GooglePesa platform matapeli wapya mjini

Last Seen

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
229
Reaction score
566
Habari wana JF,

Kampuni inayojitambulisha kama GooglePesa Platform iliyojikita jijini Arusha na kuendesha biashara ya utapeli kupitia mtandao (www.googlepesaplatform.com).

Kampuni hiyo ina muundo sambamba na iliyokuwa Kampuni ya Kalynda.

Wanatumia website na application yao iliyopo playstore.

TCRA na vyombo vya Usalama viingilie kati kabla wananchi hawajalizwa.
 
Tatizo wananchi hawasikii, kila likija lile lile lenye muonekano mpya, wanaruka nalo. Mwisho wa siku majonzi.

Wananchi wakibadilika haya mambo yataisha automatically.
 
Nishakua victim wa scatec na idea debator lilac mining na kijiji app sahz sitaki kusikia kuhusu online platform 🚮
 
Hi
Hivi ipo platform ambayo sio matapeli kweli?
 
TCRA wapo kwa ajili utukane serikali au usambaze video.
kama inalipa kodi na vibali achana nayo.

Mi na shuudia kampuni imekodi jengo la serikali hapo kuna TRA,NSSF,TAKUKURU,MKUU WA wilaya,mkurugenzi,nyuma kituo cha polisi kikubwa na usalama ila wapo kimya.

Nyamaza watu wapige pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…