GPA zetu bongo kweli ni kizungumkuti


Uzungumzii U T.O???Soma maandishi mekundu, ni ya nani yako ama.
 
Uzungumzii U T.O???Soma maandishi mekundu, ni ya nani yako ama.
Hujaelewa mada mkuuu
ndo wewe una watoto au wadogo zako wanasoma shule tofauti wanakuletea matokeo ya terminal unaangalia mwenye wastani mkubwa unasema ndo kichwa ,inakuja necta ndo anakula zero....
Kama uwezo wangu ningependekeza TCU examinations kama cambridge vyuo vyote koz zinazofanana wanafanya mtihani mmoja ,hapo ndo utajua nani mkali sioo siasa hadi kwenye elimu
 

Okay,mi huwa si argue mdogo wangu,punguza ukali toa hoja,ulikua una maana gani kutoa reference iyo niliyoiwekea red,..kukusaidi kwa hiyo reference yako ni kweli ulimaanisha kua U T.O una count.
Kubwa la msingi iyo ndio system ya vyuo dunia nzima,,,ebu funguka bwana panua mawazo yako kidogo!!!Hua Kuna List ya vyuo bora duniani, Je wote huwa wanafanya paper sawa?????
Kingine Kuna mtu kakusaidia GPA si sawa na ufanisi kazini, therefore usilalamikie GPA!!!weka akilini hilo litakusaidia na ukifika level ya kufanya kazi utalitambua hilo
 
Vyuo vya private wanauza gpa tu hamna lolote,udsm hamna pumba hizo ndo maana kinafanya vizuri katika viwango vya kimataifa..najua inawauma lkn ukweli ndo huo wadau
Proudly a UDSM alumni
 
Hivyo vyuo unavyoviona vigumu kuna wanaopata gpa kubwa. Soma dogo acha kupiga mayowe.
Gpa haitafutwi kwa malalamiko. Pia sio kila ajira wanaangalia gpa, kama unataka hizo zenye kujali gpa piga msuli kweli na uache kulalama. Ukikua utaelewa nachozungumza.
 
Utakuta mtu ana GPA ya 5.5 lakini utendaji wake ni wa ovyo kupindukia, na hawajui kimombo! Sasa mtu utajiuliza, "hivi huyu alipataje GPA kubwa kiasi hiki ilhali anaonekana kilaza?". Na mtu mwenyewe labda mwanamume, ingekuwa mwanamke labda ungehisi 'kavua'! Du, majanga!
 

Wasomi wa dot.com mnachekesha sana!! Mnashindana kupata GPA za juu wakati mko empty headed when it comes to skills & knowledge!! Shame on you!!
 
Haaaa ndugu yangu umeonekana na ww kuwa upo kwa ulimwengu wa JF lakini kwakukumbusha au kukuelimisha juu ya unalosema tu uwemjanja hata kdogo basi HAKUNAGA GPA 5.5 ktk taifa hili labda iwe yako wa kwanza na hauna kitu kichwani ndio maana unajumuisha wote kumbe ni yako peke yako hiyo gpa ya 5.5 aiseee
 
narafiki zangu watatu wame soma OSMANIA university, wote wana first class...cha kushangaza bongo walikosa vyuo!.
 

GPA 5.5 Tz??????mkuu aliyeandika ni wewe ama?
 
Mkuu GPA ya 5.5 inatokea sayari ya mars au? Au ndo nyie bora kuchangia tu hata kama mada hujaelewa...chuo umesoma combination gani? Labda chuo chako kilikua pia na combination n nat faculty
 
Waambie maana kwa uchunguzi mdogo tu niliofanya mpaka sasa hivi wengi wanaotoa kauli kama hii ya presenter wa leo ndii wenye gpa za 2.0-1.9 hivyo kupeana moyo ndio wanasema hvyo. Wise boy hebu tafakuri km mwenye gpa 4 n kilaza je wao wenye 2.0 watakuaje. Madogo someni muweze zitetea degree zenu mcjipe moyo kijinga namna hii
 
Inauma sana but ndo maisha tuliyonayo, tujitahidi kuongeza skills kwa kuwa tumebarikiwa kuwa ufahamu mkubwa na tukanyimwa GPA tukipata hata nafasi kdg tuwe so different na walopewa GPA,
 
Yaa waambie kama wameshindwa elewa maandishi walio andikwa na watu wengine wa elewe hata kwa kusikia hata maneno ya wahadhiri wao waweze kuja ztetea hzo gpa zao na tuweze jua ipi ya kupewa na ipi ya kujisukumasukuma
 

na bodi za wanazuoni kama nbaa, body ya procurement, body ya bank, body ya wakandarasi, chama cha wanasheria(tanganyika lawa society) watafanya nini?
Kumbuka hata kama una gpa ya 5.0 ili kutambulika na hizi body lazima ufanye mtihani wao.
Vyuo viendelee kutoa gpa hata kama mtu hajafanya mtihani, ila kuwe na body ktk kila fani ya kitaaluma ambayo itatoa mtihani wa jumla bila kujali chuo unachotoka(body zote nilizotaja zinafanya hivi)
ila pia kwa nacte vyuo vyote lazima vipeleke mitihani waliyoandaa ipimwe kama imekidhi viwango kabla haijafanywa, sina uhakika kama tcu wana hichi kitu.
Pia kulingana na kalenda ya vyuo huwezi kusema vyuo vyote vifanye mtihani mmoja, mfano kuna vyuo vimefanya UE may(tia, iaa etc) vingine june(udsm, duce,) na vingine ndo wanafanya nw (cbe, st John, ustawi)
unaset vip mtihani hapo?
Maadam kuna prof bodies acha waendelee ila watakapoletwa kwny body ndo tutajua gpa ya kupewa au kutafuta mwenyewe
 
Nimesoma uzi wa jamaa nilivyouelewa ni kwamba jamaa anachodai ni hawa wadau TCU kusimamia kwa dhati hii elimu ya juu maana hata mie kiukweli kwa miaka hii ya karibuni unakuta dogo amemaliza chuo na ku-perform vizuri lakini mwisho wa siku ukimwangalia unamwona yupo shallow kinoma. Kinachotakiwa TCU kuangalia namna ya kufuatilia hivi vyuo vinginevyo tutasema vijana wetu wana degree kwa kuwa tu wanavyeti lakini ukifanya assessment ya kiundani ni kama vile wana Diploma maana vyuo kiukweli vimeanzishwa kwa kasi kama shule za kata pia hata process za kuwapata wahadhiri nazo zimekuwa za kisiasa maana mtu anamaliza leo anabakishwa chuo baada ya miezi kadhaa anapelekwa masters wakati anatakiwa apate mentor kwanza kwa miaka kadhaa ili aweze kupata practical experience ya kutosha kabla ya kufanya mambo mengine.

Ni kawaida siku hizi kumkuta dogo tangu mwaka wa kwanza mpaka wa tatu amefundishwa na TA tu na wahadhiri wachache waliobobea, kwa mtaji huu hata wale wenye GPA kubwa kuna ambao ni za zali na wengine za kiukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…