Google Map Street View Africa na Tanzania kwa Jumla

Google Map Street View Africa na Tanzania kwa Jumla

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
UKwa kutumia google Map unaweza kuona hali hali halisi ya sehemu mbalimbali za dunia na kuzifahamau hata bila kufika. Hii imekuwa pia inasaidia watalii kutembelea sehemu fulani za dunia kujihakikishia wanyaoona huko Google maps.

Ukiangalia ramani ya dunia, utaona kuwa Amerika ya Kusini, Amerika ya kaskazini, Ulaya na sehemu kadhaa za Asia (ukitoa china na korea ya kaskazini) zimejionyesha vizuri sana kwenye google street view. Mashariki ya kati, Asia karibu yote (isipokuwa Korea ya kusini, japani na nchi za Aisa ya kusini mashariki) na Afrika ndiko kuna utata sana; kwa Africa ni Senegal, Ghana, Nigeria, kenya na Afrika ya kusini tu ndizo zinazopatikana kwenye google viewe. Tanzania pamoja na uzuri wake haimu kabisa labda mitaa kadhaa tu ya Zanzibar.

Ona hapa, Amerika ya kaskazini yote ipo ispokuwa tu eneo la kaskazini ya Kanada ambalo halikaliwi na watu wengi
1642707543908.png


Amerika ya kusini pamoja na visiwa vya kcaribbeana imo ispokuwa Cuba, Venezuela na msitu wa Amazon
1642707683689.png

Ulaya yote imo
1642707757086.png


Sasa ona mashariki ya kati na Asia,
1642708128959.png


Sasa geukia Afrika uone

1642708227328.png


kwa Tanzania inabidi uende Zanzibar mndipo ukute hii

1642708293512.png


Niliuliza Google kwa nini kuna sehemu hazipo kwenye gpoogle map, wakaniambia kuwa huenda hawajapata mtu au kampuni ya kuwapigia picha hizo, au mamlaka za nchi husika zinazuia. Kuna malipo si haba wanatoa kwa mtu anayewapigia picha za mtaa mzima lakini anatakiwa awe na vifaa vya google vinavyonganisha picha hizo moja kwa moja kwenye ramani ya google. Picha za sehemu moja kama sehemu fulani ya biashara hizo hazilipiwi. Sidhani kama serikali ya Tanzania inazuia picha hizo hivyo Watanzania wote magari mazito ya kuweza kuzungukia nchi nzima changamkieni tenda hiyo.
 
Vip kuhusu sheria za nchi

Maana najua wazee wa fursa wapo Ila ukiona hawachangamkii ujue kuna shida mahali
 
Mbona Iran wanasema wamepata picha toka kwenye Satelite? Au kwamba Nasa na Google hawezi kushirikiana?
 
Mbona Iran wanasema wamepata picha toka kwenye Satelite? Au kwamba Nasa na Google hawezi kushirikiana?
Google map ni picha za mitaani, wakati aeriel view ndizo picha Satellite. Hizo picha za Satellite zinapatikana kwa dunia nzima, lakini picha za mitaani ndizo tatizo. kwa mfano ukeinda pale Zanzibar Koani njia panda, mitaani panaonekana google hivi



1642712426691.png

Lakini kwenye satellite panaonekana hivi

1642712094069.png
 
Back
Top Bottom