Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

Kuna comments/hoja huwa zinawatoka tu watu bila kufikiria (kama mtu anapopata mshtuko ghafla na kusema mamaaa..)

Kwa bongo teknolojia haijaatjiri ajira kama watu wanavyotaka tuamini

Tena ninaweza ku argue kwamba some how tech imeongeza ajira, angalia sekta ya usafirishaji, angalia sekta miundombinu, angalia sekta ya kilimo (tech imeleta large scale agr. more people involvement), tuangalie kwenye afya kabla ya tech kusambaa hakukuwa na hospitali binafsi au labs za vipimo (zote hizo ni ajira kwa watu), angalia sekta ya biashara (nipo mkoani napiga simu mtu anichukulie mzigo Kariakoo kisha anitumie, kisha nampa chake), zamani tulikuwa na ajira za ma bank teller huko bank, siku hizi mpaka mtu wa la saba ni Bank teller kupitia M-Pesa, Tigo Pesa n.k)mifano ipo mingi sana
Teknolojia imeathiri vipi ajira tanzania wakati matumizi yetu ya teknolojia ni madogo sana ?

Hebu taja kada moja tu ambayo hapa nchini imeathiriwa na kuwepo kwa teknolojia hadi kupelekea ukosefu wa ajira?

Tanzania yenye population milioni 59 huku wasomi wakiwa below Milioni wakiwa hawazid hata milioni 3 unakuwaje na mass unemployment kubwa hivyo kwa graduates ?

Tuweni wakweli tu tatizo la ajira nchini ni zao la uongozi mbovu na siyo teknolojia wala mama yake teknolojia.

Kutumia a Worldwide problem theory kuzungumzia tatizo la ajira nchini siyo sahihi ni kielelezo cha kukosa maarifa tu kwa watawala wetu.
 
nimekaa mikoani kwa miaka kumi sasa
hata huku shughuli ni ngumu si rahisi kama watu wanavyofikiria
lakini dar bado fursa zipo kibao kwa kuwa kuna watu wengi ambao wanamahitaji mengi hivyo ukijitoa ufahamu kidogo tu utauza.
 
Kuna comments/hoja huwa zinawatoka tu watu bila kufikiria (kama mtu anapopata mshtuko ghafla na kusema mamaaa..)

Kwa bongo teknolojia haijaatjiri ajira kama watu wanavyotaka tuamini

Tena ninaweza ku argue kwamba some how tech imeongeza ajira, angalia sekta ya usafirishaji, angalia sekta miundombinu, angalia sekta ya kilimo (tech imeleta large scale agr. more people involvement), tuangalie kwenye afya kabla ya tech kusambaa hakukuwa na hospitali binafsi au labs za vipimo (zote hizo ni ajira kwa watu), angalia sekta ya biashara (nipo mkoani napiga simu mtu anichukulie mzigo Kariakoo kisha anitumie, kisha nampa chake), zamani tulikuwa na ajira za ma bank teller huko bank, siku hizi mpaka mtu wa la saba ni Bank teller kupitia M-Pesa, Tigo Pesa n.k)mifano ipo mingi sana
Ni kweli mkuu tunajaribu kutumia scapegoat ambayo siyo sahihi kwenye tatizo la ajira.

Mimi hainingii akilini nchi yenye watu milioni 59 na wasomi wa vyuo vikuu ambao hawafiki hata 10% ya population nzima ikabiliwe na mass unemployment kiwango kikubwa namna hii kwa graduates.

Wanasiasa wakikosa majibu sahihi ya kwanini kuna mass unemployment tunakimbilia kusema kuwa ni tatizo la kidunia bila kuangalia mahitaji halisi na mazingira yetu kama hii hoja ina mashiko.

Kuhusu teknolojia sisi hatujafikia kwenye high tech ya kuweza kutusababishia unemployment, stage tuliyopo ni teknolojia kuzalisha ajira nyingi zaidi badala ya kupunguza ajira.

Hii world wide problem theory ni faulty kwa mazingira yetu sisi
 
Yap, kwa sisi tech inazalisha ajira zaidi

Kilichopo pia ni utoaji wa elimu ambayo ni irrelevant kulingana na mahitaji

Mfano unaweza kuta kwa mwaka nchi inazalisha Maafisa Utumishi 5000 na mahitaji kwa mwaka ni 200, kwa mwaka tunahitaji Walimu wa sanaa 2000 halafu tunazalisha Walimu wa sanaa 25,000, tunahitaji watu wa Marketing 400 lakini tunazalisha 5000 (Nasisitiza huu ni mfano tu)

Ili tuwe na mahitaji makubwa ya watu hao tunarudi kwenye Serikali kuweka sera zinazo influence private sectors kuzalisha hizo kazi, pia kuwe sera wizara ya Elimu & Elimu ya juu kuzalisha Wataalan flani kwa mujibu wa mahitaji lakini la mwisho ni kuweka mkazo mkubwa kwenye elimu ya ufundi, nchi kama Ghana walifanikiwa kwenye hili

Nchi nyingi za uchumi kama wetu hazipaswi kuzalisha degrees (decision makers) bali wajuzi
Ni kweli mkuu tunajaribu kutumia scapegoat ambayo siyo sahihi kwenye tatizo la ajira.

Mimi hainingii akilini nchi yenye watu milioni 59 na wasomi wa vyuo vikuu ambao hawafiki hata 10% ya population nzima ikabiliwe na mass unemployment kiwango kikubwa namna hii kwa graduates.

Wanasiasa wakikosa majibu sahihi ya kwanini kuna mass unemployment tunakimbilia kusema kuwa ni tatizo la kidunia bila kuangalia mahitaji halisi na mazingira yetu kama hii hoja ina mashiko.

Kuhusu teknolojia sisi hatujafikia kwenye high tech ya kuweza kutusababishia unemployment, stage tuliyopo ni teknolojia kuzalisha ajira nyingi zaidi badala ya kupunguza ajira.

Hii world wide problem theory ni faulty kwa mazingira yetu sisi
 
Dah, pole sana kaka na wengine wote ambao mnapitia hali hii. Niwaambie tu kuwa usiache kumuomba na kumshukuru Mungu kwa kila unalopitia maana yeye ndiye anajua maisha yako ya miwili na kiroho.

Nakuhakikishia yatapita na yote yatabaki historia.
 
Kama wanatakiwa kupambana tu, kuna haja gani kutumia kodi za wananchi kuwapa watu mikopoooo ya elimu ya juu ambayo mwisho wa siku elimu yao inabaki kwenye vyeti.
Basi kaa ukilaumu serikali ambayo haukusikii usitafute was kulaumu maisha ni yako boss hao wameshiba hata hawakufikirii
 
Graduates wa siku hizi hata kuandika hamjui, nani awaajiri? Enzi zet tunafudishwa kuandika insha... tunamaliza chuo tuko booked.. Ila poleni sana
 
nimekaa mikoani kwa miaka kumi sasa
hata huku shughuli ni ngumu si rahisi kama watu wanavyofikiria
lakini dar bado fursa zipo kibao kwa kuwa kuna watu wengi ambao wanamahitaji mengi hivyo ukijitoa ufahamu kidogo tu utauza.
Nikweli mkuu ila changamoto hutofautiana
 
Back
Top Bottom