Goodbye our commander Umkontho

hawa jamaa si wema, magonjwa wanayatengeneza....mweusi anaafya yake ya asili, wanajaribu kuiua
 
asante ndugu
lakini Tumegee kidogo, kwa manufaa ya wengine
JUKWAA LA WAJAMAA TANZANIA (JULAWATA)

Lengo la Jukwaa hili ni kuendeleza nadharia na mapambano ya kudai Ujamaa na Umajumuhi wa Afrika. Siku zote, na popote tunapokuwa tunasimama upande wa wavujajasho. Tunaupinga Ubepari katika sura zake zote (ubeberu, uliberali mamboleo n.k ) pamoja na mifumo mingine kandamizi inayostawisha ubepari (mfumo dume,ubaguzi wa rangi, ukabila, udini, ukaburu wa kiumri n.k ). Tunapambana kuibomoa mifumo hii yote ili kujenga mfumo unayozingatia uhuru, utu, haki na usawa. Mfumo huo tunaopambana kuujenga ni mfumo wa kijamaa.
 
Asante sana ndugu, tukopamoja kabisa....endelea kutushushia nondo..hii ndio vita yetu na marehemu pia
 
Asante sana ndugu, tukopamoja kabisa....endelea kutushushia nondo..hii ndio vita yetu na marehemu pia
HISTORIA YA MAPAMBANO YA CUBA: KUTOKA HATUEY HADI FIDEL CASTRO

Na Sabatho Nyamsenda

Mara tu dege lile la Blue Panorama Airlines lilipotua, abiria walipiga makofi kumpongeza rubani kwa kutufikisha salama kwa safari ndefu ya saa 11 iliyoanzia mji wa Milano nchini Italia. Lakini zaidi, wengi wa abiria hao, nikiwamo mie, tulikuwa tukishangilia kutua katika jiji la Havana, nchini Cuba. Cuba ya Fidel Castro Ruz. Cuba ya Ernesto Che Guevara. Kisiwa cha Ujamaa kilichoushinda ubeberu wa Marekani.
Kwangu mimi, hii ilikuwa ni safari yangu ya kwanza nje ya Afrika. Nilikuwa nimeapa kuwa nikitoa mguu nje ya Afrika basi nitaenda Cuba kwa Fidel Castro nikapate “utakaso” wa kiitikadi kabla sijakanyaga kwingine duniani.

Naam, nikawasili Cuba tarehe 16 Novemba 2014. Nilikuwa nimealikwa kuwasilisha mada katika Kongamano la Kimataifa kuhusu namna ya kujenga Ujamaa katika karne ya 21. Mada yangu ilihusu jaribio la kujenga Ujamaa nchini Tanzania, chini ya utawala wa Mwl. Nyerere.

Mwalimu Nyerere na Fidel Castro walikuwa marafiki walioshibana, na nchi walizoziongoza ziliheshimika duniani kote kwa kuwa zilithubutu kujenga jamii inayozingatia misingi ya utu, haki na usawa. Baada Mwalimu kung’atuka, nchi yetu ikageukia misingi ya unyama na ujambazi, tena ujambazi unaolindwa na dola, na kuhalalishwa na sheria chini ya kauli-mbiu za uwekezaji, ubinafsishaji na utandawazi.

Nchini Cuba, hatukwenda kuhudhuria Kongamano peke yake. Tulifanya ziara sehemu mbalimbali za jiji la Havana na viunga vyake, tukitembelea hospitali na vituo vya afya, vituo vya mafunzo ya kiitikadi kwa watoto, vyama vya ushirika, na kamati za kulinda mapinduzi.

Tulizungumza na madaktari wanamapinduzi waliokula yamini kulinda afya za wanyonge, tukapiga soga na machinga na mamantilie wa jijini Havana ambao walituhakikishia kuwa wataendelea kuulinda ujamaa wa Cuba na kamwe hawataruhusu mabeberu waitawale na kuinyonya nchi yao. “Mabeberu wana silaha za maangamizi,” alituambia kijana mmoja anayefanya umachinga wa vitabu jijini Havana, “sisi tuna moyo wa ujasiri… Mabeberu wana pesa zenye sumu, sisi tuna utu. Ni utu na ujasiri huu ndio tulioutumia kuwashinda wakoloni wa Kihispania, na ndio pia tuliutumia kuwashinda mabeberu wa Kimarekani”.

UJASIRI WA KUPIGANIA UTU
Ujasiri huu wa Wa-Cuba katika kupigania na kulinda utu na uhuru wao haukuanza na Fidel Castro. Ni wa Kihistoria. Historia ya mapambano ya ukombozi wa Cuba ilianza mwanzoni kabisa mwa karne ya 16 pale tu walowezi toka Ulaya walipolivamia bara la Amerika na kuwaua wenyeji wa Bara hilo, huku wakitwaa ardhi yao na kupora rasilimali zao, hasa dhahabu na shaba.

Kama ilivyotokea katika sehemu zingine za Amerika ya Kaskazini, wenyeji wa Cuba, wanaojulikana kama “Wahindi wa Marekani” (Amerindians), walipigana kuilinda ardhi yao, uhuru wao na utu wao. Wazungu walijigamba kuwa wao ni taifa teule la Mungu, na walikuja Amerika kutimiza wajibu wao wa kuwastaarabisha wenyeji wa Bara hilo. Mikobani, wazungu walibeba biblia, na mikononi walishikilia bunduki. Midomoni udenda uliwadondoka walipoona madini tele na ardhi yenye rutuba.

Hatuey, kiongozi wa Wahindi wa Amerika, aliyekuwa amekwenda Cuba akitokea kisiwa cha Hispaniola (sasa Haiti) ambacho tayari kilikuwa kimekwishavamiwa, alihoji ni Mungu gani huyo aliyehalalisha uporaji na umwagaji damu? “Wakatili hawa” Hatuey aliwaambia ndugu zake Wa-Cuba, “wanatuambia kuwa wanamwabudi Mungu wa amani na usawa, lakini wanatupora ardhi yetu na kutugeuza watumwa wao. Wanatuambia kuhusu uzima wa milele pamoja na pepo na ahera, na bado wanatupora mali zetu, wanawabaka wake zetu na kuwanajisi binti zetu.” Akiwaonyesha wenzake nchini Cuba kapu lililojaa dhahabu na vito vya thamani, Hatuey alisema kwa uchungu, “Huyu ndiye mungu anayeabudiwa na Wahispaniola, ili kuvipata vitu hivi wanapigana na kuua; ili kuvipata vitu hivi wanatutesa, ndiyo maana tunapaswa kupambana nao na kuwatupilia baharini.”

Hatuey aliongoza vita vya kwanza vya msituni (guerrilla warfare) nchini Cuba kupinga uvamizi na ukatili huo wa Wazungu kutoka Ulaya.

Hata hivyo, wazungu walikuwa wamejizatiti kwa silaha za mauaji, ngao za vyuma na ngome imara. “Kwa kuwa hawana ujasiri kama wa kwetu” Hatuey alitamka, “[wazungu] waoga hawa wanajikinga kwa vyuma ambavyo silaha zetu haziwezi kuvunja…”

Wazungu toka Ulaya wakawaua wenyeji wa Amerika kama wanyama. Hatuey mwenyewe alikamatwa tarehe 2 Februari 1512 na kuuawa kwa kuchomwa moto. Kabla moto haujawashwa, aliletwa kasisi ili atubu dhambi zake [za kupinga uvamizi wa Wazungu] na kuomba sala zake za mwisho ili aweze kwenda mbinguni baada ya kuchomwa moto. Hatuey alikataa kujisalimisha kwa Mungu huyo wa uvamizi na uporaji.

“Je, kuna watu kama wewe huko mbinguni?” Hatuey alimwuliza kasisi wa Kihispaniola kwa mshangao.
“Wapo watu wengi kama mimi huko mbinguni,” kasisi alimjibu.

Hatuey alikataa kujisalimisha kwa mungu anayewatuma wafuasi wake kuwapora, kuwabaka na kuwaua kikatili watu wa mataifa mengine. Hivyo akagoma kujisalimisha kwa mungu huyo wa uporaji, uuaji na ubakaji. Akachomwa moto akiwa hai hadi kufariki.

Mauaji hayo ya kikatili yalifanyika kote Barani Amerika. Wenyeji wa Cuba, ambao idadi yao ilikuwa zaidi ya 112,000 mwaka 1512 uvamizi ulipoanza, waliuawa na kubaki 3,000 kufikia mwaka 1542. Mauaji ya kwanza ya kimbari katika historia ya ubepari ni yale yaliyofanywa na walowezi toka Ulaya dhidi ya wenyeji wa Bara la Amerika!

Fidel Castro aliifahamu vema historia hii ya awamu ya kwanza ya mapambano. Hatuey ni kati ya miamba ya mapambano ambayo kwayo Castro alijiegemeza. Yapo mambo kadhaa ambayo Castro alijifunza kutoka kwa Hatuey, ambayo yalimwongoza katika mapambano ya kupigania utu, usawa na uhuru.

La kwanza ni kuwa mapambano yoyote dhidi ya wavamizi yalipaswa kuongozwa na itikadi pana ya Umajumui wa Amerika (pan-Americanism). Ndiyo maana Hatuey alikwenda Cuba kuwatahadharisha ndugu zake juu ya uvamizi ulioanzia Hispaniola, na akashiriki kikamilifu kuwahamasisha ndugu zake Wa-Cuba kupambana na uvamizi huo. Kabla ya kwenda Cuba, Hatuey alikuwa amepambana na wavamizi hao kwa takribani miaka 10 katika kisiwa cha Haiti.

Somo la pili ni kuwa wapiganiaji wa utu na usawa wanapaswa kuanzisha mshikamano na wote wanaonyonywa na kuonewa. Ndiyo maana basi Hatuey, katika mapambano yake huko Haiti alishirikiana na watumwa waliokuwa wameletwa toka Afrika kufanya kazi katika ardhi iliyoporwa kutoka kwa wenyeji wa Marekani. Haishangazi basi Nicolas de Ovando, aliyeletwa kuwa gavana wa kisiwa cha Hispaniola, alimwandikia mfalme Ferdinand wa Hispania mwaka 1502, akilalamika kuwa watumwa toka Afrika walitoroka na kujiunga na Wahindi wa Kiamerika katika mapambano dhidi ya walowezi wa Kizungu. Aliyeongoza mapambano hayo si mwingine bali ni jemedari Hatuey!

Somo jingine ambalo Fidel Castro na wanamapinduzi wenzake kama Che Guevara walijifunza toka kwa Hatuey ni mbinu za vita vya msituni (guerilla warfare). Baada ya kwenda Cuba, Hatuey na wapiganaji wenzake walikuwa wakishambulia, na kisha wakajikusanya milimani ili kujitathmini na kujipanga upya kabla ya kuanzisha shambulio jingine.

Mbinu hizo pia zilitumiwa na kiongozi mwingine wa wenyeji nchini Cuba aliyeitwa Guamá kati ya 1522 na 1533. Akishirikiana na mkewe, Habaguanex, pamoja na wapiganaji wengine, Guamá pia alitumia mbinu za vita vya msituni kupambana na walowezi toka Ulaya. Inafahamika kuwa baada ya kushindwa kwa majaribio ya awali ya kuupindua utawala wa kifashisti wa Fulgencio Batista, Fidel Castro na wenzake walikwenda katika milima ya Sierra Maestra ambako walihamasisha wakulima kujiunga katika mapambano, na walitumia mbinu za vita vya msituni katika mapambano yao!

Huyo ndiye, Hatuey, jemedari wa mwanzo kabisa wa wenyeji wa Amerika aliyeongoza mapambano dhidi ya uvamizi wa wazungu kutoka Ulaya. Alipandikiza mbegu iliyokuja kumea na kuzaa ujasiri wa kukataa kunyonywa na kunyanyaswa, pamoja na ujasiri wa kupambana ili kubomoa mifumo yote ya ukandamizaji na unyonyaji.

Baada ya mapinduzi ya Cuba, serikali iliyoongozwa na Fidel Castro ilijenga mnara wa kumbukumbu mahali ambapo Hatuey alichomewa moto, na kuandika: “Muasi wa Kwanza wa Amerika”. Mara kadhaa katika hotuba zake, moja wapo ikiwa ni ile aliyoitoa Harlem (Marekani) mwaka 1995, Fidel Castro huutambua mchango wa Hatuey katika mapinduzi ya Cuba.

Katika tawasifu wake uitwao My Life, Fidel Castro anamweleza Hatuey kama “mmoja wa watu muhimu kabisa katika historia ya Cuba, mtu wa mwanzo kabisa aliyethubutu kupambana na uvamizi wa Wahispaniola.”

(Makala hii ilichapwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 30 Desemba 2016)
 
Ndugu, tunashukuru....mno....karibu kutuma makala zingine...you are one of us...tuko pamoja
 
tunahitaji vision....kusaidiana kwa upendo....wapenda haki kote duniani....tena kufanya mambo kwa kujitolea...tunahitaji sokoine wengi zaidi....
 
Somalia, the only African country without government, can you advice me, are they seniles, embeciles, or just purely insane!!!!
Say what ? Somalia has a legitimate government recognised by the International community, only a person with a malfunctioning brain can float such a lackadaisical statement ati "Somalia doesn't have a government" 😀
 
Umeomba poo, mwenyewe. Safi sana sasa get ua shiti tugeza na wachana na hizi shenanigans za middle skuli.
 
Say what ? Somalia has a legitimate government recognised by the International community, only a person with a malfunctioning brain can float such a lackadaisical statement ati "Somalia doesn't have a government" 😀
Does it...amazing.....we are so happy for you
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…