Good news: Wenye nia njema na Yanga huko CAF wamtetea Mayele, kiatu CAFCL ni chake mwaka huu, aibu kwa Karia na Motsepe

Good news: Wenye nia njema na Yanga huko CAF wamtetea Mayele, kiatu CAFCL ni chake mwaka huu, aibu kwa Karia na Motsepe

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Mungu ni mkubwa sana, baada ya figisu ya kumfungia miaka 2 msemaji aliyeipa ubingwa Yanga baada ya kuukosa kwa miaka 4 ndugu Manara , figisu ziliendelea sana

Tukaona wachezaji wa Yanga wakitaka kuvunjwa miguu marefa kimya, adhabu ya Inonga hadi leo kimya, kamati ya masaa 72 huwa ni kuwaadhibu Yanga tu

Yakaja ya Kisinda ila Mungu ni mkubwa kawapiga upofu kwenye roho zao mbaya sasa Kisinda anaenda kupima watu umri tusubiri mambio yale , ma assits yake, magoli yake, maudambwiudambwi, ma skills yake,dah itakuwa hatari sana

HABARI NJEMA TOKA CAF ni kwamba baada ya figisu figisu za Karia na Rais wa CAF Motsepe za kubadili kanuni majuzi tu ili FISTON LEWANDOSKI HARLAND MAYELE asichukue ufungaji bora wa CAF watu wenye nia njema na Yanga huko CAIRO makao makuu ya CAF na wasio na chuki dhidi ya klabu hiyo kubwa na bora kabisa barani Afrika kwa sasa wamesema NO, sheria ibaki kama ilivyo

Wananchi leo mjitokeze kwa wingi kushuhudia Fiston the greatest of all time Mayele akipiga bao 7 na kufikisha bao kumi hivyo kuibuka mfungaji bora wa champions league mwaka huu

Party ya kusheherekea KIATU CHA DHAHABU CHA CAF 2022/23 KUTUA YANGA itafanyika Kidimbwi baadaye usiku
 
Mungu ni mkubwa sana, baada ya figisu ya kumfungia miaka 2 msemaji aliyeipa ubingwa yanga badaa ya kuukosa kwa miaka 4 ndugu manara , figisu ziliendelea sana...
Ahahahaha

Halafu na mipira yote na pasi anapewa yeye leo
 
Ahahahaha

Halafu na mipira yote na pasi anapewa yeye leo
kiatu tayari kishatua jangwani hakuna atakayefikia magoli 10 ya mayele na hii team inafika fainali ya CAF , hadi kufika huko mayele ana goals 20 , goli bora la CAF
 
Kila nikimkumbuka huyu mtu alichotufanya basi icho kiatu cha cafcl top scorer apewe tu hakuna namna[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Screenshot_20220917-111314.jpg
Screenshot_20220917-111131.jpg
Screenshot_20220917-110938.jpg
 
Shida uliyonayo unaandika Kwa sababu we ni shabiki wa Yanga na mayele
Ila kama ungeandika kama shabiki wa soka usingeaandika utapiamlo huuu
 
Shida uliyonayo unaandika Kwa sababu we ni shabiki wa Yanga na mayele
Ila kama ungeandika kama shabiki wa soka usingeaandika utapiamlo huuu
tayari mfungaji bora wa mwaka huu champions league ni mayele
 
Raha ya kuwa utopolo ni kujifariji. Hakika mshabiki wa uto hata akifiwa na bwana ake kama huyu mtoa mada atafanya sherehe kwa kujiaminisha amesafiri tu kwenda kusoma ulaya
 
list ya wenye akili haijaongezeka huko utopoloni
 
Akiona post ya njaakalihatari tu we ona tu kama umebahatika kukutana na mbumbumbu mwanadamizi kutoka Makoloni. Njoo Kali ana njaa kweli kweli.
 
Back
Top Bottom