Wakati huu wa Kikwete tegemea more and more habari njema. Kwa asiyeelewa jinsi uchumi wa nchi unavyokua basi aangalie wafanya biashara walivyo na matumaini.
Yaani Bakhresa anunua meli zaidi, watu binafsi wanunua mabasi zaidi, maduka mazuri na mapya yafunguliwa kila siku, ujenzi ndio usiseme ni mauyoga tupu, Mashule ya serikali na watu binafsi kila siku yafunguliwa toka vyuo vya kawaida mpaka vyuo vikuu, piki piki mpaka vijijini, mashine za kusaga kila kijiji na....na.....na....na.... Ahhh nisimalize ukurasa hapa, Ah nimesahau Wamiliki wapya wa magazeti huibuka kila siku. Duuuu ilimradi ni maraha tu.
Sasa njoeni na zenu eti deni limekua, wacha weee hakuna nchi isiyo na deni. Fahamu kuwa Marekani ndio inayoongoza kuwa na deni kubwa zaidi. Usiniulize ni ngapi, ingia mwenyewe
www.aneki.com au ukipenda
www.cia.gov...... ni wamoja hao.