Majungu hayo. Kama una ushaidi toa taarifa kwenye vyombo husika.
Niko barabarani lakini baada ya kuona hii comment yako imebidi nipaki gari pembeni nikujibu japo kidogo kwa sababu tangu juzi nilipotoa comment yangu ya namna gani viongozi wa GPSA hawana Weledi zaidi ya kuwepo kimaslahi sikutokea tena hapa kwa sababu za kimajukumu.
Kinachoongolewa hapa Wala sio majungu ni uhalisia uliopo kwa viongozi wa GPSA, Kama ulikuwa hujui sio wote walioko GPSA ni wafanyakazi wa kawaida wengine wanaona ambayo wewe huwezi kuyaona japokuwa sipo kwa Sasa GPSA kikazi lakini naweza kuwa na uelewa wa taasisi kuliko hata wewe nikugusie kidogo tu kuhusu madili yanayopigwa na DBSS na CEO wa sasa halafu baadae nikiwa nimetulia nitarudi kuongezea.
1) Kuna mwaka (nimeusahau kidogo, nikifika nyumbani nitaungalia kwenye file zangu then nitaedit) DBSS alikuwa anaenda likizo, akajiandikia malipo ya likizo Kama 8m kama sikosei(nitaenda kuangalia upya pia) Kinyume kabisa na utaratibu wa malipo ya likizo file lilipofika pale utawala kipindi hicho ofisi ilikuwa na ma-HR (Ally, Mamboleo na Leah..sijui Kama Kuna mtu nimemsahau) na meneja utawala alikuwa anakaimu Leah Jericko (now yuko ofisi za stamico Kama sikosei, nitaangalia documents zangu vizuri baadae) huyu Leah alishtukia yale malipo hakusaini, zilipita Kama siku nne wakawa safari kikazi yeye na Ally na Ofice ya utawala akakaimu Mamboleo, DBSS akaona huu ndio mwanya wa kupitisha malipo yake akapitisha na Mamboleo hakuwa na nguvu za kuzuia, haya malipo yalishawahi kuhojiwa na wakaguzi ila Kama alivyosema
CuteJancs anatoa pesa na mambo yanaisha.
2Kwa taarifa za uhakika tena nilizopewa, Mwaka Jana alienda Likizo akajiandikia malipo ya 3m, yakafika kwa CEO japo CEO ni mtu wake akashtuka ikabidi aombe ushauri kwa mwanasheria, na mwisho haya malipo hayakuweza kufanyika( nitaenda kuangalia documents zangu nikifika nitaongezea kitu).
3) Kuna manunuzi ya Upigaji ya CCTV camera, hizi CCTV kwenye document za GPSA inaonesha CCTV zimenunuliwa na kuwekwa kwenye vituo vya mafuta vya kurasini-Dar na Dodoma( hapa dodoma kulikuwa na CCTV za zamanj ziliharika na kushindwa kufanya kazi), na zingine inasemekana zimewekwa baadhi ya sehemu za makao makuu,... Hebu nenda kaangalie thamani ya manunuzi ya hizi CCTV na habari mbaya zaidi dodoma hakuna CCTV mpya iliyopelekwa Kama inavyodaiwa kwenye document zao.
4) Ma-supplier wote wanaofanya kazi na GPSA za kusupply vifaa huwa wanatoa hongo kwa wakubwa, Hii huwafanya wapendelee watu wa kuwapa tenda huku wakijifanya kufuata utaratibu (Hapa Kuna ushahidi wa sauti za simu kati ya viongozi hawa na massupplier ambao nisingependa kuwataja majina kwa Sasa) baada ya kupewa tenda na kusambaza mzigo hawa viongozi (CEO, DBSS na DPAS) huwatuma watu ambao nisingependa kuwataja majina ili wakawachukulie pesa kwa hawa masupplier,..Hawa watu wanaotumwa wapo pale GPSA na Wala sio wafanyakazi wapo na hawana kazi maalum na wanajulikana na system kinachonishangaza ni kwa nini wanachelewa kuwachukulia hatua (Hapa upo ushahidi wa sauti za simu)
5) Kuna madili DBSS huwa anawatumia madereva zake japo wao wenyewe huwa hawajui kinachoendelea, wanapewa bahasha na wanaagizwa wa kumpelekea au wanaagizwa wafuate bahasha sehemu kipindi DBSS na hao wahusika wanakuwa wameshamalizana kwenye simu na kiasi wanachotakiwa wapeane ( ushahidi upo na hao watu wanajulikana mpaka majina na namba zao)
6) GPSA ilitumia pesa nyingi kimagumashi kununua mfumo wa mafuta(FMIS) ambao kwa Sasa hautumiki, unajua kwa nini haufanyi kazi mpaka Sasa japo ulinunuliwa kwa mda mrefu? Unafahamu ulinunuliwaje na kwa kiasi gani?Unajua ni nani anaeupinga usifanye kazi na kwa maslahi gani, wakati ndiye huyo aliyeutetea ununuliwe? Unajua walifaidikaje katika manunuzi ya huu mfumo? ukijua haya huwezi kusema huu ni umbeya.
Meneja wa ICT ( nimemsahau jina, nitaangalia kwenye document zangu nikifika then nitaedit) yuko pale Kama shati tu viongozi wanamzunguka wanapiga pesa kwenye manunuzi yote ya vifaa vya kielectronic, na kwa taarifa za uhakika Kuna mifumo mingi haifanyi kazi na Wala haijawahi kufanyiwa ukaguzi.
7) Kuna scandal niliambiwa na nikafatilia nikakuta ni ukweli ilikuwa inahusu ununuzi wa gari aina ya Scania ya kubebea watalii Mali ya maliasili na utalii ( Mwaka nimeusahau nitaenda kuangalia ila ni hivi karibuni) yenye gharama ya zaidi ya Tsh 500m+ pesa za kitanzania ambazo waliingiziwa na maliasili wawanunulie gari mpya, kilichotokea ikanunuliwa gari kukuu kutoka Scania ambayo baadae Maliasili waliikataa (hii kesi anaijua katibu mkuu wizara ya fedha na katibu mkuu wizara ya Maliasili na utalii), Watu waliokuwepo PMU ( nimewasahau majina nitaenda kuwaangali) walijitahidi kusolve hili na mwisho wa siku walifanikiwa na baada ya kufanikiwa kuficha hi scandal, viongozi walijilipa pesa kwa ajili ya kujipongeza kujinasua kwenye huu mtego( sijui Kama umeelewa hii scenario)
8) Unajua hawa viongozi wa GPSA walipanga kutumia billions of money kununua flowmeter Kinyume na utaratibu na isiyo na maslahi kwa taasisi zaidi ya maslahi yao binafsi?
9) Huyu DBSS alikuwa na kampuni yake ya forwarding and Clearing iliyokuwa inafanya kazi sawa na ambazo taasisi yake inafanya, hapa pia mhasibu wa ugomboaji(Allen) nae alikuwa na kampuni ya namna hii kilichokuwa kinafanyika walikuwa wana-divert kazi zilizokuwa zipitie GPSA zikawa zinapitia kwenye kampuni zao Kinyume kabisa na sheria za utumishi wa umma matokeo Kitengo Cha ugomboaji kikachoka sana kimekuja kufufuka baada ya maagizo ya rais magufuli.
Niishie hapa nitarudi...ngoja niendelee na safari