Graduates wengi mkiweka aibu na uoga pembeni, basi mtaani mnaishi

Mitandao ya kikuda ni ipi mkuu ?
 
Waache waendelee kukaa kijiweni na home ili hata bando la kuingilia huku jf likikatika waendelee kuomba dada zao si hera tunawahonga hamna noma. [emoji16][emoji16][emoji848][emoji848]
 
Umeongea ukweli mtupu sana humu. Ni wazi vijana wengi tunaishi kwa matumaini na hii inatokana na jamii tulizolelewa nazo ambazo nyingi zinaamini ukisoma basi mafanikio yatakufuata nyuma, kitu ambacho kwa miaka ya karibuni kimekuwa hakitekelezeki. Ni wakati sasa vijana tusahau kuwa tuliwahi vaa majoho na kuudhuria mihadhara ambayo ilitupa matumaini makubwa juu ya maisha baada ya chuo.

Vijana tunakwama wapi ? Kwa nini tunakosa ubunifu na kila mmoja kutaka auze nguo, mikoba, mashuka na simu ? Je nani atamsupport mwenzake ?
 
Kwenye ubunifu ndiyo shida. Kuna mwanangu nilimpa idea tena inasolve tatizo. Akanijibu kwa nini tusifuge kuku?
Yaani tunapenda vinavyofanywa tu hatuwezi vipya
 
Kwenye ubunifu ndiyo shida. Kuna mwanangu nilimpa idea tena inasolve tatizo. Akanijibu kwa nini tusifuge kuku?
Yaani tunapenda vinavyofanywa tu hatuwezi vipya
Tatizo kubwa ni kwamba tunataka kufanya vitu vinavyoendana na hadhi fulani pasipo kuangalia maslahi. Ndio maana ni rahisi kuona graduates wenye vidgree waliojiajiri basi wakifabya biashara online, wakiuza simu, wakiuza mikoba, wakiuza nguo za kiume na sasa wakiingia kichwa kichwa kwenye kilimo wakati kuna biashara au ideas ndogo ndogo mtu akizifanyia kazi zinaweza kumpa faida kubwa na kuwa na mzunguko mkubwa wa hela ukilinganisha na hizo.
 
Hata hiyo ya kuuza vitu online ni Idea nzuri sana mkuu.
 
Niliwahi kuishi maeneo flani,tajiri mkubwa wa lile eneo alitajirika kwa kuanza na biashara ya kuuza vitumbua,alikuwa anatembeza mkono kwa mkono nyumba kwa nyumba,alipofanikiwa akaendeleza mambo mengine,maduka,hoteli n.k.Baada ya miaka kadhaa nilikuwa kwenye mkoa mwingine nikamshawishi mtu mmoja naye aanzie kwenye biashara hiyo kwani alikuwa hana mtaji wa biashara,mpaka leo haongei na mimi anasema nimemdharau sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…