Goodluck Gozbert unaelekea wapi?

Goodluck Gozbert unaelekea wapi?

Wabongo bwana, hao wanaomdiss ndio wa kwanza kufanya hivyo vitendo alivyosema na kujifanya 'watakatifu jina'

Mtu kabadilisha ladha na maudhui bado mnamkosoa... tambua huwezi kuridhisha wote

Watanzania tuache unafiki
 
Yeye mwenyewe alisahweka wazi kuwa anaimba Inspirational songs na sio Gospel songs.
 
Binafsi namuheshimu jamaa kama binadamu yeyote anavyopaswa kupewa heshima yake.Anayoyafanya ni mambo yake binafsi tu kwa ajili ya kupambana na maisha yake kiuchumi.HAKUNA KINACHOHUSIANA NA MUNGU HAPO .Hapo yuko kazi kama wengine tunavyokua kwenye dili zetu na mishen town.Hakuna analofanya hapo LENYE KUMTUKUZA KRISTO kwa ufaham wangu mdogo wa elimu na maarifa ya IMANI ya KIKRISTO.
Hapo yuko kwenye kama kazi zingine.MUMGU TUMWEKE KANDO HAPO JAMANI .hayupo wala hakuna chochote hapo kwenye video ambacho NI CONSTRUCTIVE KUMJENGA KIIMANI MKRISTO.
Ila kama ni BURUDANI ,aahh dogo KATISHA SANAA
 
Kaka kweli ukiishi kwa kufata wanachopenda wanaokuzunguka Basi huwez fanya chochote
Wabongo bwana, hao wanaomdiss ndio wa kwanza kufanya hivyo vitendo alivyosema na kujifanya 'watakatifu jina'

Mtu kabadilisha ladha na maudhui bado mnamkosoa... tambua huwezi kuridhisha wote

Watanzania tuache unafiki
 
Angalia uchezaji ule mavazi na hata muundo wa nyimbo ni wakidunia sana
Gospel bases much on the soul rather than the fresh ... David, alicheza hadi nguo zikadondoka then mke wake akamcriticize mwishowe she got cursed in a way she could not give birth until her death.
 
Mziki biashara
Wakuu habari

Hivi hii nyimbo mpya aliyoitoa Goodluck Gozbert ni ya dini au maana sio kwa maudhui Yale kwa upande wa video na audio pia
Huyu atakua kama Willy Paul
Mana nayeye alkuaga anafanya gospel Kama bongofleva and at the end of the day tumeona alipo sasa alivovyoamua tu kuingia kwenye bongofleva moja kwa zote
maybe Mungu ambadilishe tuuu gozbert kama alivoimbaa vile
 
Huyu atakua kama Willy Paul
Mana nayeye alkuaga anafanya gospel Kama bongofleva and at the end of the day tumeona alipo sasa alivovyoamua tu kuingia kwenye bongofleva moja kwa zote
maybe Mungu ambadilishe tuuu gozbert kama alivoimbaa vile
Kwa kweli
 
Achague kuwa wa baridi au moto.. Naona anakuwa wa vuguvugu sasa....
 
Ni ngumu sana kwa wakristo kumuelewa Godluck Gozbert kwenye huu wimbo.

Wanazuga kuwa hawapendi Uchezaji na staili ya mavazi kwenye video, lakini kiukweli wanachukia zaidi mashairi ya wimbo.

Mkristo sio mtu anaetaka kuiimba "Nibadilishe", yaani akiri mbele ya watu kuwa yeye ndo ana matatizo, ana dhambi? ni mchungaji gani anaweza upenda huo wimbo? yaani unataka Kakobe au Gwajima, au Nkone, aimbe Mungu Nibadilishe na kuconfess dhambi zake za sirini mbele ya watu? Maana hicho ndicho anachoimba dogo.

Laiti kama dogo angeimba "Mbadilishe" na akawa anafocus kwenye nafsi ya tatu, " Kwanza umenyoa denge, unapenda sana michezo ya nywele......., Omba Ubadilishwe......" Wakristo wengi wangeupenda, regardless ya michezo na mavasi, kwa kuwa wangeutumia kwenye hata ushuhudiaji, na kusemana, maana wanapenda kuwasema sana wale wanaowaona sio wakamilifu.

Yaani kwa maneno machache angeimba nafsi ya tatu, wimbo ungekuwa wa ushuhudiaji, na wakusengenyana, na ndizo wakristo wengi wanazipenda, ila kaimba nafsi ya kwanza, umekuwa wimbo wa confession, ambao wakristo hawapendi kuconfess mbele za watu.
 
Back
Top Bottom