GR Hotel Mbeya inaongozwa na mtu aisye mtanzania kwa miaka 3 sasa. Je, hakuna mtanzania mwenye sifa ya kuwa Meneja hapo?

GR Hotel Mbeya inaongozwa na mtu aisye mtanzania kwa miaka 3 sasa. Je, hakuna mtanzania mwenye sifa ya kuwa Meneja hapo?

Shida ni kuongozwa na mgeni au mgeni kutokuwa na kibali cha kufanya kazi? Una chuki na meneja?
 
HOTEL SUPERMARKETS VIWANDA meneja mhindi na mtunza pesa.Hapo utafanikiwa.Lakini mbongo kwanza Wizi,atawala wafanyakazi mabinti wote,Majungu.
Hata Mengi na uzalendo wake Bonite Meneja mhindi.Azam
IPP yote ukicheki board of directors ni wahindi tupu,bila shaka Mengi anajua kwanini alifanya hivyo.

dodge
 
Tuko vizuri wapi mkuu? Tungekuwa vizuri tungepewa hizo kazi. Kwani kuna mtu anapenda kuajiri wageni kama wenyeji wanafanya kazi vizuri?

Sikatai. Lakini si kweli kuwa ni lazima tuendeshwe na foreigners ndiyo tuende mbele. Huo utakuwa wehu wa kiakili. Tumo huku Tz wazuri sana. Nyanja zote.
Nawapinga wanaojikataa. Eti kuwa hatuwezi. Upuuzi 360 degeees
 
Hahaa sijakuelewa hapa mtoa mada, Ktk mfumo wa uchumi wa kisasa hauangalii vigezo vya uraia hasa hasa kuendesha biashara inayohitajika kutengeneza faida ktk sekta binafsi. Ww unaweza kumpa mtu akuendeshee biashara yako ambaye hajawahi kuendesha biashara husika kwa mafanikio kisa ni m-Tanzania? Hata Dar es Salaam na Arusha hoteli karibu zote zenye hadhi ya nyota 5, General Managers sio wazawa. Binafsi naona hoja yako haina mashiko best talent ndo hupewa nafasi regardless of your nationality.

Kigezo kikubwa ni uwezo zaidi na uzoefu ndivyo vinavyoangaliwa sana. Pia ktk biashara ya kuendesha hoteli yenye hadhi kuanzia nyota 3 kinachoangaliwa kingine ni uwezo wako wa kumudu lugha kuanzia mbili za kimataifa kuzungumza na kuandika kwa ufasaha. Kitu ambacho wa-Tanzania wengi hatupo vizuri kwa mujibu wa tafiti za Twaweza.
 
Soma tena ulichoandika hizo Paragraph za mwisho..
Manager wa pale ni mkenya,ni rafiki yangu na alikuwa boss wangu pale landmark tukuyu, (hotel manager,) anaitwa "S" Amefanya kazi sehemu nyingi hapa Tanzania ikiwepo Regency kule mikocheni, akafanya corridor spring hotel arusha,(Kama sales and marketing manager) hotel zilikuwa zinajaa Sana sijui anapataje wageni ila alikuwa na mzungu mmoja kwenye hizo hotel akiwa sales Yule mzee ni marehemu.

Alifanya kazi briefly grand villa, baadaye kuna trainee alikuja field pale land mark bonge akawa anamla. Alipomaliza field akaondoka.

Either mjombaake au ami yake akawa anataka kufungua lle hotel, fatma huyo bonge akamwaambia amlete that guy.

Yule manager amefungua ile hotel na kuifikisha pale ilupo. So many offers zimekuja hata Mimi Mara kadhaa nimempa michongo amekataa. He deserves that position, najua unakitu kingine just tell us what it is tukusaidie. He is a short black guy anavaa miwani.

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Sababu ni Watanzania wenyewe hatupo serious tukiajiriwa wakati mwenye hotel ana mkopo bank, wavivu na wapigaji
This Hotel for three years or so, is under the management of a foreigner, though is locally owned by a Tanzanian.

Ni kweli hakuna Mtanzania anaweza kuwa manager hapa? Tunalalamikia kazi hakuna, ni kweli hatuna mtanzania anaweza endesha hotel hii ya kiwango cha chini hivi?

Authorities kazi kwenu. Uhamiaji. Kuna tatizo hapa mkoani Mbeya maagizo ya Mh Rais hayafuatwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sie wabongo tuko nyuma saana kwenye customer care, hasa hasa management ya customer care ndo maana sishangai hili.
ni ngumu saana kumpata good manager na ukimpata wabongo wenzake watamtilia majungu mpaka aonekane hafai. ila hao wabongo wakifanya kazi chini ya mgeni wanapiga kazi balaa na wanapelekeshwa kama punda ila kwao ni afadhali wapelekeshwe na mgeni kuliko kuwa chini ya mbongo mwenzao
 
Kabisa. Hii ni hazina ya social capital tuliyonayo. Kila mtu ni ndugu na ndivyo tumezaliwa na kukua tukijua hayo. Inaathiri sana utendaji hapa nchini. Kwa mfano ukiwa very strict utaitwa kila jina. Wakati wenzetu hilo tu linaweza kukupa promotion

Ila kasi ya maisha ya sasa imetubadili. Ukimbwela mbwela tu unapigwa out. Wengi tumebadilika. Ni lazima tujiaminishe kuwa tumebadilika badala ya kuwa waoga na kutojiamini.

Ni aibu sana kusema mtandaoni hapa kuwa Wakenya wana uwezo kuliko sisi. Fedheha sana. Ni kujikana na inadhihirisha dhahiri kuwa wengi wetu hatujulijui. Tupo tupo tu
 
Wakenya uwezo wao ni mdogo saana, ila wako strict na ndicho kinachowawezesha kwenye menegement. otherwise ni weupe tu
 
GR is among the best hotel in Mbeya, wacheni wageni tupate huduma bora. Mtu unalala chumba cha tzs 35,000 unamkia supu ya kuku, viazi mchemsho, chai, mayai, nk???

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa malazi pako sawa sana na very affordable,mimi pale ni kijiwe changu kikuu kila nikiwa Mbeya.
Panafaa sana kwa kazi zingine za kihuni.panakua a bit of class with very affordable prices. Plus......Sam ni mtu poa sana.sijui tu wafanyakazi wake wanamsemaje
 
Wakenya uwezo wao ni mdogo saana, ila wako strict na ndicho kinachowawezesha kwenye menegement. otherwise ni weupe tu
Yes. Hivyo ndivyo hasa walivyo. Kama huyu jamaa wanamsifia GR. Ukimsikiliza maongezi yake ufahamu ni wa mtu wa kawaida wa mtaani. Ambapo kuna watu pia utawakuta hapa wana ufahamu mkubwa sana.

Shida ni woga na kutojiamini
 
Acha apewa huduma zilikuwa mbovu sana. Tunabahtisha sana wabongo.

Imagine ungekuwa wewe ndiye mmiliki. Kama analipa kodi, huduma zipo vzr,wewe nenda kalale zile za mameneja wabongo.

Kuna kundi la wahasibu, usiombe hawa wabongo asee wakuandalie hesabu,ipo siku TRA watakudai kodi kama ile ya ACCACIA. Wao wanatazama fedha tu,ila ubora wa kazi hakuna ni ujanja ujanja wanamalizana na TRA vitu vikisanuka kama hawajui.

Watu wameamua kuwaajiri wahindi tu. Mambo yanaenda safi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna jamaa kaonekana anaingiza 160M kwa mwezi toka juzi anasema hataki hata mke wake amsemeshe!..
bongo elimu za makaratasi tu!.
😂😂
 
Back
Top Bottom