Mtia nia nafasi ya ubunge kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Grace Kiwelu, amerejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Vunjo, huku Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema akitaka uchaguzi uwe huru na wa haki
Lema ameyasema hayo leo Agosti 14, 2025 wakati wa shughuli ya urejeshaji wa fomu iliyoenda sambamba na uzinduzi wa ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pamoja na mambo mengine, ameonya vitendo vya rushwa katika uchaguzi na kusema chama hicho kipo tayari kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Aidha, amesema chama hicho kinaendelea kupokea fomu za ubunge na udiwani mpaka Agosti 26, 2025 na tayari watiania wa ubunge katika majimbo sita ya mkoa huo wameshachukua fomu
Naye, mtiania wa ubunge Jimbo la Same Magharibi, Gervas Mgonja ambaye alichukua fomu jana, aliwashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumuunga mkono kuhakikisha anagombea katika Jimbo hilo
Chanzo: Mwananchi_official