Graduates wengi tunapitia wakati mgumu sana, sema jamii inaona kama hatujielewi

Nilipitia hali kama hiyo. 2011-2014, nimefanya Freelancing Bayport ServiceTz,Cliend Adviser Advans Bank.... orodha ni ndefu. All in all fanya chochote kiko kwenye uwezo wako upate kitu cha kufanya, muaminj MUNGU wako utashinda. Bottom line haijalishi unapitia changamoto gani, lakini hakuna kukata tamaaa
 
Jaman tusikatae ukweli wala kutupiana lawama, ajira za serikalini na kuajiliwa sehemu binafsi kwa kipato,/mshahara mkubwa Ni tatizo.
Vijana tufanye kazi, tujitume kujiajili wenyewe, na mtaji wa kwanza Ni nguvu zako mwenyewe.

Uhalisia wa Maisha Ni tofauti ukiingia mtaani, hakuna Cha bure Wala Cha dezo, Ni kukomaa tu na Maisha.

Shida graduate tunachagua Sana kazi za kufanya halafu tunataka kutusua mapema.
 
aiseeh kuna watu wana bahat, miez miwil tu, mi huu ni mwaka wa 5 bilabila daaah!
 
Ukweli Mkuu, kukata tamaa mwiko
 
Kweli mkuu.
 
Kwanza kushindwa biashara moja hakumaanishi kushindwa biashara zote.

Hata huko mkoani hakuna 'guarantee' ya kwamba utafanikiwa.

Jambo la msingi ni kujaribu "Tena na Tena"
Mkoani hakuna hela ya mzunguko kama Dar. Ndio maana makampuni yamejazana Old Bagamoyo road hapo kama HQ zao!
 
Ukiwa msomi utajificha wapi Tanzania hii?

Ukikimbilia ruvuma huko ndani ndani unauza miwa iko siku afisa vijiji umesoma nae atakuona tu
 
Sijui kwanini Dar kunalemaza Sana .yaani unahis huwezi survive kwingine!
Kiukweli mikoani maisha sio magumu kama Dar. Ila patakuchukua muda sana kusogea kimaisha tofauti na Dar. Ni ngumu sana kukusanya laki1 kama faida mkoani kama ilivyo kwa Dar.

Inabidi uwe na hesabu kali tu utumie hela kwa kubana ili ubakiwe na nyingi ya kusave ukiwa dar.
 
We acha tu mkuu, heshima huja kwa kuwa na kitu ktk haya maisha yetu ya kibongo
Ukikosa kazi bora hata uwe na kabiashara unaonekana unafanya, ila ukiwa unakula kulala tu aisee hata paka anaweza kukukojolea tu bila kuwaza.🤣🤣🤣

Kukosa kazi bongo ni kama gunia la msumari. Hamna mtu atakuheshimu hata uwe na PhD as long as haizalishi pesa umeisha.
 
Kaka umegusa Maisha ya wengi hata wachumba tunaogopa kutongoza yani ni shida mnoo
Ukitongoza mchumba utaishia kuachwa tu mkuu kwa fedheha nzito maana kila akiwaza utatusua umuoe wewe ndio unazidi kula mitama kwenye interviews na kazi hupati kabisa.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkoani hakuna hela ya mzunguko kama Dar. Ndio maana makampuni yamejazana Old bagamoyo road hapo kama HQ zao!
Asee mkoani hapana acha tubanane hapa hapa dar nyoso

Nilienda likizo juzi nikacheki mishe naona chenga tu, hadi nikajiuliza watu huku wanamake vip money

Arachuga hiyoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…