Graduate, Umekaa tu bure nyumbani na unataka ule milo mitatu?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
We kijana uliyesoma soma huko,

kuna sera mpya inakuja haiwezekani ule milo mitatu hivi hivi wakati huna kazi yoyote unayofanya hapo nyumbani

Halafu ukute anayekulisha amekubali kuteseka na kazi ya laki na nusu kwa mwezi...

amka upambane tukutane mezani Jioni tu

Milo mitatu ni kwa watoto wadogo
 
Utaambiwa ulimzaa wewe mwenyewe kwa kupenda starehe zako, hakukuandikia barua ya maombi kuwa anataka kuletwa duniani.

Soooo, beba mzigo wako 😎.
 
changamoto zingine tumetengeneza wazazi wenyewe kwenye jamii inawezekana bila kujua au kwa kujua tukiongozwa na kauli pendwa kuwa mimi nipate tabu na mwanangu apate tabu? siwezi kubali kwa kweli nakumbuka wakati tunasoma ni familia chache sana zilikuwa na maisha haya ya ajabu hata watoto wa Janguo aliyekuwa mkurugenzi wa bandari pamoja walikuwa navyo ila walikuwa na utu fulani si hizi aisee.
mambo yafuatayo yanaweza kuleta matokeo ya uvivu kwa vijana hawa:-
  • kuwachagulia watoto muundo wa maisha
    • aina za shule wanazosoma na kuwajengea wao kudharau wengine wanaosoma shule za kawaida.
    • kuwachagulia marafiki wa kucheza nao
    • kuwaona wao hakuna wanachoweza bali wasaidiwe kila kitu, ni kitu cha kawaida binti wa kazi kufua chupi za msichana aliye mwaka wa kwanza chuo kikuu.
    • maisha fulani ya fensi (gate ni zuri lakini tukumbuke halizuii vitu vibaya kuingia ndani tu bali huzuia na vitu vizuri visiingie ndani pia)
  • wazazi kuamini elimu ndio kitu pekee cha kumsaidia mtoto mzazi akilipa ada kamaliza hana muda wa kumwelekeza maisha mengine.
  • familia kutunzwa kwa fedha zisizo halali kiasi kwamba hawaoni uchungu au mzigo katika familia kwa mzigo uliopo.
  • malezi ya mzazi mmoja na hasa mama mapenzi yanahamia kwa mtoto (yaani mtoto anakuwa kama mwanasesele) mtoto linakwa jicho la mama na matokeo yake ni mtoto kumtawala mzazi na si mzazi kumtawala mtoto.
  • kuwajengea watoto kudharau mila na desturi na kudhamini destuli za wazungu. tumekubali watoto waishi maisha ya thamthilia na si maisha halisi.
yapo mengi lakini nishiriki kwa machache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…