Google inajaribu kuweka mfumo wa kuchuja kelele kwenye calls

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Katika Android 13, kuna kipengele kipya kinaitwa “Clear Calling”. Kipengele hicho kinawezesha kuchuja na kuondoa kelele ambazo zinasikika kwenye calls.

Mtumiaji wa Android 13 akiiwasha option hiyo, inaonekana inachuja kelele za background na inasaidia kama mtumiaji akiwa anaongea na simu katika mazingira ambayo kuna kelele.

Google ilianza kujaribu mfumo wa noise-canceling katika chip yake ya audio ambayo ina cores 6. Ina mfumo ambao una akili bandia ambayo inaweza kutambua aina za sauti, kelele, vitu na mazungumzo. Na inaweza kuchuja sauti ambayo haitakiwi mfano kelele na background noise.

Chip hiyo ipo katika Pixel Buds Pro ambazo zimetoka hivi karibuni. Google imesema data zote hazitoki nje ya simu na hakuna sauti ambayo itatumwa Google. Kazi yote ya kuchuja sauti inafanyika katika chip ya simu na Pixel Buds bila kutumwa nje ya simu au kutumia intaneti.

Bado swali kubwa linabaki katika usalama wa teknolojia hizi. Je ni kweli chip za Earphones na simu hazitumi sauti nje ya simu? Je hazihifadhiwi na kutumika bila watumiaji kufahamu?

So, Android 13 itakuwa na uwezo wa kuchuja sauti na feature hii itasaidia kuwezesha watumiaji kuongea na simu katika maeneo ambayo kuna kelele.

Credit: ItsApolloo
 
hii itasaidia sana hasa ukiwa kwenye mikusanyiko au sehemu zenye kelele za vitu/watu mbalimbali. nasante sana teke linalokujiaaaa
 
watu wa apple kupitia facetime audio call ni kama mko room moja na mhusika.

wafanye haraka.
 
Katika Android 13, kuna kipengele kipya kinaitwa “Clear Calling”. Kipengele hicho kinawezesha kuchuja na kuondoa kelele ambazo zinasikika kwenye calls.

Mtumiaji wa Android 13 akiiwasha option hiyo, inaonekana inachuja kelele za background na inasaidia kama mtumiaji akiwa anaongea na simu katika mazingira ambayo kuna kelele.

Google ilianza kujaribu mfumo wa noise-canceling katika chip yake ya audio ambayo ina cores 6. Ina mfumo ambao una akili bandia ambayo inaweza kutambua aina za sauti, kelele, vitu na mazungumzo. Na inaweza kuchuja sauti ambayo haitakiwi mfano kelele na background noise.

Chip hiyo ipo katika Pixel Buds Pro ambazo zimetoka hivi karibuni. Google imesema data zote hazitoki nje ya simu na hakuna sauti ambayo itatumwa Google. Kazi yote ya kuchuja sauti inafanyika katika chip ya simu na Pixel Buds bila kutumwa nje ya simu au kutumia intaneti.

Bado swali kubwa linabaki katika usalama wa teknolojia hizi. Je ni kweli chip za Earphones na simu hazitumi sauti nje ya simu? Je hazihifadhiwi na kutumika bila watumiaji kufahamu?

So, Android 13 itakuwa na uwezo wa kuchuja sauti na feature hii itasaidia kuwezesha watumiaji kuongea na simu katika maeneo ambayo kuna kelele.

Credit: ItsApolloo
mie nina google pixel 6 pro nimeupdate juzi kwenda android 13 ila hiyo calling clear sijaiona wala kuipata!!

Sent from my Pixel 6 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom