Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Megan Garcia ameshtaki Google na kampuni ya akili Mnemba inayohusika na "Chatbot" kwa madai ya kuhusika katika kifo cha mwanaye Sewell Setzer (14)
Inadaiwa Sewell alikuwa akiwasiliana kimapenzi na programu ya "Chatbot" akitumia mhusika wa "Game of Thrones" Daenerys Targaryen, ambapo baadae alimshawishi kijana huyo Kujiua
Mnamo Februari 2024, Kijana huyo alijipiga risasi baada ya chatbot huyo kumshawishi mara kwa mara kujitoa uhai
Megan anadai fidia ya kiasi amabcho hakijaekwa hadharani akidai programu hiyo ilimshawishi kijana wake kushiriki mazungumzo ya kingono, ambayo yangekuwa kinyume cha sheria kama yangefanywa na binadamu.
Aidha, Kampuni ya California imedai kuendelea kufanya maboresho kwenye programu zake ili kuzuia watoto chini ya miaka 18 kukutana na maudhui ya kingono au unyanyasaji, na kuwakumbusha watumiaji kuwa programu hiyo si binadamu
Wazazi/walezi ambao mmewapa Watoto wenu Vifaa vya Kielektroniki, huwa mnafuatilia matumizi yao?