Gonjwa la efrancyia dawa yake kuzaa

Gonjwa la efrancyia dawa yake kuzaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Na Gladness Mallya

Msanii bonge wa filamu Bongo ambaye hivi karibuni alieleza kusumbuliwa na tumbo chini ya kitovu (chango), Efrancyia Mangii ameshauriwa kufanya jitihada za kuzaa ili kuepukana na tatizo hilo.


Akizungumza na Amani hivi karibuni, mtaalam wa masuala ya afya anayeandika makala za afya ya uzazi na nyinginezo kupitia magazeti ya Global Publishers, Dr.Chale alisema kuwa wengi waliokuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo wamepona baada ya kuzaa.

Alisema kuwa, tatizo la kuumwa tumbo chini ya kitovu linatokana na njia ya uzazi kuwa ndogo hivyo kwa mwanamke mwenye nalo anatakiwa abebe ujauzito kisha azae ili njia ya uzazi iweze kutanuka.

“Hili hujitokeza hata kwa wanawake ambao wameshazaa, hivyo hufanyiwa uchunguzi na kama anaumwa tumbo mara chache hupewa dawa, lakini kama ni tatizo linalojirudia wengi hushauriwa kuzaa.

“Endapo tatizo hilo halitaisha, mgonjwa atafanyiwa uchunguzi wa kina zaidi kama kuna uvimbe au maambukizi ya magomjwa mbalimbali katika njia ya uzazi,”alisema Dk. Chale.

Kufuatia maelezo hayo, mwandishi wetu alizungumza na Efrancyia kwa njia ya simu akiwa Dodoma ambapo alipoambiwa ushauri huo wa daktari alisema;

“Kwa kweli siko tayari kuzaa kwa sasa, hata hivyo nashukuru naendelea vizuri lakini nilipoenda hospitali walinipatia matibabu tu na hawakuniambia chochote kuhusu kuzaa,”alisema msanii huyo.http://www.globalpublishers.info/profiles/blog/show?id=5398006%3ABlogPost%3A269733&commentId=5398006%3AComment%3A269698&xg_source=activity
 

Attachments

  • efransia.jpg
    efransia.jpg
    63.8 KB · Views: 151
Back
Top Bottom