Graduates mnaopata loans, funds etc Msituangushe

kijana13

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
1,981
Reaction score
3,631
Habarini wakuu, Nandika ujumbe huu kwa Vijana Graduates ambao walipata mafunzo ya kitaalamu ya namna ya kuendeshea biashara etc pia baadhi yao kupata either loans or grants kutoka mabenki, taasisi za serikali, mashirika ya kimataifa na taasisi zingine.

Nitoe Hongera kwa vijana walioweza kutumia fursa hizi vizuri na kufanikiwa kibiashara. Pia nasikitika kwa Vijana waliopata mitaji wakatumia kwa malengo ambayo hayakukusudiwa

Naandika ujumbe huu baada ya kufanya tathimini fupi/kidogo.
Mfano mwaka 2009 na 2012 kuna program ya shindano la mchanganuo wa biashara lilikuwa linaendeshwa na TPSF baadhi washindi pia walikuweno Vijana graduates waliofanikiwa kushinda na kupatiwa grants miongoni mwao kuna waliopata from 3 mill hadi 25. Wengi wao walishindwa kuanzisha biashara ingawa walikuwa na business plans nzuri.

Mfano wa pili ntakaoulezea ndio umenifanya kuandika hii thread.
Ni Vijana wa SUA waliopata fedha kupitia CRDB bank kwa ufadhili wa USAID, Tetesi ni kwamba baadhi ya Vijana waliopokea fedha kiasi cha mill 20 etc kwa ajili ya kuanzisha biashara baadhi yao walianzisha biashara na hadi sasa zimekufa kwa sababu zinazotokana na uzembe na kutokuwa serious, hali hii imepelekea benki kuwa discourage kwa kuendelea na progam hii.

Pia kuna program zingine ambazo nazifahamu ambazo graduates walipata funds hawakuanzisha biashara.

Wito wangu kwa vijana, ni kubadilika maana hali hii inapelekea graduates kutoaminika katika taasisi za kifedha na wahisani wengine.Pia mnaziba fursa kwa graduates wengine ambao wana nia ya kufanya biashara na wanabusiness plans nzuri.
 
kwangu mimi naweza kusema si vema kuwalaumu walioshinda kuwa wamewaangusha maana kwangu mimi ninavyoifahamu nchi yangu hii na jinsi mifumo ya kipuuzi tuliyoijenga.

hakuna mtanzania leo hii anaweza kushinda shindano kama hilo kwa kuwa na best business plan bali anayeshinda shindano la mtu kupewa milioni 20 tanzania ama awe na yafuatayo

1. awe na bosi katika mfumo wa kumsimamia
2. aahidi parcent fulani ya hiyo hela kwa baadhi ya watu walioko katika maandalizi ambao wanauwezo wa kumfanya ashinde.

hivyo ukiangalia tangu mwanzo mchakato unagubikwa na ujanja ambao ndio tanzania unaoweza kukupatia ishu kama hizo.

kama kuna mwenye kubisha hawa jamaa watuwekee proposal zote zilizopokelewa kwenye mtandao na ilishinda tena kwa vigezo vipi.

taasisi nyingi zinaendeshwa hivi tenda, kazi zinatangazwa kukamilisha matakwa ya sheria ya manunuzi lakini kupata hasa kwa taasisi za serikali ni kwa kujuana na rushwa tu. na hivi ndivyo vinasababisha miradi kutekelezwa kwa kiwango cha chini lakini wakandarasi wakilipwa ela yao yote na wasimamizi wao
 
Back
Top Bottom