GPA yako ndo itakupa ajira

BUMIJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
5,950
Reaction score
11,295
Wadau vyuo vimekua vingi sana na wahitimu ni wengi.Tunapoelekea tetesi ni kua itafikia kipindi wenye GPA kali ndo wanaajiriwa kama udokta,ualimu,wahandisi
 
Mkuu hivi unajua vigezo vya ajira kweli???Unajua kuna watu wana GPA kubwa lakini kichwani hakuna kitu.???Maana kabla ya kupata hiyo ajira kuna usaili (oral and written)
 
Mwakani kwenye ualimu wanaangalia iyo.
 
dah fikiri vizuri jog coz GPA SIKU HIZI zinanunuliwa mtu anaweza kua na GPA kali ila ndani ya kichwa hewa
 
Tanzania lakini cheti Mbele
 
Bhululu kwa iyo Gpa sio ubora wa kazi
 
Mbisom just romours or grapevine
 
Sam Love ni kweli
 
kumbe unahisi..sasa hiyo heading mbona kama una uhakika. Ajira ni cheti kuanzia pass mpaka first class na uzoefu tu mkuu,wanacheza hapo! Mengine yote mbwembwe!
 
Bhululu kwa iyo Gpa sio ubora wa kazi
Mkuu GPA isikutishe, ingawa ni vizuri kuwa na GPA nzuri.Ila katika vigezo vya kupata kazi, vitu vingi sana vinaangaliwa.Mbali na GPA kwenye cheti, mwajiri atataka kujua je, kilichoko kwenye cheti na kichwani vinaendana?? Sasa hapo mtu anaweza kuwa na 'A' za IT, ila hata kuwasha computer hajui!!!
 
Bhululu kwa iyo kilichopo chetini sio cha kichwani sometimes
 

Hahahahahahaha!mkuu umenichekesha aisee
 
Ajira kama kufundisha sawa. Ila ni better ukawa upo fiti kote.
 
Saa Mbovu hivi perfomance in exam na utendaji ni sawa?
 
kupata mwajiriwa mzuri kuna vigezo vingi vinaangaliwa mbali na GPA.

kuna formula moja inaitwa SWOT.. strength, weakness, opportunities and threat analysis.

kwa mwajiri mzuri, lazima aangalie hivi vitu either katika interview au wakati wa kazi..

una labourers wengi hubweteka sana makazini na kukalia kujisifia gpa walizopata vyuoni badala ya kufanya kazi.

ndio maana siku hizi kigezo kinachonagaliwa sana ni personal attitude toward a certain job unayofanya. creativity, spirit na kujitoa kwako.

japokuwa gpa inachangia sana kukupa kazi, lakini vigezo nilivyotaja huko juu ni vya msingi sana!
 
GPA nzuri ni ufunguo mzuri wa kupata interview, kama unaangalia matangazo ya kazi sikuhizi wana tabia ya kutumia GPA kama kigezo kimojawapo,ishu ni kuwa nafasi za kazi ni chache na wanao graduate ni wengi hasa katika fani za social sciences, hivo basi kwa kuwa hawana uwezo wa kuwaambia msitume maombi, wanachofanya ni kuwapunguza kwa ukubwa wa GPA ,wanajua wanafunzi wengi wana lower na pass, hivyo watataka upper na first..ushauri ni kujitahidi uwe na GPA nzuri pia ujifunze mengi kwenye fani yako ili uonekane mjuzi pia kwenye interview.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…