Graduate wa chuo, tafuta documents zifuatazo omba passport ya kusafiria nenda Ulaya ukapate ramani ya maisha yako

Graduate wa chuo, tafuta documents zifuatazo omba passport ya kusafiria nenda Ulaya ukapate ramani ya maisha yako

Nimetumiwa barua ya kujiunga na chuo lkn sina passport .na passport nimenyimwa na Nina kila kitu yani cheti cha kuzaliwa,Nida. Inauma sana tena sana .na anaye nifanyia unyama huo yeye pia anatoka kigoma mmmh
 
Kupata documents Sio shida shida ni Hela angalau uwe na milioni 5 hivi ili ufike ulaya.
Sasa mtoto wa mkulima anapata wapi milion 5
 
Baada ya mzazi kushindwa kujieleza vizuri basi jamaa wa uhamiaji akaona ndo frusa ya kupata pesa akaniambia nimpe M1 kama sina niombe uraia .mm nikamwambia sina na nitaombajr uraia na wakati nimezaliwa hapa tz na documents zote nazo. BC jamaa ndo akachukua frusa hii kunikandamiza zaidi akapeleka paka kwa PCO documents zangu kwamba mm uraia haujakamilika.badae utasikia vijana hawachangamkii frusa wakati nchi ndo inakua ya kwanza kuwakatisha tamaa vijana.Leo unanifanyia hivi je kesho unajua mm nitakuwa nani? Ndo maana magu akawa na hasira sana sabab hapo mwanzo kuna watu walimfanyia unyama
 
Ni changamoto sana na unaweza kuwa na hivyo vyote na bado ukakosa .yani nchi hii hatari sana yani nimepewa ukimbizi wa kulazimishwa kisa mzazi hajajieleza vizuri.nimezaliwa hapa wazazi pia lkn nimekosa passport kisa wazazi kwao ni kigoma na tayari niliomba chuo China wamenikubaria na wameshanitumia barua lkn nimekosa passport nimeambiwa uraia wangu haujakamilika .ndugu zangu usiona kijana anatumia madawa ya kulevya,pombe sana au kuwa panya road au mhalifu au kuwa gaidi sikwamba anapenda ila ukweli nchi yetu inachangia sana vijana kuhalibika na kupoteza ndoto zao kwa mambo ya kibinafisi.inaniuma sana tena sana nchii hii imejaa rushwa ,ubinafisi .nimekosa passport kisa wazazi hawajui kujieleza vizuri na kila kitu ninacho
Umepata chuo gani China, na kipo mji gani.
 
Baada ya mzazi kushindwa kujieleza vizuri basi jamaa wa uhamiaji akaona ndo frusa ya kupata pesa akaniambia nimpe M1 kama sina niombe uraia .mm nikamwambia sina na nitaombajr uraia na wakati nimezaliwa hapa tz na documents zote nazo. BC jamaa ndo akachukua frusa hii kunikandamiza zaidi akapeleka paka kwa PCO documents zangu kwamba mm uraia haujakamilika.badae utasikia vijana hawachangamkii frusa wakati nchi ndo inakua ya kwanza kuwakatisha tamaa vijana.Leo unanifanyia hivi je kesho unajua mm nitakuwa nani? Ndo maana magu akawa na hasira sana sabab hapo mwanzo kuna watu walimfanyia unyama
Kwani huyo PCO ndio final nchi hii mnakwama wapi mbona zipo mamlaka nyingi tu za kuripoti Kama ujatendewa haki
 
Hakuna mtu asiyepajua Ulaya kwamba ndio mahali pekee pakupata exposure ya maisha na elimu. Sasa unataka vijana waelezwe nini. Graduate anaweza ingia Ulaya kufanya kazi au kusoma elimu ya juu.
Vihehere vya wapigania Uhuru ndio vimewaletea shida ya maisha magumu waafrika tusingedai uhuru tungekuwa Dunia ya pili
 
Baada ya mzazi kushindwa kujieleza vizuri basi jamaa wa uhamiaji akaona ndo frusa ya kupata pesa akaniambia nimpe M1 kama sina niombe uraia .mm nikamwambia sina na nitaombajr uraia na wakati nimezaliwa hapa tz na documents zote nazo. BC jamaa ndo akachukua frusa hii kunikandamiza zaidi akapeleka paka kwa PCO documents zangu kwamba mm uraia haujakamilika.badae utasikia vijana hawachangamkii frusa wakati nchi ndo inakua ya kwanza kuwakatisha tamaa vijana.Leo unanifanyia hivi je kesho unajua mm nitakuwa nani? Ndo maana magu akawa na hasira sana sabab hapo mwanzo kuna watu walimfanyia unyama
Kuzaliwa bongo Sio tiketi ya kuwa raia labda Kama babu na bibi zako wote wamezaliwa bongo.
Wengi hawajui kimbembe huja wakienda omba passport uelewa wakishachelewa wakati hitaji la safari lipo mlangoni
 
Mchanganuo wa Nyaraka za zinazohitajika kwa anayetafuta Pasipoti ya Kusafiria Kwa Safari ya Ulaya na Kuweka Mipango ya Maisha.

Kabla ya kuanza safari yako ya Ulaya na kuanza hatua mpya ya maisha yako, unahitaji kuwa na nyaraka sahihi zinazohitajika wakati wa kuomba pasipoti ya kusafiria. Hizi ni nyaraka ambazo unaweza kuhitajika kuwasilisha ili kuhakikisha kuwa maombi yako ya pasipoti yanapokelewa. Nyaraka hizi ni kama ifuatavyo:

  1. Barua ya Uthibitisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata/Mtaa kwa Mzazi/Mlezi Asiyeajiriwa: Barua hii inathibitisha uhusiano wako na mzazi/mlezi asiyeajiriwa na inaonyesha idhini yao kwa safari yako ya Ulaya. Inaweza kuhitajika kwa ajili ya kudhibitisha utambulisho wa familia yako.
  2. Barua ya Kujiunga na Shule/Chuo: Barua hii inaonyesha kuwa unakusudia kuendelea na elimu yako baada ya kuhitimu chuo. Inaonyesha nia yako ya kukuza elimu yako na inaweza kuwa na athari chanya katika maombi yako ya pasipoti.
  3. Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa cha Mzazi wa Mwombaji: Cheti au kiapo cha kuzaliwa cha mzazi wako kinaweza kutumika kudhibitisha uhusiano wa kifamilia na mzazi wako. Ni sehemu muhimu ya nyaraka za kuthibitisha utambulisho wako.
  4. Cheti/Kiapo cha Kuzaliwa cha Mwombaji: Cheti au kiapo chako cha kuzaliwa kinathibitisha tarehe yako ya kuzaliwa na utambulisho wako binafsi. Ni nyaraka muhimu katika mchakato wa kuomba pasipoti.
  5. Kadi ya Mpiga Kura ya Mzazi/Mlezi: Kadi ya mpiga kura ya mzazi/mlezi inaweza kutumika kuthibitisha utambulisho wao na pia kuonyesha msaada wao kwa safari yako ya Ulaya.
  6. Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Afisa Mtendaji wa Kata: Barua hii inaonyesha utambulisho wako kutoka kwa mamlaka ya serikali ya mtaa au afisa mtendaji wa kata. Inaweza kuwa na athari nzuri katika kuthibitisha utambulisho wako.
  7. Kitambulisho cha Taifa cha Mzazi/Mlezi: Kitambulisho cha taifa cha mzazi/mlezi kinathibitisha utambulisho wao kama raia. Ni nyaraka muhimu kwa kudhibitisha uhusiano wa kifamilia.
  8. Vyeti vya Elimu (Shule/Chuo): Vyeti vya elimu vinavyothibitisha mafanikio yako ya kitaaluma katika shule au chuo. Vinaweza kuonyesha juhudi zako za kujifunza na uwezo wako wa kufikia malengo.
  9. Fomu ya Maombi ya Pasipoti: Fomu hii inayojazwa kwa usahihi na taarifa zote muhimu kuhusu maombi yako. Inapaswa kuwa kamili na sahihi ili kuhakikisha kuwa mchakato wako wa kuomba pasipoti unakwenda vizuri.
Ukiwa na nyaraka hizo, unaweza kuwa na uhakika kwamba maombi yako ya pasipoti ya kusafiria yatafanikiwa.

Hata usipo ingia Ulaya unaweza kuingia CHINA, US, SOUTH KOREA, INDIA kokote kapate exposure uje na ramani.

SAFARI NJEMA
Kupata pasport mbona easy tu. Shida kuingia huko south korea
 
Back
Top Bottom