tatizo sio JF, tatizo ni umri unaenda, majukumu kuongezeka na mambo kuwa mengi kiasi kwamba kasi ya JF inatushinda wengi na ndio maana tunaona kama haina mvuto sana.
Leo hii mtu kugawa muda wa kazi, familia, Insta, Whatsapp, Snap, nk ndani ya masaa 24 ni ngumu, lazima ubongo uanze ku-sacrifice baadhi ya vitu.
Mtu aliyejiunga JF 2008 ana miaka zaidi ya 10 humu sawa na mtoto aliyeanza darasa la kwanza leo atakuwa form IV.
Waliokuwa sekondari leo wamemaliza vyuo, waliokuwa single leo wameoa/kuolewa na watoto juu, waliokuwa wanakaa kwa mashemeji leo wanakazi zao na zinawahitaji muda, waliokuwa, wengine humu wameanza kuzeeka, maisha yanabadilika.