Google wameifuta blog ya Linda Ikeji

Na hawa wa huku kama lemutuz,sinta,mange wanalipwa sh.ngapii

Kampuni zinazotoa matangazo kwenye blog marketin manager wanapiga panga kwahiyo kina le mutuz and co wanalipwa 500$ per month so wakikusanya mapato ya matangazo yote wanaweza wakapata usd 2000.
 
Yaani siku hizi hawa mablogs mpaka magazeti ya udaku wana copy huku Jamie forum... Bongo Watu wavivu kuumiza vichwa!
 
Update:

Blog imerudishwa na inapiga kazi kama kawaida na ameeleza kilichotokea kikubwa ni watu wanamuonea wivu.Kupata $$ 900,000 kwa mwaka si mchezo.

Piga kazi Linda .
 

(photo source:lindaikeji.blogspot.com)

Blog maarufu ya lindaikeji.blogspot.com imerudi tena hewani baada ya kusimamishwa kwa muda hapo jana na kampuni ya Google. Sababu za kusimamisha blog hiyo ilikuwa ni malalamiko yaliyoifikia Google kuwa baadhi ya content blogini humo zilinakiliwa bila ruhusa ya wenyewe (copyright infringement claims).

Linda ikeji ni miongoni mwa mabloga wakubwa barani Africa na labda bloga tajiri kuzidi wengine. Vyanzo mbalimbali vinakaridia kuwa Ms Ikeji huingiza zaidi ya milioni 50 za Tanzania kila mwezi kutokana na matangazo katika blog yake. Kukupa picha, tangazo moja lenye ukubwa wa pixeli 200 kwa 300 ambayo wakati naandika post hii yako zaidi ya 10 kwenye blog yake yanagharimu Naira laki 300,000 kwa mwezi, kwa bei ya mwaka jana.

Hivyo kwa mahesabu ya haraka anaingiza zaidi ya Naira milioni 3 au zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 30 kwa mwezi kupitia matangazo haya pekee, ukiacha mbali aina zingine 4 za matangazo kwenye blog yake.

Mara kadhaa Ms Ikeji amekuwa akisherehekea mafanikio yake kwa kuonyesha vitu mbali mbali anavyoweza kumudu kununua kupitia blog yake. Mwaka jana aliweza kuwajengea wazazi wake nyumba na mwaka huu aliweza kuongeza Range rover ya kisasa (2014) katika collection yake ya magari mengine ambayo pia alinunua kupitia mapato ya blog yake. Kwa wale ambayo mtakuwa inspired kumfuata nyendo zake kumbukeni kuwa alianza blogging tokea mwaka 2006.


(photo source:lindaikeji.blogspot.com)
 
Hata hivo kwenye blog lake anaandika vitu vya maana si kama hizi za bongo kutangaza picha za fumanizi
 
Kwa watumiaji wa blackberry Z10,blog inapatikana mda wote tangia majuzi##
 
Hiyo itakuwa siri yao sidhani kama watasema,ila nadhani yule wa zoom atakuwa anaingiza hela

Michuzi nafikiri ndio blogger anaeingiza pesa nyingi kwa matangazo.
 
Michuzi nafikiri ndio blogger anaeingiza pesa nyingi kwa matangazo.

Yah ila may be kwenye matangazo kwa sana,ukiangalia hana google adds,wenzetu wanaingiza hela Google adds
 
Du nilitaka Kudata bora imerudi ...Linda na Bela Naija sikosi kupita aiseee ....wenzetu wapo mbali
 
Aaaa huyu pia ana ugomvi na mange nimemgoogle nikampata

Mhhhh! Shosti unavyotuchukiaaa! hivi unakumbuka alichukua Picha za Mamiss Tanzania kwa Mange na kwenda kupaka kwenye Blog yake eti Wanawake wa TZ na Nigeria wapi wazuri ?? acha watuseme Ndio kajiugomvi kalipotokea Jamani ...Mnyonge Mnyongeni lol !
 
Du nilitaka Kudata bora imerudi ...Linda na Bela Naija sikosi kupita aiseee ....wenzetu wapo mbali

Sisi ni copy cats mpk blog zimegeuka kero... WaTz tumefanana sana kiakili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…