Sikuwa na nia ya kutia neno kwenye andiko hili lakini baada ya kuona GPSA imetajwa imenibidi nifungue account mpya nishare experience yangu ya kuwa pale kwa takribani miaka 9 kabla ya kuhama . Account yangu iliyozoeleka haitanipa uhuru Kuna watu humu najuana nao wengi na tunafamiana katika maisha halisi nisingependa wanifahamu , hii account itanipa uhuru zaidi na najua kabisa Mr Malik mwenyewe atanifahamu kwa maelezo nitakayotoa hapa na nataka anifahamu kwa sababu hana cha kunifanya na ananijua vizuri sijawahi kumtetemekea.
Alichokisema Mkuu
mwamba02 na hasa mdada
CuteJancs ni ukweli kabisa, Huyu DBSS wa GPSA Mr Malik hafai kabisa kuwa kwenye ofisi yoyote ya umma katika utawala huu wa Magufuli achilia mbali GPSA bali anatakiwa awe nyuma ya nondo za magereza hapa TAKUKURU fanyeni kazi yenu na Tanpol pamoja na maafisa usalama wa taifa hili.
Kiukweli huyu jamaa sio mtu sahihi kwa ustawi wa GPSA ni mwizi wa mali za umma anaeishi maisha ya anasa KIGAMBONI na anamiliki zaidi ya Yard 3 za kuuza Magari hapa mjini, huku akiwanyanyasa wafanyakazi wake,
Lakini najua TAKUKURU mnamfahamu huyu DBSS wa GPSA, kwa sababu hata taasisi aliyotoka TACAIDS alikuwa na skendo ya wizi na ambayo nadhani bado mnaichunguza na sijui mnakwama wapi kwa huyu mtu japo inasadikika anatumia ulozi/uchawi sana ili kuficha mambo yake, Lakini ni kweli mmeshindwa kwa ajili ya hizi nguvu zake za giza anazotumia? Huyu akiondoka GPSA na akapatikana mtu smart kwenye hicho kiti na mwenye maono na asiye na maslahi binafsi GPSA itapiga hatua, hii iko wazi kabisa.
Huyu jamaa ana swahiba wake wa kabila moja pale utumishi, Somebody Sanga kama sikosei yaani mtumishi akitaka kuhama GPSA barua ikifika utumishi kwa huyu Sanga anampigia simu huyu DBSS kumuuliza kama amtoe au amuache huyo mtumishi... Usipokuwa Ngangari GPSA hutoki huyu ameiharibu sana hiyo taasisi na Kuna somebody Mwakibinga kama sikosei alikuwa GPSA now yuko wizara ya fedha ni mtu mkubwa kidogo, ni watu wa ukanda mmoja pamoja na kwamba anaijuia GPSA vizuri na ana mamlaka makubwa zaidi ya huyu ndugu yake cha ajabu nae amegeuka kuwa Mbeleko yake.
Kuna kipindi nikiwa bado Niko GPSA alishawahi kuniita ofisini kwake akaniambia "wewe fulani Sikupendi, na sitaki uwe hapa makao makuu siku yoyote nitakupeleka mkoani, sitaki kukuona hapa mjini nilimjibu kwa confidence ambayo hakuweza kuamini, siogopi kwenda mkoani nipeleke lakini kamwe sitokubali kufanya kazi kinyume na utaratibu" hii ni baada ya kuwa nakwamisha kazi ambayo baadae niligundua ilikuwa na baraka zake haikufuata taratibu pale. Nikamfata CEO aliyekuwa anakaimu kipindi hicho Kibona nikamweleza, sijui walimalizana vipi ..., Hapa sitaki niingie zaidi kwenye Ufisadi wake hii mada nitaielezea siku nyingine, lazma huyu jamaa vyombo vya usalama vipate taarifa zake ili viaanze kumchunguza kama vilimsahau japokuwa naamini kabisa baadhi ya ushahidi binafsi wa huyu mtuTAKUKURU mnazo , Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Generali
John Julius Mbungo,tuma vijana wako upya wakaiokoe taasisi.
KWA NINI NAUNGA MKONO KWAMBA GPSA MANAGEMENT NI MBOVU?
1. Kuna Mhasibu mmoja alikuwa nadhani mkoani Kagera kama sijakosea, huyu mama aliumwa kansa tena ikawa imefika ile level mbaya kabisa na matibabu akapangiwa MUHIMBILI, akaomba uhamisho ili ahamie Dar awe anahudhuria clinic ya matibabu na akaweka na viambatanisho huyu jamaa DBSS alikataa katakata mama wa watu akahangaika wee akashindwa, Baada ya mda Ikabidi aombe hata ahamie Morogoro ili angalau awe karibu na Dar na hapa Sasa tayari kansa ilikuwa juu ilikuwa mbinde sana mpaka kumkubalia akahamia Morogoro mpaka mwaka jana mauti yanamkuta (R.I.P) eti nasikia baada ya kufa GPSA ikapeleka 600k kama rambirambi kwa familia..wakati kipindi anaumwa hawakuonesha kujali.
2. Kuna Mhasibu mwingine alikuwa Mbeya kwa bahati mbaya mama yake akapooza mwili mzima, familia yake nayo ikapata ajari ambayo ilimuua mke wake na mtoto akapooza, mama na watoto wakawa wamepooza na mke akafariki yeye ndiye akawa muangalizi wao wagonjwa bila msaidizi asubuhi anawaandaa then anaenda kazini, bila huruma Hawa jamaa wakamuhamisha wakampeleka Songwe mzee akawaeleza matatizo yake japo walikuwa wanayajua hawakumuelewa hakuwa na namna baada ya kushindikana kupewa msaada na ofisi yake akaendelea kufanya kazi akiwa anatoka mbeya anaenda Songwe, wakaona haitoshi wakamhamisha tena wakampelekwa Rukwa kumbuka ana watu wamepooza na mbeya ndiyo alikojenga na kwamba huko anakohamishiwa sio kwamba Kuna upungufu ila ni kutaka kumkomoa tu, mzee wa watu akawaeleza tena tatizo lake japo walikuwa wanajua lakini hakuna aliye muelewa mzee wa watu akapiga mahesabu kati ya maisha ya familia yake na Kazi kipi bora, Akaamua kuacha kazi ...Hebu jaribu kuvaa viatu vya huyu mtumishi wakati alikuwa na miaka michache tu astaafu (Hii nimepewa taarifa na rafiki yangu ambae bado yuko hapo GPSA na huyu mzee kwa vile namfahamu imenibidi nimpigie simu kuthibitisha na amenihakikishia ni kweli)
3. Kuna Afisa masoko mmoja alikuwa anaitwa David, huyu alikuwa ni mtu anayejua haki zake yaani ni ile aina ya watu aina yangu ngangari kwelikweli.. Huyu DBSS akamuundia majungu akampa kesi, kipindi kesi inaendelea ikatokea uhakiki wa vyeti vyeki, jamaa alichokifanya ni kuishawishi ile kamati imfute jamaa kazi kwa vile haingii kazini ( kumbuka kesi bado inaendelea) ile kamati sijui iliingiaje mkenge ikamfukuza kazi ikimuunganisha kwenye lile group la vyeti vyeki, siku wanamfukuza kazi DBSS alifanya sherehe ofisini kwake aliita wapambe wake huku akiwa mwenye furaha akawaeleza "nimemkomesha huyu harudi tena nawaambia huku akipigapiga meza na mikono yake kuashiria ushindi" baada ya huyu jamaa kutambua kafukuzwa kazi kinyemela akaenda mahakamani, kesi ikaendeshwa ikaonekana hakuwa na kosa bali alionewa, ikaamuliwa arudishwe kazini na alipwe mishahara yake yote na posho za kipindi chote alichokuwa amesimamishwa kazi...akalipwa zaidi ya 17m akarudi kazini hapohapo GPSA, kwa taarifa za uhakika huyu jamaa nasikia Sasa hivi kahama yuko chuo cha maji.
4. Kuna watumishi waliajiriwa nimesahau mwaka lakini ninachokumbuka mmojawapo kwenye intake hio ni Mhasibu wa morogoro (Benson), intake hii yote haikulipwa pesa za kujikimu.. Sasa huyu jamaa Benson akawa na uelewa akaanza harakati za kufatilia haki yake baada ya mda mrefu kupita, huyu DBSS alipoona jamaa ni mjanja Ikabidi amlipe yeye tu wengine wakabaki, huyu jamaa akawashtua wenzake nao wakachachamaa (kumbuka mda ulikuwa umeenda ni zaidi ya miaka 5 walinyuti bila malipo haya) ,DBSS alipogundua huyu Mhasibu ndio kawashtua wenzake alichokifanya ni kuanzisha bifu na mfanyakazi wake...( Utawala wa GPSA) mwisho wa siku ikabidi walipwe wote na bila hivo pesa zilikuwa zimeshaliwa.
Kuna mengine mengi nimeshau na watakaokuwepo kwa Sasa watasaidia kusema,
Kinachotokea kwenye utawala wa GPSA ni vitu vya ajabu kabisa badala ya kuwa-wamotivate wafanyakazi wao wawe na Ari ya kufanya kazi wao wanawa- stress huku wakitegemea matokeo chanya,
Pale Kitengo cha Rasilimali watu ( HR department) wengi wamegeuka kuwa genge la majungu na umbea, badala ya kubase kwenye utawala wao wapo kwa ajili kukusanya na kupeleka habari za umbeya kuhusu watumishi na maamuzi yanafanyika kwa misingi ya majungu na umbeya,Hiki kitengo kina watu wasiojiamini kabisa na wanaotegemea kujiipendekeza Zaidi.
Ukiangalia GPSA na MSD zinafanya kazi zenye nature ambazo zinafanana kwa karibu japo MSD wamebase kwenye madawa, lakini sasa kwa weledi wa management ya MSD, Ikitokea ukaichukua management yote ya MSD ukaihamishia GPSA wakawa na wafanyakazi haohao wa GPSA walio na makunyanzi unayosema na maslahi kiduchi na wasio na morali na taasisi yao halafu GPSA management yote ukawapeleka MSD wakakuta wafanyakazi haohao wanaolipwa vizuri na wenye Ari na taasisi yao, baada ya miaka 3 tu, GPSA inakuwa level sawa na TCRA na BOT na wafanyakazi watakuwa wenye furaha na maslahi makubwa kupindukia, Kipindi hicho hicho MSD itakayokuwa chini ya management ya GPSA itakuwa imechoka level za taasisi ya mpiga chapa wa serikali na wafanyakazi wake waliorithi wakiwa na Ari na taasisi yao na mishahara minono wataomba wahamie GPSA...
Nakubaliana kabisa na
CuteJancs Hawa GPSA Wana vyanzo vingi vya mapato lakini viongozi hawana Vision, wengi wapo kimaslahi.Kule Ugomboaji now hawana mpinzani nchi hii soko liko kwao tu... Lakini nenda kawaangalie.
Mpaka sasa Ofisi haina Standby Generator, Umeme ukikatika iwe week, week mbili ama Zaidi kazi zote za ofisi zinasimama, sio kwamba hawana Pesa za kununua, Ila management inachoamini ni bora wao(Viongozi) wakopeshana mamilioni kwa ajili ya kununua Magari ya kifahari kuliko kununua Generator, Kinachofurahisha sasa wanachukua mkopo Cash kwenye taasisi wanaenda kufanya mambo yao binafsi na magari wananunua Vi-paso wakati mikopo wanachukua ya PRADO, huku wakiwa hawajali kabisa mamilioni ambayo taasisi inapoteza pale umeme unapokatika na usumbufu wanaotoa kwa wateja wao, Just Imagine
😎
Kwa Sasa sijui posho zao sijui, Mimi mpaka natoka nadhani ilikuwa ni 50k kwa mtumishi ya nauli kwa mwezi pekee kama sijakosea, hapa cutejancs atatusaidia kujua.
CEO wa Sasa watu walitegemea ataleta mapinduzi , nasikia mambo yamekuwa tofauti jamaa zangu walioko huko wananiambia ni bora hata angeongezewa mda kibona au Lilian, huyu ameshakuwa sehemu ya DBSS anachokifanya Sasa ni kutumia pesa nyingi za taasisi kuhamishahamisha watumishi kama alivyosema
CuteJancs kisa majungu tu au kumkomoa mtumishi, yaani akisikia umepambana umenunua gari au umeanza kunenepa anaona umefaidi anakuhamisha mjini na huko unakoenda akisikia umejenga anakuhamisha
😀😀😀,... haya mambo ni kama wanarithishana waliokuwa zamani wanajua watumishi wa GPSA tulikuwa tukinunua magari tunayapaki ofisi za MISITU kuogopa majungu na kuhamishwa, GPSA ya Sasa nasikia asilimia kubwa uhamisho ni kukomoana na sio kwa ajili ya maboresho ya taasisi... Hebu angalia hii scenario CEO uatumia pesa za taasisi kipuuzi nanmna hii, na Kwa mawazo haya unategemea taasisi ya GPSA ipate ustawi
😳😗