Huu mradi wa kuiigiza copy & paste toka China na Japan ni mgumu kweli kweli maana gharama yake kumlazimisha mkandarasi kuweka mbwembwe nyingii zisizo na lazima ili tu matarajio ya CCM Mpya kisiasa yatimie yanaifilisi nchi yetu Tanzania.
Kupitia video hii ya SGR reli Tanzania kulinganisha na mitandao ya reli za nchi zingine zenye uchumi mkubwa za Marekani ya Kaskazini, bara ulaya , Mashariki ya mbali China, Japan, Korea ya Kusini mpaka Oceania hapa CCM Mpya imeamua kutumia fedha nyingi bila ulazima wowote.
Tusubiri hii SGR reli Mpya itakayokuwa na urefu wa kilometa 1,200 kuona lini itakamilika na kama itaweza kuchochea makuzi ya kiuchumi na viwanda ndani ya Tanzania.
Maana tunaona ujenzi wa reli Mpya ukiendelea bila serikali kuanisha migodi mingapi ya makaa ya mawe ya Tanzania, viwanda vingapi vya ndani, mifugo ipi , mazao ya kilimo n.k itasafirishwa toka kona moja ya nchi yetu kwenda pembe nyingine ya Tanzania kuleta ajira rasmi nyingi za kuongeza thamani mazao, madini ya chuma pia upanuzi wa masoko ya ndani n.k