GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti

MENISON

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
726
Reaction score
621
Naona matangazo ya kuongeza elimu, kazi n.k eti GPA sijui above 3.8, wengine 4.0 n.k n.k
Sasa swali langu je ni ya chuo gani? kwasababu kuna vyuo unaanza mpaka unamaliza hakuna mtu aliwahi kupata GPA ya 4 mifano tunayo ,na kuna baadhi ya vyuo yaani watu wameishia GPA ya 4.0, ukiangalia GPA zao ni vichekesho eti 4.9, 4.8 siuji 4.7 ambayo mimi na U T.O wangu siwezi kwa hiki chuo nilichopo. Elimu ya chuo kikuu bongo ya kijinga kungekua na TCU examinations watu washindane GPA ila sio uhuni wengine wanapewa wengine wananyimwa.
Yaani ni sawa necta zisingekuwepo halafu unachagua watu kwenda Form Five kuangalia matokeo ya shule zao ya terminal unaweka cuuttpoint kabisa kuanzia 75,na wakati kila shule ilifanya mtihani wake .Nazungumza hivi kwasababu kuna shule wastani utakuta wanaanzia 65 wengine 95 n.k
Hakuna elimu mbovu kama ya chuo ,unfair.. elimu form IV tu na six huku kwingine mbwembwe ,ngoja na mimi nianzishe chuo changu wanafunzi GPA zao hazitakua chini ya 4.5 wote wawe na vigezo muhimu .
 
Umeongea ukweli UDSM gpa wanatubania, nenda SAUT , ST.JOSEPHY gpa wanapewa tu
 
Acha uongo we kama kichwa chako kibovu acha kuweka rawama me nilienda ofis za udsm pale sabasaba kila department wakanipa true fact ya usomaji na upataji wa gpa nzur na list ya waliofanya vizuri tangu chuo kianze
 
Kweli mkuu hizi kazi utakuta hata serikali wanatangaza sifa uwe na GPA 3.5 above hawa wenye 3.4 below hawana haki kuajiliwa?
 
Umeongea ukweli UDSM gpa wanatubania, nenda SAUT , ST.JOSEPHY gpa wanapewa tu

Acheni ujinga madogo, someni.
Mm nimemaliza UDSM law, tena miaka ile wakati chuo kina sifa zake (acha skuhzi kimejaza vilaza), gpa yangu ni 4.1, nilipewa bure?
Ujinga wako usiulazimishie kwa watu wengine.
Ushinde unacha facebook halafu upate 4!!!?
 
Tumaini wanatoa au sio?

Hicho cha Tumaini sijui siwezi kuelezea,nimeongelea SAUT ninachokifahamu.Humu kuna watu wanafuata mkumbo tu bila kujua ukweli wa mambo!
 
Hicho cha Tumaini sijui siwezi kuelezea,nimeongelea SAUT ninachokifahamu.Humu kuna watu wanafuata mkumbo tu bila kujua ukweli wa mambo!

SAUT na Tumaini vinasifika kwa product zao haziendani na GPA walizo pata.
 
Acheni ujinga madogo, someni.
Mm nimemaliza UDSM law, tena miaka ile wakati chuo kina sifa zake (acha skuhzi kimejaza vilaza), gpa yangu ni 4.1, nilipewa bure?
Ujinga wako usiulazimishie kwa watu wengine.
Ushinde unacha facebook halafu upate 4!!!?

Maisha hayaangalii Gpa soma elimika, pata hela basi acha kulalamika humu hata uwe na gpa ya 5/5 na huna skills on hand na huna hela ni HASARA
 
Acheni ujinga madogo, someni.
Mm nimemaliza UDSM law, tena miaka ile wakati chuo kina sifa zake (acha skuhzi kimejaza vilaza), gpa yangu ni 4.1, nilipewa bure?
Ujinga wako usiulazimishie kwa watu wengine.
Ushinde unacha facebook halafu upate 4!!!?

hata mwigulu alikushinda? Na ana pumba kuliko wewe
 
Hivi JK alikuwa na GPA ya ngapi? Maana huyu ndo rais wetu, tena sisi wenyewe ndo tumemuajiri..!
 
Back
Top Bottom