Google (GMail) imekuwaje?

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
Google siku hizi imekuwa takataka. Wakati wanajaribu kuboresha ulinzi kwenye data za mtumiaji wa huduma zao kumbe ndiyo wanaharibu kabisa.

Simu yangu iliharibika, sasa account yangu ya GMail ndiyo ipo kwenye hiyo simu. Leo nimebadilisha simu lakini cha ajabu siwezi ku-access account yangu kwasababu tu nimetumia kifaa kipya na hakuna njia nyingine ya kuthibitisha kuwa mimi ndiyo mwenye account.

Huu wanaofanya Google ni ujinga, ingekuwa naweka taarifa zisizo sahihi (password) hapo sawa ilipaswa kuzuia mimi ku-access hiyo account lakini sababu ya kuwa kifaa ni kipya ila password ipo sawa na bado sipati access ni mapungufu makubwa sana kwa GMail.

You can’t recover your account at this time because Google doesn’t have enough info to be sure that this account is yours.
 
Bro ni changamoto za kimtandao tu seriously hakuna kitu kama hicho, mimi naunga account yangu ya Gmail kwa simu zaidi ya 3 kwa siku na sijawahi kuona hiyo changamoto, labda changamoto kubwa niliyoiona ni kwenye kufungua account mpya, kama tarehe yako ya kuzaliwa haikumechi na tarehe ya kitambulisho ulichosajilia line ndio utakuwa umeyatimba, maana hautoweza kumalizia kufungua account.
 
Kaa nao chini mmalize tofauti zenu.hawana shida hao
 
tumia browser ku log in halafu zima au switch off 2 step verification halafu tengeneza au create passkey
 
Ndo maan mnashauriwa muadd two-factor recovery mode sidhani kama ungeteseka mkuu, anyway pole kwa tatizo lililokupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…