GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

GPSA: Tuhuma za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na mengineyo

GPSA. Mkurugenzi wa miaka ile enzi ya Mkapa alikuwa baba yangu Mkubwa. Bwana Lenard Mwavala. GPSA ya wakati ule ilikuwa na hadhi sana.

Maelezo Yako ni mazuri Sana Ila unapotoa claims next time kama hizi unatakiwa uainishe shida ipo wapi badala ya kuandika mfumo wa chuki na majungu. Serikali mara nyingi inafanyia kazi matatizo na Sio chuki.

Aidha, binafsi naunga mkono GPSA kutumbuliwa. Kwanza kwa Sasa hivi taasisi zote zinazofanya manunuzi zenyewe kama MSD, mizigo yake inatakiwa kuwa cleared na GPSA. Balaa linaanzia hapo; mzigo unaweza kukaa hapo bandarini mwezi mzima ukifuatilia malipo pale MSD unaambiwa MZIGO haujafika.

Wakati mzigo upo bandarini miezi 2.

Ukienda GPSA unaambiwa bado tunashughulikia, matokeo yake mizigo unatoka ukiwa unakaribia ku expire. Najiuliza taasisi za umma zinashida gani ?

Suala la kuhonga wakaguzi ni suala la taasisi za umma nyingi sana wanafanya hivyo. Lakini kiujumla GPSA inahitaji reform for sure.

Taasisi ambazo serikali izitolee macho na zenye ufisadi wa Hali ya juu uliojificha na wanaotumia pesa nyingi kuhonga wakaguzi ;
GPSA, MSD, TTCL, TANROADS, HESLB, Utumishi ( wale wanaopeleka watu Duce kwa interview), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa -Dar, you name them.

Serikali tunatoa hizi taarifa fanyieni kazi ni Taarifa muhimu sana inawezekana watu wa system nao waliokwenye taasisi hizo wana maslahi yao hivyo hawatoi taarifa sahihi.

Ndio maana Mpaka Kesho kuna wafanyakazi hewa kwenye taasisi hizo na upigaji.

ongezea TAMESA hapo! hawa jamaa ni tabu nyingine gharama ya services au matrngenezo ya magari hapo ni mara tatu zaidi ya bei ya mtaani. Sababu wao wenyewe hawana vifaa na mafundi so wanaisub contract kazi kwenda kwa garage za mtaani ambazo taasisi za serikali zinazuiwa kwenda moja kwa moja.
Naunakuta taasisi za serikali wanakarakana zao na hao TAMESA hawataki motokaa za taasisi hizo zitengenezwe na magereji mengini isippkuwa wao tu.
 
hivi gawio alitoa kwa mkuluuu?!
gpsa hata majengo yao hawapaki rangi kuonyesha uhai au ubunifu ofisi zimechooka sana na watumishi wamekata taamaa kwa mionekano yao.
wahusika wafanyie kazi hiki kwa kweli.
Duh..!!
Kumbe ishu hii ni serious?
 
hivi gawio alitoa kwa mkuluuu?!
gpsa hata majengo yao hawapaki rangi kuonyesha uhai au ubunifu ofisi zimechooka sana na watumishi wamekata taamaa kwa mionekano yao.
wahusika wafanyie kazi hiki kwa kweli.
Gawio lilitolewa kaka..
Kama mwanzo nilivoeleza, GPSA ni taasisi yenye vyanzo vingi vya mapato, mojawapo ni kumiliki visima vya mafuta Tanzania nzima na wateja wake sio wa kutafuta.

Huwezi kuwa na management yenye maslahi binafsi kwenye taasisi halafu utegemee taasisi ipate maendeleo. Hiki ndicho kilichopo GPSA,Kinachotokea ni kuwagawa wafanyakazi ili viongozi wawe wanapelekewa umbeya unaohusu madhambi yao ...matokeo taasisi imegeuka kuwa ya kimbeya, unafiki, majungu na morali na Ari ya kazi kwa watumishi ndani ya taasisi haipo kabisa. Yaani mtumishi ukiwepo GPSA unajiona kama umelaaniwa vile

Angalia namna Kitengo cha rasimali watu kinavyofanya kazi..kazi yao imegeuka kutafta habari za umbeya badala ya utawala...Hiki Kitengo kingevunjwa chote waletwe watu wenye kujua majukumu ya utawala.

Viongozi wanatumia Pesa nyingi kufanya uhamisho ambao sio wa maboresho na hauna tija kwa taasisi ila kwa sababu tu wamepata majungu kuhusu mtumishi....Special Audit ikifanyika hapa kuona gharama za uhamisho taasisi inayotumia na sababu zake wanaweza wasiamini watakachokiona..mtu mmoja anaweza kuhamishwa sehemu mbili ndani ya miezi4 na huko kote akalipwa mamilioni ya pesa...Sasa angalia hali ya ofisi zao zina hali gani halafu linganisha na gharama wanazotumia kuhamishahamisha watu.

Tungepata management kama ya MSD, GPSA tungekuwa mbali...yule CEO na DBSS hawana uwezo wa kuivusha GPSA zaidi wataididimiza kwa uroho na Ufisadi wao
 
Niko barabarani lakini baada ya kuona hii comment yako imebidi nipaki gari pembeni nikujibu japo kidogo kwa sababu tangu juzi nilipotoa comment yangu ya namna gani viongozi wa GPSA hawana Weledi zaidi ya kuwepo kimaslahi sikutokea tena hapa kwa sababu za kimajukumu.

Kinachoongolewa hapa Wala sio majungu ni uhalisia uliopo kwa viongozi wa GPSA, Kama ulikuwa hujui sio wote walioko GPSA ni wafanyakazi wa kawaida wengine wanaona ambayo wewe huwezi kuyaona japokuwa sipo kwa Sasa GPSA kikazi lakini naweza kuwa na uelewa wa taasisi kuliko hata wewe nikugusie kidogo tu kuhusu madili yanayopigwa na DBSS na CEO wa sasa halafu baadae nikiwa nimetulia nitarudi kuongezea.

1) Kuna mwaka (nimeusahau kidogo, nikifika nyumbani nitaungalia kwenye file zangu then nitaedit) DBSS alikuwa anaenda likizo, akajiandikia malipo ya likizo Kama 8m kama sikosei(nitaenda kuangalia upya pia) Kinyume kabisa na utaratibu wa malipo ya likizo file lilipofika pale utawala kipindi hicho ofisi ilikuwa na ma-HR (Ally, Mamboleo na Leah..sijui Kama Kuna mtu nimemsahau) na meneja utawala alikuwa anakaimu Leah Jericko (now yuko ofisi za stamico Kama sikosei, nitaangalia documents zangu vizuri baadae) huyu Leah alishtukia yale malipo hakusaini, zilipita Kama siku nne wakawa safari kikazi yeye na Ally na Ofice ya utawala akakaimu Mamboleo, DBSS akaona huu ndio mwanya wa kupitisha malipo yake akapitisha na Mamboleo hakuwa na nguvu za kuzuia, haya malipo yalishawahi kuhojiwa na wakaguzi ila Kama alivyosema CuteJancs anatoa pesa na mambo yanaisha.

2Kwa taarifa za uhakika tena nilizopewa, Mwaka Jana alienda Likizo akajiandikia malipo ya 3m, yakafika kwa CEO japo CEO ni mtu wake akashtuka ikabidi aombe ushauri kwa mwanasheria, na mwisho haya malipo hayakuweza kufanyika( nitaenda kuangalia documents zangu nikifika nitaongezea kitu).

3) Kuna manunuzi ya Upigaji ya CCTV camera, hizi CCTV kwenye document za GPSA inaonesha CCTV zimenunuliwa na kuwekwa kwenye vituo vya mafuta vya kurasini-Dar na Dodoma( hapa dodoma kulikuwa na CCTV za zamanj ziliharika na kushindwa kufanya kazi), na zingine inasemekana zimewekwa baadhi ya sehemu za makao makuu,... Hebu nenda kaangalie thamani ya manunuzi ya hizi CCTV na habari mbaya zaidi dodoma hakuna CCTV mpya iliyopelekwa Kama inavyodaiwa kwenye document zao.

4) Ma-supplier wote wanaofanya kazi na GPSA za kusupply vifaa huwa wanatoa hongo kwa wakubwa, Hii huwafanya wapendelee watu wa kuwapa tenda huku wakijifanya kufuata utaratibu (Hapa Kuna ushahidi wa sauti za simu kati ya viongozi hawa na massupplier ambao nisingependa kuwataja majina kwa Sasa) baada ya kupewa tenda na kusambaza mzigo hawa viongozi (CEO, DBSS na DPAS) huwatuma watu ambao nisingependa kuwataja majina ili wakawachukulie pesa kwa hawa masupplier,..Hawa watu wanaotumwa wapo pale GPSA na Wala sio wafanyakazi wapo na hawana kazi maalum na wanajulikana na system kinachonishangaza ni kwa nini wanachelewa kuwachukulia hatua (Hapa upo ushahidi wa sauti za simu)

5) Kuna madili DBSS huwa anawatumia madereva zake japo wao wenyewe huwa hawajui kinachoendelea, wanapewa bahasha na wanaagizwa wa kumpelekea au wanaagizwa wafuate bahasha sehemu kipindi DBSS na hao wahusika wanakuwa wameshamalizana kwenye simu na kiasi wanachotakiwa wapeane ( ushahidi upo na hao watu wanajulikana mpaka majina na namba zao)

6) GPSA ilitumia pesa nyingi kimagumashi kununua mfumo wa mafuta(FMIS) ambao kwa Sasa hautumiki, unajua kwa nini haufanyi kazi mpaka Sasa japo ulinunuliwa kwa mda mrefu? Unafahamu ulinunuliwaje na kwa kiasi gani?Unajua ni nani anaeupinga usifanye kazi na kwa maslahi gani, wakati ndiye huyo aliyeutetea ununuliwe? Unajua walifaidikaje katika manunuzi ya huu mfumo? ukijua haya huwezi kusema huu ni umbeya.

Meneja wa ICT ( nimemsahau jina, nitaangalia kwenye document zangu nikifika then nitaedit) yuko pale Kama shati tu viongozi wanamzunguka wanapiga pesa kwenye manunuzi yote ya vifaa vya kielectronic, na kwa taarifa za uhakika Kuna mifumo mingi haifanyi kazi na Wala haijawahi kufanyiwa ukaguzi.

7) Kuna scandal niliambiwa na nikafatilia nikakuta ni ukweli ilikuwa inahusu ununuzi wa gari aina ya Scania ya kubebea watalii Mali ya maliasili na utalii ( Mwaka nimeusahau nitaenda kuangalia ila ni hivi karibuni) yenye gharama ya zaidi ya Tsh 500m+ pesa za kitanzania ambazo waliingiziwa na maliasili wawanunulie gari mpya, kilichotokea ikanunuliwa gari kukuu kutoka Scania ambayo baadae Maliasili waliikataa (hii kesi anaijua katibu mkuu wizara ya fedha na katibu mkuu wizara ya Maliasili na utalii), Watu waliokuwepo PMU ( nimewasahau majina nitaenda kuwaangali) walijitahidi kusolve hili na mwisho wa siku walifanikiwa na baada ya kufanikiwa kuficha hi scandal, viongozi walijilipa pesa kwa ajili ya kujipongeza kujinasua kwenye huu mtego( sijui Kama umeelewa hii scenario)

8) Unajua hawa viongozi wa GPSA walipanga kutumia billions of money kununua flowmeter Kinyume na utaratibu na isiyo na maslahi kwa taasisi zaidi ya maslahi yao binafsi?

9) Huyu DBSS alikuwa na kampuni yake ya forwarding and Clearing iliyokuwa inafanya kazi sawa na ambazo taasisi yake inafanya, hapa pia mhasibu wa ugomboaji(Allen) nae alikuwa na kampuni ya namna hii kilichokuwa kinafanyika walikuwa wana-divert kazi zilizokuwa zipitie GPSA zikawa zinapitia kwenye kampuni zao Kinyume kabisa na sheria za utumishi wa umma matokeo Kitengo Cha ugomboaji kikachoka sana kimekuja kufufuka baada ya maagizo ya rais magufuli.

Niishie hapa nitarudi...ngoja niendelee na safari
Aisee! Hii ni hatari kubwa sana wanayoifanya. Bado nakuna kichwa ujasiri huo wanautolea wapi!?
 
Government Procurement Service Agency (GPSA) tatizo ni management kama yule DBSS hafai kabisa kuwa ofisini ni fisadi halafu mbinafsi na mbaya Zaidi anawahonga wakaguzi wanapokuja kumkagua na mambo yanaisha, na ili kulinda ugali wake anawala (anawagegeda) wafanyakazi wa kike walio wepesi kutongozeka ili wawe wanampelekea umbeya ambapo wengi wao anazawadia kwa kuwapa kipaumbele cha visafari na semina pale inapotokea yaani kama una mke wako anafanya GPSA humu jamaa hajali yeye anachovya tu,..na wa kiume nao anaselect wa kuwa wanampelekea umbeya kuhusu wafanyakazi wengine..

Ukiwa hujipendekezi GPSA maisha yako yanakuwa magumu, na CEO naye amemezwa na DBSS na mpenda sifa na maJungu Zaidi ya ufanisi wa kazi anatumia pesa nyingi kuhamisha watumishi kwa sababu ya umbeya tu anaopelekewa, kiufupi hana weledi wa kuongoza taasisi, na hawezi kuifikisha mbali na mara mia angepewa Liliani aliyekuwa ana - kaimu.

GPSA inatakiwa iwe juu ya MSD kimapato na kimaslahi kwa watumishi wake,tuna vyanzo vingi vya mapato lakini viongozi wanawaza ufisadi tu, sasa eti wafanyakazi wa mikoani tunalipwa posho kidogo kulinganisha na makao makuu kisa tuko mikoani tunatakiwa kulipwa tofauti na wa makao makuu, sasa kama hatuna umuhimu kisa tuko mikoani si bora tuhamishiwe wote makao makuu na mikoani kusiwe na wafanyakazi kama hawaoni umuhimu wetu na posho sio ya uhakika mpaka viongozi waanze kupiga majungu na kuchagua watu wa kuwapa…

KINACHOTOKEA SASA watu majembe wote wanaondoka, asilimia 90 ya wafanyakazi wa GPSA hawana moyo wa kufanya kazi kwenye ofisi hiyo wapo wakisubiri wapate nafasi waondoke sehemu zingine
.
serikali ingetakiwa ipangue management ya GPSA YOTE, wengine wangetakiwa wawe magerezani kabisa kama DBSS..

Wanaidhinisha makato ya mshahara ya watumishi bila idhini yetu, eti mfuko wa faraja GPSA. Yaani unashangaa mshahara unatoka unakutana na makato usiyoyaelewa, sawa ni jambo jema.. why wasingekata hata kwenye nauli..mishahara yenyewe ni midogo na ndio tunategemea kuikopea, wanaongeza makato kitu ambacho kinatupunguzia kiwango cha mkopo bank wakati walikuwa na option ya kukata hiyo pesa ya mfuko kwenye posho zingine.

Hii tasisi watu hawaipendi kiasi kwamba ni vigumu kukuta watu wamevaa fulana ya GPSA maofisini, zaidi tukipewa huwa tunawapa wafanyakazi wetu wa ndani wavae au wpigie deki, ama tunawapa mama ntilie

Tatizo kubwa na huu ndio ukweli ni kwamba GPSA ilikuwa shamba la bibi huko zamani sasa hivi taasisi hii inafanya vizuri mno.

Tatizo watumishi wamekaa sehemu moja miaka na miaka kwa kuwa hakukuwa na uwezo kutoa stahiki za uhamisho, kwa sasa Wakala huu unavyopiga hatua kuongeza mapato inahamisha watumishi kwenda maeneo ya kukusanya mapato ya serikali ili kuchangia uchumi wetu, mbona wengine tumehamishwa na tumekubaliana kuwa ni kwa maslahi na hitaji la utumishi wa umma na hatulalamiki?

Wapo tuliohamishwa kwenda kwenye mikoa na sio kijijini ni makao makuu ya mikoa ya Tanzania bara kuongeza nguvu au kuongoza utamaduni huu haujakuwepo tangu GPSA imeanza na wapo waliohamishwa na idara kuu ya utumishi yani Wizara ya utumishi kwa kuwa ni kwa maslahi mapana ya umma nikiwepo mimi, watu waliokulia hapo hapo na ikaonekana tuhamishww kuleta maboresho kwa Wakala uliofikia hatua ya kufutwa kabisa kwa kuwa ulikuwa haujawahi kufikia lengo la kuanzishwa kwake, tumehama tulipewa stahiki zote kwa mujibu wa kanuni za utumishi!

Kwa mara ya kwanza bila kushurutishwa GPSA imetoa gawio serikalini ile awamu ya kwanza kabisa . Ni maendeleo makubwa mno na brand yake imekuwa kuliko miaka yote ya huo uongozi unaoonekana ulikuwa na afadhali! Na kama ni suala la watumishi posho, haijawahi kutokea hata siku moja miaka yote huko nyuma kuwa na posho hizo? Sasa hivi waliopo pale wanapewa! Sasa kwa nini tusione sasa hii ni mwanzo mzuri kwa uongozi uliopo? Mimi ambaye nimehamishwa ninaona maendeleo na haya hapa ni majungu ya baadhi yetu tuliohamishwa kwa maslahi mapana ya umma.

Pia uongozi wa serikali umeendelea kuboresha taasisi zake na baada ya muundo mpya wa GPSA wapo ambao ni viongozi nafasi zao hazikuwepo kwenye muundo huo mpya kwa sasa ndio wanataka kuongoza majungu haya. Ikumbukwe GPSA ina maslahi makubwa ya nchi.

Hiyo clearing inayotajwa tajwa inafanywa kwa kiwango kikubwa na hapa wengi wanaotaka kuhujumu serikali wana hasira kwa kuwa walikuwa na makampuni au wako nyuma ya makapuni ya watu binafsi tangu tukiwepo hapo. Sasa wanaumia kwa sababu biashara hiyo sasa inasimamiwa na GPSA yenyewe ujanja ujanja hakuna.

Ninashauri pia tuangalie zamani GPSA ilikuwa inatoa kiasi gani serikalini na sasa wanatoa nini? Na ni kwanini serikali ilifikia hatua ya kuifuta Wakala huo na kwanini leo hii serikali imewapa dhamana ya kugomboa mizigo yote ya serikali! Sio kwamba wameaminika?

Mimi niliekuwepo hapo GPSA ninaona kabisa baadhi yetu tumeanza kuhujumu umma na juhudi za serikali katika kuongeza mapato yake huu ndio ukweli. Tuache maslahi binafsi na taamaa zetu na badala yake tujikite kujenga nchi! Na tukumbuke kuwa sio lazima wote kuwa viongozi na tukiendelea hivi huku tulipo tutaonekana hatufai.
 
Mzee jakatugu wewe inawezekana kabisa ni mmojawapo mnaofisadi hii taasisi unajificha kwenye hoja dhaifu unazozitoa kwa mdada CuteJancs hebu pitia maandiko yangu humu halafu unisaidie kutoa majibu yanayoeleweka kabla hatujaendelea kufunua mafile mengine ukiangalia maandiko yangu nimeanza kuelezea Ufisadi tangu enzi za mwambega acha blah blah na uwe umejipanga kwelikweli hapa Mimi nataja majina kwenye reference usidhani naweka code.

Nakusubiri
 
Mzee jakatugu wewe inawezekana kabisa ni mmojawapo mnaofisadi hii taasisi unajificha kwenye hoja dhaifu unazozitoa kwa mdada CuteJancs hebu pitia maandiko yangu humu halafu unisaidie kutoa majibu yanayoeleweka kabla hatujaendelea kufunua mafile mengine

Mkuu mimi niko hapa tangu 2017 wee upo tangu tarehe 2/4 siwezi kukimbia . Tukubali kwamba hii ni network yenu ya clearing iliyofutwa nyie ndio mliibia sana serikali na hamtaki kukubali kwamba nyakati zimebadilika serikali ina macho na inaona ukweli. Kubalini kwamba serikali imeamua kusimamia taasisi yake na si janja janja


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Vipi kuhusu hoja za FRAME-19
Ndio maana namsubiri aje kabla sijapost andiko lingine hapa..

Aje akiwa amejiandaa hapa hamna umbeya Mimi nataja majina kabisa na nini wamefanya siweki code ili ajue tunafahamu.

Na ukipitia maandiko yangu nimezungumzia ufisadi tangu enzi za mwambega na kinachofanyika Sasa huyu mzee aache blah blah kama ametumwa huku akiwa na hoja dhaifu.

Nipo hapa namsubiri
 
Mkuu mimi niko hapa tangu 2017 wee upo tangu tarehe 2/4 siwezi kukimbia . Tukubali kwamba hii ni network yenu ya clearing iliyofutwa nyie ndio mliibia sana serikali na hamtaki kukubali kwamba nyakati zimebadilika serikali ina macho na inaona ukweli. Kubalini kwamba serikali imeamua kusimamia taasisi yake na si janja janja


Sent from my iPhone using JamiiForums
Acha blah blah jibu hoja zangu kwa evidence sio swala la kuwepo JamiiForums...sema ni kampuni gani niliyokuwa nayo na inamilikiwa na nani?
 
Vipi kuhusu hoja za FRAME-19

Huwezi ukamjibu Frame- kwakuwa wote mna maslahi wote mlikuwa mnamiliki na mnatumiwa na wafanya bishara zamani kuhujumu serikali acheni tamaa msijifiche kwa uhuni wa kuharibu taasisi .


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huwezi ukamjibu Frame- kwakuwa wote mna maslahi wote mlikuwa mnamiliki na mnatumiwa na wafanya bishara zamani kuhujumu serikali acheni tamaa msijifiche kwa uhuni wa kuharibu taasisi .


Sent from my iPhone using JamiiForums
Wataje majina hao watu...huo ndio uzalendo tunaoutaka hatutaki umbeya...wewe taja utakuwa umeisaidia serikali kuwafahamu ili hatua zichukuliwe
 
Wataje majina hao watu...huo ndio uzalendo tunaoutaka hatutaki umbeya...wewe taja utakuwa umeisaidia serikali kuwafahamu ili hatua zichukuliwe

Wanajulikana mwingine hata jina lake linasadifu na nimemtaja hapo juu. Yeye na wenzake wanawake hao wawili. Wamebaki kudistabilize taasisi hata baada ya kuhama na mwingine kubaki hapo. Tujifunze kuwa watumishi na si wambea


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mzee jakatugu nijibu hili, unajua kwa nini CEO alimuondoa Aliyekuwa Mhasibu ( nadhani anaitwa amani) kama mwenyekiti kwenye kamati ya mapokezi ya Vifaa pamoja na kwamba alipendekezwa na PMU lakini jina lilipofika kwa CEO likakatwa na wote aliokuwa nao kwenye kamati iliyopita wakabakishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Afisa utawala (Ally) na mda mfupi akahamishiwa mkoani?
 
Wanajulikana mwingine hata jina lake linasadifu na nimemtaja hapo juu. Yeye na wenzake wanawake hao wawili. Wamebaki kudistabilize taasisi hata baada ya kuhama na mwingine kubaki hapo. Tujifunze kuwa watumishi na si wambea


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu itabidi nikupuuze naona kama unaleta umbeya kwa mambo yaliyo serious nimeshakuruhusu utaje majina kuvisaidia vyombo vya kiusalama kufanya kazi yao, humu ndani TAKUKURU, TISS na vyombo vya serikali vinasoma huu uzi wataje acha porojo za umbeya na hoja za kitoto

Ngoja nivute file lingine niweke hapa
 
Mzee jakatugu nijibu hili, unajua kwa nini CEO alimuondoa Aliyekuwa Mhasibu ( nadhani anaitwa amani) kama mwenyekiti kwenye kamati ya mapokezi ya Vifaa pamoja na kwamba alipendekezwa na PMU lakini jina lilipofika kwa CEO likakatwa na wote aliokuwa nao kwenye kamati iliyopita wakabakishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Afisa utawala (Ally) na mda mfupi akahamishiwa mkoani?

Kwa bahati mbaya sana nimegundua haujui maana ya mhasibu, mhasibu ni Mtu mwenye CPA, nakumbuka wakati ninatoka amani alikuwa ni karani wa mahesabu. Lakini pia kiutendaji kazi ya CEO ni kupokea mapendekezo kijiridhisha na kisha kuamua,kama aliamua kumuweka au kutomuweka ni maamuzi yake kiutendaji


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa bahati mbaya sana nimegundua haujui maana ya mhasibu, mhasibu ni Mtu mwenye CPA, nakumbuka wakati ninatoka amani alikuwa ni karani wa mahesabu. Lakini pia kiutendaji kazi ya CEO ni kupokea mapendekezo kijiridhisha na kisha kuamua,kama aliamua kumuweka au kutomuweka ni maamuzi yake kiutendaji


Sent from my iPhone using JamiiForums
Nilichogundua wewe utakuwa ni mfisadi unaweweseka...Nalog off ingia hapa saa2:30 usiku utakuta bandiko lililojaa ushahidi na watu watatajwa majina humo na Ufisadi waliofanya nikishindwa leo naliweka kesho mapema sana..

Hapa tunaisaidia serikali kupata taarifa za Ufisadi hatutoi umbeya
 
Back
Top Bottom