Graduates wengi mkiweka aibu na uoga pembeni, basi mtaani mnaishi

Graduates wengi mkiweka aibu na uoga pembeni, basi mtaani mnaishi

Juzi imepita Nissan Primera moja iko mafuta sana. Ghafla nikaona imerudi mpaka nilipokua. Jamaa akashusha kioo.

Jamaa: Oya niaje?
Mimi: Freshi chief, karibuu (Hapo
nimemtambua, niliskulinae)
Jamaa: Sikuhizi ndo uko hapa?
Mimi: Ndio chief, shuka nikupigie maji ndinga
hiyo, buku tano tuu.
Jamaa: Mwanangu acha kutusanif bwanaa, we
jamaa ulikua na maakili ulikua
unatukimbiza kwenye namba.
Mimi: Akili zangu kwasasa zimeishia hapa.
Jamaa: We si nilisikia ulikua unasoma
madegree huko. We ulitakiwa uwe
mabenki hukoo, maana yale mahesabu
nomaa

Kufupisha story:
Jamaa amenikuta car wash naosha gari za watu akakataa kukubali akirefer ufalme wa shule kua sikutakiwa kua pale.

Hiyo ndo jamii inayomzunguka graduate. Tunahitaji kujikana ili uishinde.
Ahahaha
 
Nilikutana na kimbunga cha uchumi kuyumba 2016 mishe zote zikafa. Nikafungua mgahawa mwananyamala biashara ikagoma ,ikabidi nitengeneze toroli ili iwe mobile kitchen.

Nikawa napika chapati ,nilianzia posta pale kituo kinapakana na usalama wa taifa,tra na mamlaka ya bandari. Baishara ilikua nzuri kweli ila usalama wa taifa wakanitimua. Nikahamia na toroli langu kigamboni nako biashara inawa ngumu Sana,kimara,mbezi kote hola.

Nikaamua kubeba toroli langu mkoani mbeya,nimepambana soweto kama miezi 6 hola. Huku nasikia maneno tu huyu amechanganyikia make amesoma ulaya saizi ilitakiwa awe na kazi nzuri tu.

Baada ya mapambano ya muda mrefu gizani sasa jua limewaka. Waliokua wanasema mbovu wanajificha huku wengine wakijisogeza karibu ili waonje keki ya mafanikio. Maisha ya kutafuta hela inatakiwa kujikana nafsi tu ,usione aibu kwani njaa ni yako na familia yako. Unaemuonea aibu ndiye awe mteja wako wa kwanza.
Hongera
 
Aibu na Uoga ni janga kubwa sana. Asikuambie mtu, mtu asikuambia mimi sina mtaji ila ukweli ni Aibu na Uoga.

Kuna Mtumishi mmoja Baba yake na Mkurugenzi wa Jamiiforums aliwahi tuambia mafanikio huanza pale Uoga na Aibu zinapoondoka

Tuna hivi vitu moyoni.

1.Wazazi watanielewa kweli kijana wao mwenye Degree?

2.Hivi Shemeji yangu akisiki itakuwaje?

3.Hivi Mchumba wangu atanielewa kweli kwamba ni mimi niliyekuwa Chuo?

4.Marafiki zangu watanielewa kweli?

5. Majirani vipi?

Combination ya hivyo vyote humfanya mtu aone bora akae tu kisingizio kiwe sina mtaji

Unaondoaje AIBU na UOGA?

1. Jitoe ufahamu kabisa, weka pamba masikioni hapa na pale ambapo inafikia stage wanakuona kama unerukwa na akili ila wewe na Mungu wako ndio mnajua unacho kifanya.

Hii hatua ni ngumu sana kujitoa ufahamu sio mchezo manake inabidi kweli uwe na roho ya Chuma au Roho ngumu sana.

2. Hama nenda mbali na wanako kujua. Kama home ni Korogwe pale na wanakujua ulikuwa Chuo kikuu basi nenda Karatu Arusha anza makazi pale fanya chochote hata kuuza vocha na sigara na karanga.

Hii ni njia nzuri sana manake unakuwa mbali sana na unakuwa kivyako vyako au na mshikaji wako na mnafanya mambo.

3. Usijaribu kumshirikisha mtu yoyote yule hata Wazazi wako kwamba unataka kufanya nini au unafanya nini bali waje kujua wenyewe baadae sana.

Kitendo cha kuwaambia Wazazi au Ndugu na Jamaa na Marafiki kwamba kwa sasa nataka nifungue kibanda cha kuuza Vocha wengi hawatakuelewa na watakukatisha tamaa balaaa.

Hii inachangiwa na imani kwamba Chuo kikuu ni ni levo tofauti.

4. Jitenge na ma-met zako au Marafiki walio na kazi watakutia Uoga zaidi manake ukiwa unawaona wanatokea kazini utaumia zaidi.

5. Washikaji na ndugu na Jamaa wakiwa wanakupigia pigia simu wewe wajibu in short una kibarua unafanya sehemu. Ili kukata mazungumzo manake wakipiga ukaawambia unauza Vocha Dah, hawatakuelewa kabisa kabisa.

Jitahidi kuwakatisha na wajibu in short tu.

MWISHO
Achana na kwamba una Degree hata ikibidi watu wengi waambie hujaenda shule au uliishia tuu Form four.

Ondoa Aibu na Uoga wacha watu wakuone kama umechanganyikiwa, wacha wakuseme, wacha wakucheke, wacha wakukebehi ila mwisho wa siku unajua unacho kifanya.

Kwa sasa Naishia hapa.

MAFANIKIO HUANZA PALE TU AIBU NA UOGA VINAPO TOWEKA
Hahahaha Nakumbuka hata mm niliondoka home nikaja town wazaz wakawa wananiuliza unafanya kaz gan huko nawaambia nimejiliwa kweny campuny ya voda hahahaha kumbe nilikua nasajil lain tu kitaa nikienda home napiga mashat ya voda nimetoka mbal

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Watoto wa DAR kila siku wanashuhudia Wenzao Kutoka Mkoa wametoboa kimaisha kwa sababu jamaa wa mkoani wakija DAR hata guta au mkokoteni anaendesha ila wazazawa ni kushinda Home kucheki Series au kukaa Saloon na vijiweni

Vijana ma Magraduate Dar mnakwama wapi
We unafikiri ni rahisi hivyo?


We uko Dar na una degree huna ajira?if yes je meshafanya kazi ngapi za kujitoa ufahamu
 
Niliwahi kuishi maeneo flani,tajiri mkubwa wa lile eneo alitajirika kwa kuanza na biashara ya kuuza vitumbua,alikuwa anatembeza mkono kwa mkono nyumba kwa nyumba,alipofanikiwa akaendeleza mambo mengine,maduka,hoteli n.k.Baada ya miaka kadhaa nilikuwa kwenye mkoa mwingine nikamshawishi mtu mmoja naye aanzie kwenye biashara hiyo kwani alikuwa hana mtaji wa biashara,mpaka leo haongei na mimi anasema nimemdharau sana...
Wewe ni tajiri?na wangapi wanauza vitumbua tangu hatujazaliwa mpaka leo maisha magumu?
 
Wewe ni tajiri?na wangapi wanauza vitumbua tangu hatujazaliwa mpaka leo maisha magumu?
Kwani wote wenye maduka ya vifaa vya umeme ni matajiri,au wote wenye restaurants ni matajiri?kila mtu kwenye biashara ana ubunifu wake, huenda na yeye kwa kufanya hiyo biashara kwa kutumia ubunifu wake angeweza kutoka,sikumwambia afanye hiyo biashara ili awe tajiri ila nilimpa mfano wa mtu ninayemjua alietoka na kuwa tajiri kwa biashara ya vitumbua...
 
Mi ni mhanga wa kusimangwa na jamaa yangu mmoja tuliyesoma wote advance lakini vyuo tofauti ;siku moja alinikuta nafanya kazi ya umachinga mwanza alinicheka sana.Alinicheka si kwamba yeye alikuwa na ajira no,ila alikuwa na pa kula na kulala.
 
Mi ni mhanga wa kusimangwa na jamaa yangu mmoja tuliyesoma wote advance lakini vyuo tofauti ;siku moja alinikuta nafanya kazi ya umachinga mwanza alinicheka sana.Alinicheka si kwamba yeye alikuwa na ajira no,ila alikuwa na pa kula na kulala.

Haha
 
Watoto wa DAR kila siku wanashuhudia Wenzao Kutoka Mkoa wametoboa kimaisha kwa sababu jamaa wa mkoani wakija DAR hata guta au mkokoteni anaendesha ila wazazawa ni kushinda Home kucheki Series au kukaa Saloon na vijiweni

Vijana ma Magraduate Dar mnakwama wapi
Kuna mda nawalaaani sana watoto wa Dar kuna kipindi ata akipata mwenza wa kimaisha kama yuko nje ya Dar anamkataa, kitukikubwa wanabweteka na vitu vya watu. Tanzania ni kubwa sana na pengine fursa nyingi zimeshachukuliwa na wenye capital njooni mikoani mtafaidika. Niishie hapa akati wewe unafikiria kutoka Dar ni utumwa, kuna mchina analilia arudi bongo auze ata maandazi akiwa na amani ilhali wewe unalia lia tu, dunia kijiji tuamke tupambane.
 
Aisee hii ipo sana mitaani,
Mi ni mhanga wa kusimangwa na jamaa yangu mmoja tuliyesoma wote advance lakini vyuo tofauti ;siku moja alinikuta nafanya kazi ya umachinga mwanza alinicheka sana.Alinicheka si kwamba yeye alikuwa na ajira no,ila alikuwa na pa kula na kulala.
 
Back
Top Bottom