Goodluck Gozbert sio mwimbaji wa Gospel

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
Habari wana JF,
Moja kwa moja kwenye mada, kama tujuavyo neno Gospel maana yake ni Habari njema kwa watu wote (kutokana na imani ya kikristo). Na kuna waimbaji wengi (hatuwaiti wasanii maana hamna usanii kwenye dini) wanaimba kama njia ya kumtumikia Mungu.Wapo wengi kama kina Bahati Bukuku, Rose Muhando,Christina Shusho n.k

Mwanzo nilikuwa nasita kupinga kuwa Goodluck gozbert sio muimbaji wa Injili ila ni mziki wake ni wa Bongo flavour tu. Hili linajidhirisha vyema kupitia nyimbo yake ya 'Nibadilishe' ambayo ndani yake mahadhi ya nyimbo na style za kucheza hazitofautiani na zile za kina Harmonise, Diamond, Burna Boy n.k. Hii inaniaminisha kuwa huyu si muimbaji wa gospel bali anafanya Bongo flavour kwa kivuli cha dini. Kama hujaona wimbo huo...Angalia kwenye link hapa chini....


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Author, Unachokifanya hakiakisi hata tone ya vile unavyojiita. Niliposoma kichwa cha uzi wako na jina lako nilihamasika sana kufungua huu uzi wako lakini nimesikitika sana baada ya kuona na kusoma ulichoandika kwa sababu kadha wa kadha.

Kwanza, Umeshindwa kuchunguza na kuelewa kuwa Gospel ambayo anaimba msanii wa Tanzania ni Bongo Fleva pia. Kwa lugha nyepesi umeandika bila kuelewa undani wa hicho unachokiandika. Pole sana.

Pili, Gospel sio lazima iimbwe juu ya biti za vinanda. Hio ni kwa sababu Gospel ni ujumbe na sio uzuri au ubaya wa biti. Swali ni kwamba ujumbe aliouonyesha Gozbert humo unahamasisha injili au unapinga injili??

Naomba unielewe kuwa sikatai kuwa unachokisema ni sahihi. Unaweza kuwa sahihi au usiwe sahihi. Ninachoshangaa ni kwamba umeshindwa kuthibitisha malalamiko yako. Ni kama watu wanaotaka bangi ihalalishwe - huwa wapo sahihi, ila hawajui kuitetea hoja yao.

Anyways, Ukijibu hayo maswali hapo juu naomba nikupe home work. Nenda uisikilize Album ya Kanye West, Jesus is King.
 
Nini tatizo la hiyo video na wimbo kwa ujumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sabato bado kidogo
 
umejitahidi kumwangalia kwa jicho la tatu , ongeza juhudi kwa jicho la nne utamwona yupo ndani ya YESU
 
Huu mjadala ulishaisha.

Kama hukuelewa baki na ujuavyo.
 
Mawazo mazuri,,ila Injili haipimwi kwa maneno Chachasteven....soma uzi wangu tena
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…