Elections 2010 Graduate, Mtoto wa Fukara, Shabiki wa CCM

Elections 2010 Graduate, Mtoto wa Fukara, Shabiki wa CCM

huo muungano wangetuamia walifanyia wapi mkutano na ulihudhuriwa na na nani na walifikiaje hilo azimio la kuwambia waombe radhi kwa kutumia kipemhele kipi cha katiba tungejua wasomi wetu lakini sasa wamejidhalilisha sana wanaonekana wameingizwa kwenye propanganda zilipokuwepo kwenye nchi za ulaya mashariki na urusi nyakati za kikomunisti ,halafu wengi wanajua ni propaganda tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu wasomi wameishiwa hata kabla hawajahitimu halafu tungeambiwa tamko la mwenyekiti au katibi wa huo muungano hapo wanafunzi wachache wamechakachuliwa ovyo kabisa wanafunzi wa aina hii kwenye nchi yetu hatutafika
 
Ulichoandika si kweli. Labda tu useme hukubaliani na hoja zilizotolewa. Hivi, mfano ukitaka kumkosoa kocha wa timu kwa kupanga kikosi kibaya utalazimika kusema wewe umesaidia vipi? Hapa imetolewa hoja, kama una majibu toa kama huna subiri wenzako wakusaidie. Hatuwezi kukaa kimya mambo yanaenda vibaya kwa sababu kuna watu watataka tuseme kwanza tumefanya nini! Hata hivyo kitendo cha ku-take time na kuweka thread kama hizi ambazo zinatoa nafasi kwa mjadala kwa vigezo vya hoja ni mchango mkubwa sana. Unaweza ukadhani "una busara" kuiga misemo ya "toa boriti kwanza kwenye jicho lako...." kumbe unanakili vitu vila kufahamu matumizi na muktadha. Anyway, mtu mmoja alisema "Commonsense is not common."
Not relevant
 
Big up Ngwanangwa yaani kama uikuwa kwenye mawazo, huo umati wa vijana wanaojiita wasomi kutoka chuo cha Kata Dodoma wamechoka inaonyesha ni watu from familia duni saana, badala ya kufikiria ukombozi wao wanashabikia siasa wasiozijua bila kujali hali ya kwao na wao hapo baadae, yangu macho and shame on them...
 
Yaani umesema kama vile kutoka moyoni kwangu. Hili jambo linaniudhi sana. Na mafisadi wanatumia vizuri sana hii weakness ya vijana. Sijui kwa nini hatujifunzi kwa vijana wenzetu kama Kenya!?
 
Mtoa maada katoa maelezo mazuri na yanayojitisheleza kabisa hivyo michango hasi kutoka kwa "wasomi"katika suala chanya kama hili inaonyesha jinsi gani usomi wetu usivyo na manufaa kwa jamii. Mleta maada anavyosema watoto wa mafisadi wakiwa "upanga"kwa akili za kawaida kabisa unatakiwa kujua anamaanisha wakiwa maeneo mazuri na si kuwa upanga wanakaa mafisadi tu.Hebu tuchukue muda kuielewa mada kabla ya kuchangia.
 
Wasomi!Wasomi!Ni maana ya usomi?Kuna msemo hapa bongo kuwa Mtu aliyesoma anaangalia maslahi lnk asiyesoma anapenda sifa.Lakn pamoja kuangalia maslahi,tuangalie hayo maslahi yawe kwa ajili ya nchi yetu na sio matumbo yetu.
 
Ninawasikitikia sana vijana wa Tanzania. Vijana wanaotokea familia masikini, mafukara ambao wazazi wao wanaishi kwenye nyumba za tembe na kulala kwenye vitanda vya ngozi za ng'ombe.

Vijana wamejaaliwa vipaji vya elimu. Wazazi wao (wanaoshabikia CCM kwa sababu wanafikiri Nyerere bado yupo hai) wamejikamua kuuza mifugo na mazao wapate elimu. Baadhi ya vijana hawa wamepata bahati ya kufika vyuo vikuu na kupata shahada na stashahada. Wapo mijini. Hawataki kurudi vijijini kwa sababu vijijini hakuna umeme. Vijijini hakuna zahanati na hospitali. Vijijini hakuna lami. Vijijini hakuna daladala wala taxi. Wala vijijini hakuna warembo kama huku mjini. Vijini kupata 'netweki' ya simu ni ishu. Vijijini kuchaji simu mpaka ulipie sh. 500 kwa mtu mwenye jenereta.

Mmmh! Vijana. Wasomi. Wanafanya mambo ya aibu. Wanakula takrima za CCM na kufanywa makamanda wa Green Guard. Wanafanya kazi ya kuratibu ugawaji wa fulana na kofia za CCM. Wanasafirishwa kwa malori na wengine kupoteza maisha kwenye ajali kwa ajili ya kuwatumikia mafisadi, wakati watoto wa mafisadi wako Upanga wanagombania rimoti za TV na kupunguza/kuongeza ubaridi wa viyoyozi.

Vijana masikini wa Tanzania wamesahau shida walizonazo wazazi wao. Wamesahau kuwa CCM na watawala wake wanaokula rushwa ndiyo chanzo cha matatizo yote ya nchi hii.

Tanzania inawalilia enyi vijana kutoka familia masikini za Tanzania. Jitengeni na CCM. Waacheni watoto na ndugu zao ndiyo wawe wapambe wao kwenye mikutano yao. Jiungeni na kundi la ukombozi.

Wakati ni huu. 2015 ni kesho tu.

Naomba tuchunguze wanaoenda UDOM wana IQ kiasi gani, then tujadili ubora wa elimu zinazotolewa(hapa tutagundua wasomi wetu wanataalumika badala ya kuelimika).
Pia nina shida na vyuo vyetu, they are too passive struggling to earn a degree through cheating or otherwise. Hapa tunahtaj elimu ya kukabili mazingira yanayotunguka. Huwezi amini haya yote yanatokea katika mazingira ya wasomi hao lakini wapo kimya au wengine wanatoa matamko ya kijuha... Wasomi walio vyuoni wana sehemu yao, wakicheza vyema tutafikisha nchi yetu pazuri.
Mniwie radhi kwa kuchanganya lugha
 
........ Graduate siyo mtu wa kumburuza na kumpeleka peleka. Labda awe mjinga mjinga
Yeah, right.
Unanikumbusha wale (sijui ndio wajinga wajinga unaowasema) waliokuwa wakibebwa na malori kama mifugo kwenye kampeni za CCM!
 
Back
Top Bottom