GoT - Mnafanya nini kuhusu hii meli ya Zanzibar?

Kafrican

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2015
Posts
7,251
Reaction score
7,037
Nilikua nasoma story flani, nikapata hiipicha hapo chini, kuna meli flani inayoitwa "Lucky star Zanizibar" ilishikwa na tani 15 za samaki bila kibali cha kuwa ndani ya maji ya kenya.... meli hio ilishikwa mwaka wa Mei 2014 hadi sasa haujawahi achiliwa,

Meli kama hii yenye uwezo wa kuvua samaki zaidi ya tani 15 ni thamani kwa uchumi wa nchi kama Zanzibar/Tanzania yani (Blue water economy), nashangaa ni hatua gani (za kisheria au ki diplomasia) serekaliya Tanzania imechukua ili meli hii irudi majini na kufanya kazi, manake nijuavyo mimi kama ni meli ya Kenya ingekua imefanyiwa hivi hakungekalika, kama serekali ingezubaa kidogo tu, ingekua kila mwezi wanahabari na wanasiasa bungeni wanawapatia pressure serekali kwa kuwakumbusha wananchi kwamba meli inaoza bandarini mwa nchi nyengine. nimetafuta online na sijaona hata tovuti moja ya kiTz inaongelea kuhusu hii meli inayoooza pale mombasa...

Aama hii meli si yenu???



Tanzanian fishing vessel Lucky Star Zanzibar with registration number 51M387 at Mbaraki Wharf Mombasa , the vessel with 15tones of fish has been held since May 5,2014, since it did not follow required bureaucratic by conducting it activities in Kenyan water .Photo Elkana Jacob

Kenya may ban international fishermen from her waters

Tanzania vessel seized in Kenya
 
Sasa hii taarifa yako ndo itaamsha bongolala. Hivi karibuni wataipeleka kule instagram. Hehehe ni ajab.
 
Hahahaha kumbe sio bombardier peke yake...Wanapovu Mkono wapi ama ni kimya kimya tu.
 
Inaonekana ueleo wako wa uandikishaji wa meli ni mdogo. Meli inaweza kuandikishwa na kupeperusha bendera ya nchi fulani lakini sio mali ya hiyo nchi. Kenya imepata vyuma chakavu, sasa ulitaka GoT wafanye nini?
 
labda ingekuwa serekali ya tanzania ndo imekamata.ungeona wakosoaji watako jaa hapa na roho za kwanini.
kinacho nichosha sasa hivi watanzania tumekuwa kama waswahili ambao tunaishi mtaani nao unapo fanya maendeleo wana kasilika hata kukufanyia makusudi ilimradi wakukosoe tu.
hakuna hatakaye sumbuka na huzi wako kwa sasa wanadili na magufuli
 
hahaha... kule wanapapurana balaa
Sijui huku Kenya tuanze teamKaligraph vs teamKingKaka angalau tusahau siasa. TeamKaligraph kwa jina lingine tutakuwa tunawaita Nightwalkers au ukipenda Wazunguu. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Una akili sana. Wengi wa wabongo wana inferiority complex so kwa Kenya kama ndio wameikamata wanaona poa Lin ingekuwa ni huku kwetu, wangekesha kuitetea Kenya kuwa, sisi ni wachokozi sijui hatujui diplomacy na mengine kibao.
Mpaka leo watu wengi wanamlaumu JPM kwa hatua yake nzuri ya kukamata meli ya uvuvi kuwa kailetea nchi hasara, hapo bado huoni tatizo la wabongo?
 
Reactions: Oii
Watanzania huwa tuna argue na common sense hiyo meli sio ya Tanzania wala ya mtanzania zanzibar imeshatumika sana na maharamia kusajilia meli zao ikiwamo Iran, North Korea, Saudi etc

Hivyo watanzania hatuna akili za mbayuwayu kugombana na visivyotuhusu kisa tu titled Tanzanian huo ulimbukeni mnao nyie kupiga mayowe kwa vifaranga vya mtanzania kisa tu vimetokea Kenya.
 
Sources of your evidence please?
 
It is true, many North Korean ships have been caught registered as Tanzanian or Zanzibar
Yes, many ships but not this one. Provide credible evidence to support your claims. Kama sio ya Tz ni ya wapi?
 
Nakubali sheria ziwe zinachukua mkondo wake, walipe fidia inayotakiwa ili ikombolewe.
Wao wanajinasibu kukamta vya wenzao lakini Tz wakikamata ngombe waliongia bila kufuata sheria ya nchi wanalilia sana. Hawa jamaa ka mademu kulialia kwingi. Sheria ni msumeno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…