vyenu vidani, ukiwa na la Azizi,
Kucheka bila kifani, kwenye bustani ya wazi
Gombe la mwalimu zee, wala mstie hofu
 
Back
Top Bottom