Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 35,566
- 104,386
GoPro Hero ni jina maarufu sana kwa wapenzi wa camera, especially Action Camera.
Tokea Hero 1 mwaka 2009 hadi Hero 13 Black mwaka 2025 mengi sana yametokea kuboresha tasnia ya Action Camera.
Upinzaji mkubwa kutoka DJI Osmo Action umemaumbua sana GoPro siku za usoni, na baadhi ya watu kusema toka Hero 9 hadi Hero 13 hakuna mabadiriko makubwa ya ubora wa camera zaidi ya features ndogo ndogo tu.
Sasa jana tarehe 14 April 2026 GoPro wamebadirisha uelekeo kabisa na kuachana na Hero series, na kutambulisha Mission 1 Series camera. According to GoPro, “haya mabadiriko siyo tu mabadiliko ya jina, bali ni mabadiliko ya falsafa kutoka kwenye camera ya kawaida ya mkononi kwenda kwenye camera ya kiwango cha filamu (Compact Cinema Camera)”.
Manadiriko aya makubwa ni baada ya GoPro kushtukia kuwa soko la sasa la maudhui (content creation) limebadilika; watu hawataki tu camera inayostahimili maji au higher altitude kama Hero series zilivyo, bali wanataka ubora wa picha unaoweza kushindana na camera kubwa za kiprofesheno.
Hadi sasa, GoPro wamezindua Mission 1 Series tatu, ya kwanza ni Mission 1 Pro (hii ndio flagship), ya pili ni Mission 1 Pro ILS na ya tatu ni Mission 1 standard.
Kupitia Mission 1 Pro, GoPro wameleta kitu ambacho wadau wengi walikuwa wanakililia kwa miaka mingi: 1-inch Sensor ya 50MP na uwezo wa kurekodi video za 8K/60fps.
Mission 1 Pro ILS (Interchangeable Lens System) ni habari njema sana kwa "creators" wa hapa nyumbani Tanzania wanaofanya mambo ya kitalii au sinema fupi. Kwa mara ya kwanza, GoPro itakuwa na mount ya Micro Four Thirds (MFT), ikimaanisha unaweza kufunga lenzi tofauti tofauti (prime au cinema lenses) kwenye GoPro. Hii inaiondoa GoPro kwenye kundi la "just a camera" na kuiingiza rasmi kwenye kundi la Professional Workhorses.
GoPro pia wamezindua chip mpya ya GP3 Processor. Hii chip siyo tu inaruhusu 8K, bali itasolve kero ya muda mrefu ya GoPro overheating na kuzima katikati ya kurecord. Pia, wameleta teknolojia ya 32-bit Float Audio, ambayo kwa lugha rahisi ni kama sound isolation wakati unarecord especially kama unarekodi kwenye mazingira yenye kelele nyingi au upepo mkali.
Nadhani sasa DJI na Insta360 wamepata challenge.
BTW mwezi huu pia DJI atazindua best selling camera DJI Osmo Pocket 4 baada ya kufanya vizuri sana kwenye Pocket 3.
Content Creators, andaeni pesa.