Google Earth na athari yake kwa usalama wa nchi

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712

logo-Google-earth.jpg

Kwa ufupi:

Google earth imesaidia katika mambo mengi hasa kwenye masuala ya uhandisi, kwani baadhi ya wahandisi wa barabara hawalazimiki kwenda porini kwa ajili ya kuchukua ramani au baadhi ya vipimo vya maeneo wanayotaka kuweka barabara.

Google earth ni programu inayomwezesha mtumiaji kuangalia ramani, miundombinu, jiografia na mambo mengine duniani kwa kutumia mtandao.

Kabla ya kuitwa google earth, programu hii ilijulikana kwa jina la Earth3D Viewer chini ya Kampuni ya KeyHole iliyokuwa inadhaminiwa na Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA).

Picha zote zinazoonekana unapofungua programu hii huwa zinatolewa na shirika la mambo ya anga za juu la Marekani (NASA) na bila mtandao huwezi kupata picha yoyote.

Kuna aina mbili ya programu za google earth; ile ya Google Earth na Google Earth Pro. Tofauti ni kwamba hii Google earth Pro ni ya kulipia, yaani inauzwa na inakuwezesha kupata mambo mengi zaidi ya hiyo ya kwanza.

Programu hii inakuwezesha kuruka juu kuangalia dunia jinsi ilivyo, kutembelea maeneo mbalimbali ya dunia kuanzia mbuga za wanyama, viwanja vya michezo, majengo, barabara, mitaa na vitu vingine vingi.

Google earth imesaidia katika mambo mengi hasa kwenye masuala ya uhandisi, kwani baadhi ya wahandisi wa barabara hawalazimiki kwenda porini kwa ajili ya kuchukua ramani au baadhi ya vipimo vya maeneo wanayotaka kuweka barabara.

Kwa wale wageni wa maeneo wanaweza kutumia google earth kwa ajili ya kutengeneza ramani ya maeneo wanayopenda kutembelea kisha wanahifadhi kwenye vifaa vyao.

Kama uliwahi kusikia mradi wa magari yatakayokuwa yanajiendesha yenyewe, programu kama google earth ndiyo inawezesha utendaji wa magari kama hayo na vifaa vingine vinavyojiendesha vyenyewe.

Hata hivyo, Google earth kwa upande mwingine imekuwa chanzo cha migogoro kati ya mataifa hasa katika masuala yanayohusu mipaka. Pia kuna suala la CIA kukusanya taarifa za watu na vitu bila ya wahusika kujua. Hii ilifanyika sana wakati ule wa Earth3D Viewer.

Hapa kwetu suala la google earth liliwahi kuleta mgogoro kidogo baada ya watu kutumia programu hiyo kuweka mipaka ya Ziwa Nyasa na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kama vile ndiyo halisi kumbe haikuwa na ukweli wowote.

Huko Marekani kwenyewe kipindi cha nyuma kidogo kuliwahi kuibuka kelele kutoka kwa mamlaka nyingine za usalama kutokana na programu hii kutoa ramani za maeneo mbalimbali kama viwanja vya ndege, kambi za jeshi na barabara.

Kimsingi faragha za watu ni kitu kinacholeta shida katika matumizi ya programu hii. Wakati mwingine mtu anaweza kupiga picha ya jengo au nyumba ya mtu na kujua mengi.

Programu hii na taarifa zake zinazidi kuboreshwa na kuongezewa kila siku kutokana na mahitaji pamoja na watu wanaotembelea au kujitolea kila siku.

Hata hivyo, siku zijazo kunaweza kuibuka matatizo makubwa zaidi endapo hakutakuwa na udhibiti wa mipaka ya utendaji wa kazi wa programu.

Nchi kama Tanzania inatakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya ukaguzi kwenye programu kama hizi na nyingine zinazofanana kwa ajili ya kulinda usalama wake na wa raia.

CHANZO: Mwananchi
 
Wezi wa wenzetu kuliko endelea hii kitu ni sehemu ya vitendea kazi
 
Niliwahi kuona picha ya nyumba yangu na kuona jinsi nyasi zilivyoota nyingi, kiasi cha kumuuliza kijana anayetunza nyumba kwa nini hakati majani! Alishangaa nilijuaje hilo, nilimwambia kuwa naweza kuona mahali popote kutoka mbali!
 
hahahhaaa, ulimbahatisha tu, maana picha nyingi za huku kwetu zinakuwa za miezi kadhaa nyuma!
 
halafu mwandishi na yeye naona ameongezaea ka-propaganda hapo mwisho; mipaka ya Nyasaland na Malawi ilichorwa hivyo toka enzi za ukoloni, miaka mingi kabla ya google earth, hata ukitizama ramani nyingi za miaka ya nyuma na za sasa utaona hivyo!
 
Kweli, maana ndio kwanza walikuwa wame update baada ya miaka mingi!

Wakuu samahanini kwa kuwainterfere.

Nahisi hizi google earth ziko version tofauti tofauti, mi nimeanza kutumia google earth kama mwaka wa pili sasa.

Nimeobserve kwamba iyo kitu ipo uptodate sana, sana, sana.
Kwani niliweza na naweza kutrace hata mabasi makubwa yaendayo mikoani, na pia naweza kutrace boti au meli.

Sehemu kana kuna mvua nawezajua kwa kuona kiwingu kilichoiva ktk eneo husika, aghlabu kukiwa na mvua nashindwa kuona kilichopo chini kutokana na kuzibwa na kiwingu hicho.
Si hivyo tu, pia kunatofauti kubwa ya picha nnapoangalia usiku ukilinganisha na nionavyo mchana. Na hata nikiangalia mida ya jioni huona bati (za nyumba) ziking'aa upande wa magharibi kitu ambacho ni tofauti na pale nikiangalia asubuhi au mchana.

What do you think?
 
Jinsi muda unavyoendelea kwenda ndivyo maisha yana rahisishwa na technologia lakin kila chenye faida hakikosi hasara....intanent,madini ya uraniam yanotengeneza nishati ya nyuklia
 
Wakuu samahanini kwa kuwainterfere.

Nahisi hizi google earth ziko version tofauti tofauti, mi nimeanza kutumia google earth kama mwaka wa pili sasa.

Nimeobserve kwamba iyo kitu ipo uptodate sana, sana, sana.
Kwani niliweza na naweza kutrace hata mabasi makubwa yaendayo mikoani, na pia naweza kutrace boti au meli.

Sehemu kana kuna mvua nawezajua kwa kuona kiwingu kilichoiva ktk eneo husika, aghlabu kukiwa na mvua nashindwa kuona kilichopo chini kutokana na kuzibwa na kiwingu hicho.
Si hivyo tu, pia kunatofauti kubwa ya picha nnapoangalia usiku ukilinganisha na nionavyo mchana. Na hata nikiangalia mida ya jioni huona bati (za nyumba) ziking'aa upande wa magharibi kitu ambacho ni tofauti na pale nikiangalia asubuhi au mchana.

What do you think?

Mkuu isijekuwa uko marekani, maana naona kama unapata live feed uko mapentagon mzee! Kusema kweli Google Earth navyofahamu huwa hawafanyi global update ya mara moja, huwa wanaupdate maeneo tofautitofauti, japo kwa wenzetu naskia wanaupdate mara mbili kwa mwezi kwa baadhi ya maeneo, sijajua wewe uko wapi lakini mimi kuna sehem nina kaproject kangu huwa natembelea mara kwa mara lakini nikiingia hata sasa nakuta mashamba ndiyo kwanza yamelimwa..hizo picha ni za mwezi wa kwanza sasa hivi mashamba ndiyo kwanza yanaandaliwa!! again, inawezekana eneo ulilopo lina bahati ya kuwa updated sana!
 
Niliwahi kuona picha ya nyumba yangu na kuona jinsi nyasi zilivyoota nyingi, kiasi cha kumuuliza kijana anayetunza nyumba kwa nini hakati majani! Alishangaa nilijuaje hilo, nilimwambia kuwa naweza kuona mahali popote kutoka mbali!

Hehheee kijana lazima amekuhisi we mchawi
 
Mkuu isijekuwa uko marekani, maana naona kama unapata live feed uko mapentagon mzee! Kusema kweli Google Earth navyofahamu huwa hawafanyi global update ya mara moja, huwa wanaupdate maeneo tofautitofauti, japo kwa wenzetu naskia wanaupdate mara mbili kwa mwezi kwa baadhi ya maeneo, sijajua wewe uko wapi lakini mimi kuna sehem nina kaproject kangu huwa natembelea mara kwa mara lakini nikiingia hata sasa nakuta mashamba ndiyo kwanza yamelimwa..hizo picha ni za mwezi wa kwanza sasa hivi mashamba ndiyo kwanza yanaandaliwa!! again, inawezekana eneo ulilopo lina bahati ya kuwa updated sana!

Mmh! Mbona mi niko kitiizii!

Embu kama unasimu kubwa jaribu kugugo 'application: google earth' or google map.

Katika simu nyingi tu za kisasa wameekewa hiyo kitu, tatizo ni kwamba wengi hawajui kuitumia. Coz nimewaelekeza frnd wangu kama watatu namna ya kutumia huku nikiwashawishi wengine wadownload hiyo makitu.

Watu wengi hushindwa kuitumia au kuiona haina maana kwa kushindwa kuibadili mwonekano wake kutoka map view kwenda satelite view.

Ukiidownload inakuwa ktk map view.
 
halafu mwandishi na yeye naona ameongezaea ka-propaganda hapo mwisho; mipaka ya Nyasaland na Malawi ilichorwa hivyo toka enzi za ukoloni, miaka mingi kabla ya google earth, hata ukitizama ramani nyingi za miaka ya nyuma na za sasa utaona hivyo!

excuse me,toka enzi za ukoloni?!...how comes ile inayotumiwa na CNN provides real time images?.umewahi kujaribu Google earth Pro?.
 
Mmh! Mbona mi niko kitiizii!

Embu kama unasimu kubwa jaribu kugugo 'application: google earth' or google map.

Katika simu nyingi tu za kisasa wameekewa hiyo kitu, tatizo ni kwamba wengi hawajui kuitumia. Coz nimewaelekeza frnd wangu kama watatu namna ya kutumia huku nikiwashawishi wengine wadownload hiyo makitu.

Watu wengi hushindwa kuitumia au kuiona haina maana kwa kushindwa kuibadili mwonekano wake kutoka map view kwenda satelite view.

Ukiidownload inakuwa ktk map view.

Google Earth ndiyo nayotumia, hata nikiangalia hapa nilipo tu naona iko off zaidi ya miezi miwili kwa sababu kuna jengo hapa limeezekwa mwezi wa saba lakini halipo kwenye ramani!!
 
excuse me,toka enzi za ukoloni?!...how comes ile inayotumiwa na CNN provides real time images?.umewahi kujaribu Google earth Pro?.

mipaka ilishakuwa defined na wakoloni enzi hizo upande wa Tanganyika hatukuwa na chezu mpaka ulikuwa kwenye ufukwe wa ziwa, hao google earth wamefuata ramani za mkoloni! angalia kwenye vitabu vya zamani mkuu utaona mipaka ilivyo.
 
hayo mambo ya mipaka ni google map.mada inaongolea google earth.
 
nilikuwa nareffer propaganda za mwandishi kusema wameingiza mipaka kwenye google earth!
"Hapa kwetu suala la google earth liliwahi kuleta mgogoro kidogo baada ya watu kutumia programu hiyo kuweka mipaka ya Ziwa Nyasa na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii kama vile ndiyo halisi kumbe haikuwa na ukweli wowote."
Google Earth hawana matatizo wao wanakupa satelite image, wanaochora ramani ni walio chini, na hizo ramani nyingi wanareffer kwenye ramani za enzi za mkoloni!
 
Kama mnakumbuka hata kwenye ile ndege ya "iliyopotea" wachina ndiyo walikuwa wanatoa picha ambazo ziko updated, lakini si live feed, kupata live feed ya dunia nzima si jambo la mchezo itahitaji maelfu ya satellite!
 
Back
Top Bottom